18 November 2009

NILIPOJIFUNZIA KUOPOSHA SAMAKI 'MANDONGO'


Hishangazi kukumbuka wakati nikiwa mdogo huku tukiamka mapema yaani kujalawa kwenda ziwani siku za mwisho wa juma. Hili eneo la Makoro au Pamuhumu, ambapo tulikuwa tunatumia sehemu ya mwisho katika kuoposha samaki aina ya Mandongo.
Nakumbuka wakati huo zoezi la kuoposha lilikuwa gumu kwangu lakini yote yalifanikiwa tokana na jitihada za aliyekuwa akinifundisha kuwa mkali kama pilipili. Nakumbuka ukikosea tu lazima utachapwa makofi. Ukiona samaki anajongelea katika chambo yako lazima umweleze ili akufindishe namna ya KUKWECHEKA yaani kumuopoa toka majini. Unatazama mwelekeo wake na namna alivyoikamata ndoana mdomoni kwake kisha unafanya mambo matamu.
Nakumbuka wakati ule mwalimu wangu alikuwa Edgar Chumila a.k.a Chipota alikuwa mkakamavu na mpenda mazoezi. Alikuwa mkali kwangu kuhusu suala la mbinu za kuoposha hata mbinu za kuogelea. Ndiyo maana nashangazwa na watoto wa mjini wanaogelea huku wameziba pua zao, nawaambia mbona hili ni zoezi rahisi sana kwa mahali pasipo na dhoruba? Nakumbuka kwetu hapa nyasa dhoruba kali ilikuwa kwetu furaha ya kuogelea na kuonyesha ufundi huku tukicheza mchezo wa CHIMPYALI yaani unamkimbiza mwenzako ndani ya maji hadi umguse ndiyo anatakiwa kumtafuta mwenzake naye amguse.
Ilikuwa pouwa sana. Nakumbuka wakati fulani mwaka 1993 Chipota alinikosa kwa kofi zito baada ya kunielekeza namna ya kumwoposha samaki aina ya Mandongo aitwaye LINDONGO NGOKU yaani lindongo kuku. Nakwambia huyu samaki anapatikana sana muda wa saa sit mchana, ni samaki jeuri asiye na mfano achilia mbali LINGOMBOLI. Huyu anaweza kukumalizia chambo zako buree hata usimpate.
Lakini siri moja kuu ni kwamba anahusudiwa na wengi sana tena sana. Kama ilivyo kwa Lindongo Ngaka maana ni samaki wadogo lakini watamu sana. Hata wale wavuvi wa zana za kisasa wanasifia ujanja wa samaki hawa. Tukirudi eneo la picha hiyo ni kwamba palikuwa mahali ufukwe wake ulikuwa mashuhuri na bado mashuhuri tokana na wageni wengu waliopendelea kupumzika nyasa yetu hususani Lundu.
Moja ya sifa ingawa ni mbaya, kuota kwa majini ya Bangi ambayo ilikuwa ni matokeo ya jamaa mmoja aliyeitwa Edgar, mzungu ambaye alikuwa yeye na bangi ni kama chanda na pete. Alikuwa fundi bomba, lakini alikuwa mvutani mzuri wa bangi. Sasa eneo hilo linanikumbusha mengi sana hasa kwa wazee wetu kupatumia kama mahali pa KULANGA HIPA yaani kutazama dagaa huku nyavu zikiwa zimetegwa.
Sualoa la uvuvi na uogeleaji wa wanyasa ni jambo rahisi sana, na nakumbuka hata waliokuwepo katika msukosuko wa meli zetu zile wanakwambia wao hawaogopi maji lakini watu watokao mijini wana misemo yao ambayo inalenga kukatisha tamaa eti hakuna aliyemtalamu wa maji katika kuogelea. Huo ni uwongo kabisa. Nimekumbuka sana eneo hili, nimekumbuka nitokako, napenda sana hilo.

No comments:

Post a Comment

Andika maoni yako