11 November 2009

NIMERUDI; ZAWADI YAKO DADA YASINTA


Nimerudi. Ndivyo ninavyoweza kusema, maana ni siku kadhaa zilitoweka bila kuaga hapa ingawaje sina kawaida ya kuaga bali kutangaza wapi nimeibukia. Na aktika kuibuka huko kumbuka usiaambie uhamiaji suala hili kwani unaweza kuleta utelezi katika jitihada za kudanganya too ili liweze kunifanikishia mipango ya ukubwa . Si unajua danganya toto ni uwongo? Pouwa msomaji wangu.
Pamoja na kusema hivyo utashangaa huyu mzee wa Lundunyasa alikuwa wapi? Usijiulize hilo ila kumbuka mambo ya elimu mtaani bongo poa ila magumashi kwahiyo vuta pumzi vuka boda hata kama ni masikini wenzetu. Nimerudi kwa mtind uleule wa kawaida kama ilivyo mambo ya nyasa, na inawezekana ikawa mwanzo wasafari zisizokwisha kama ambavyo wakoloni wa kiingereza wasemavyo TRAMP. Mmmhh! nakumbuka nilikuwa na begi lenye neno hilo sababu yule rafiki yangu alipenda kuniita hivyo kwakuwa nilikuwa mtu wa mizunguko isokwisha.
Nipo msomaji wangu, nimekuja tena kama kawaida ingawa nitakuwa nawe mara chache, bila shaka shule na mwendo wa kuongeza shule unandaliwa ndiyo maana natoweka. Mipango mingi na hapa ni nyumbani kwangu nyasa sitoweza kuwakimbia. Najua kaka Mzee wa Changamoto atanza zake za kazi kulea mwana........ Lol
ZAWADI SIYO? Ni moja ya michezo mingi ninayoicheza katika hii tarakilishi wakati mwingine natumia majina yenu na picha zenu wanablogu kutengeneza vitu ninavyovipendelea.....
Lakini hii ndiyo ilinipa hamasa zaidi kwani ndiyo nilianza kuitengeneza na madoido ya kingoni.
Ni maalum kwa dada yangu kipenzi Yasinta Ngonyani a.k.a Nangonyani..... si unajua watu dadangu MUHEKELA PANGENDE KUMOYO LUTIMBA LONGI! unaona dadangu haya mambo? usiwatajie wala nini lakini najua wadadisi watachokonoa kama wachokonozi.
CHUKUA ZAWADI HIYO KWAKO NA FAMILIA. MUNGU MKUBWA, AMANI IWE NAWE.
karibuni sana Nyasa, na karibuni Mitindo huru kijiwe cha makala zangu za sasa na zamani ingawaje bado sijaweka mambo mazito. Tungojee mengi.

3 comments:

 1. Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti!11 November, 2009

  Aksante kaka, meseji sent and delivered!!!!

  haki ya mt simon unatisha...lol

  ReplyDelete
 2. Wow! akina Yasinta vamehele kweli Usengwili! na pia karibu tena.

  ReplyDelete
 3. Aaaah wenga kyani wenga eji kwa Yasinta Nangonyani mwana wa mzee gervas veve woliiiiiiii????

  ReplyDelete

Andika maoni yako