22 December 2009

ASANTENI WASOMAJI+WACHANGIAJI+ WANABLOGU= NAWAFIKIRISHA MAPENZI

Nimetulia tu hapa, labda nawaza kile nisichojua, lakini nimetulia baada ya kupokea ugeni toka Nyasa yetu, maana ndugu na jamaa walikwenda huko kuburudika, ni raha sana maana imewabadilidilisha kiasi chake. Kimsingi nyasa safi sana asikwambie mtu, au ukadhani mie mbishi wa kijijini najisifia tu kwalo. SASA.....pamoja na hayo ndugu yangu, mwenzangu nataka kukufikirisha kitu hiki ambacho niliwafikirisha sana pale Soma Cafe mgahawa wa vitabu mnamo mwezi Septemba pale Mikocheni
Niliwafikirisha sana kwasababu ya mda iliyojadiliwa kuhusu mapenzi, Kuna swali liliulizwa na binti mmoja huku akiungwa mkono na wenzake. Binti mwenyewe kwanza nilicheka sana, yupo kidato cha 3 pale Benjamini Mkapa Sekondari...eti kama anaye mpenzi wake, na anampenda sana, pia wakati huohuo mpenzi wake anataka wachunguliane uvunguni/kungonoka/kuongonoana (nadhani unanielewa) lakini yeye hataki anasubiri wakat muafaka. Cha ajabu ni kwamba pengine mpenzi wake anao wasichana wengine..... je afanyeje wakati yeye anampenda ingawaje hataka kungonoka naye?
KWANGU MIE;<>: ilipofika zamu yangu kumshauri binti huyo nilicheka kwanza, ili kuwapoteza maboya. Kwani niliona waziwazi ushauri unaopewa ni mwepesi au labda kwa kumwonea aibu ma kwa kulea watoto kisasa. Sasa nilitulia na kuanza kumweleza kuwa huo NI UJINGA na nikasema hana hoja ya kunishawishi kwamba yeye kwa wakati huo anajihisi kumpenda mpenzi hadi kuiathiri akili yake. Nilimweleza mimi kama msomaji wa saikolojia, nimesoma malezi, nasoma makuzi yalivyo ni upuuzi kuniambia au ningekuwa mzazi wako nikusikilize upuuzi wako...ningetulia ukoloni kumweka sawa.
Nilimwuliza maswali yafuatayo, ayajibu kabala sijampatia ushauri bingwa wa kufanya amweke mpenzi wake kati bila kungonoka na kuchunguliana uvunguni.NI HAYA NAKUFIKIRISHA NAWE MSOMA
1. UNATAKA MPENZI KWAKUWA YUPO2.UNATAKA MPENZI KWAKUWA UMECHOKA KUWA PEKE YAKO?
3 UNATAKA MPENZI KWAKUWA HUWEZI KUWA BILA MPENZI?
4. UNATAKA MPENZI KWAKUWA NI DESTURI?
5. AU UNATAKA MPENZI ILI UONEKANE?6.UNAAMINI UNAMPENDA MPENZI WAKO
7. HIVI KWANINI UNATAKA MPENZI?8. UNAMPENDA ILI IWEJE?
hayo ndiyo maswali yangu ambayo naona ni vema nawe msomaji nikakufikirisha katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka maana kwangu mimi tayari nimeshaanza kazi za mwakani. Hata hivyo nilimpatia ANGALIZO kuwa Baada ya hapo nilimpatia msimamizi wa mjadala wetu, kisha nikamweleza kazi kwenu, ninyi wazazi hamuwezi kuitikia porojo za huyu binti. PUNDE BAADA YA MJADALA.......ndiyo nini anauliza ninapoishi...duh! na mshikaji fulani naye akakaba mtoto akala naye sambamba...wakaanza mastori huku wameongozana kwa madoido...ndiyo nini tena tulipoondoka tupo kituoni...nadhani unajua kinachoendelea pale watu wanapokutana hivi wanapeana nini kwanza....Lol..... kazi kwako msomaji ni bora ukiona jinsia hizo jifanye umeona kichwa cha ahabri cha gazeti tu.................................................................. aaah ngoja nimsome zangu MALCOM X anipe stimu za kulalia leo

No comments:

Post a Comment

Maoni yako