13 November 2009

Natamani Ningemwona,
Ili Nimjue Vema,
Nimwambie ya Maana,
Aziepuke Lawama,
Mficha Uchi Hazai,
Mtoa Uchi Hafai.


Lakini bahati Sina,
Karejea kwa karima,
Yuleyule maulana,
Mficha uchi hazai,
Mtoa uchi hafai.


Sababu isiwe haba,
Ahadi ijazwe kibaba,
Mtima wenye msalaba,
Mficha uchi hazai,
Mtoa uchi hafai.


Nenole Usilinene,
Jichole tena lisione,
Na sikio lisisikie,
Usiige kujua lolote,
Mficha uchi hazai
Mtoa uchi hafai.


Embe dodo natamani,
Kulila kwangu mdomoni,
Harara zangu za thamani,
Mficha uchi hazai,
Mtoa uchi hafai.


Nimelia sana maishani,
Katu siyashangai machozi,
Asilani liwazo si machozi,
Mficha uchi hazai,
Mtoa uchi hafai.


Maumivu yangu, huzuni yangu,
Tamaa yangu, furaha yangu,
Kipi kifaacho kwangu?
Furaha au huzuni yangu?
Mficha uchi hazai,
Mtoa uchi hafai.


Furaha na huzuni vi wapi?
Mwangu moyoni ama mwilini?
I wapi tofauti hii mpenzi?
Yako wapi yale mapenzi?
Mficha uchi hazai,
Mtoa uchi hafai.


Jamvi nalitandua,
Ukingoni nimetua,
Penzi sitolivua,
Kwako hakika nimetua,
Mficha uchi hazai,
Mtoa uchi hafai.

2 comments:

  1. umenikumbusha Lundo kulkuwa na migomba mingi sana.

    ReplyDelete
  2. Dada Yasinta, halafu fikiria jinsi hewa ya hapo ilivyo nzuri kwa afya ya binadamu na viumbe vingine. Hakuna moshi na uchafu kutoka viwandani kama ilivyo kwenye miji mikubwa. Angalia, hakuna makaratasi na mifuko ya plastiki iliyozagaa kwenye eneo hilo, kama ilivyo kwenye miji kama Dar au kando kando kando ya barabara kuu nyingi ambayo ni uchafuzi wa mazingira. Fikiria ubora wa vyakula vya hapo. Vyakula hivi vinakuzwa bila madawa. Kuku wa hapo ni wa kienyeji. Safi kabisa. Halafu ongezea na samaki, dagaa, na likungu. We acha tu.

    ReplyDelete

Maoni yako