08 December 2009

BLOGU MPYA+JUKUMU LILELILE =MWANDISHI YUELYULE


Nashukuru dada Yasinta likwisha kulitanabaisha ujio huo. Namshukuru kwani nilikwisha kufanya majadiliano naye siyo moja bali mara nyingi. Ingawaje nilikwisha kuelewa kuwa ili nisibanwe na mbano wa zama natakiwa kupanua kipaji changu cha Uandishi.
Nashukuru baada ya kuweka ujio huo kaka zangu walinikaribisha kwa moyo uleule walionikuta nao. Nasadiki kuwa jukumu langu la kusema mambo ya Nyasa ni sehemu ya kujizungumzia...na mara nyingi nimedokeza hilo.
Kilichobakia ilikuwa sehemu ya kutunza makala zangu mbalimbali ambazo nimekuwa nikizindika kwaajili ya magazeti ama nimekuwa nikiandika na kuhifadhi katika baruapepe yangu. Naamini sasa nitafungua mlango zaidi wa kujifunza mengi kwa kuweka makala zangu hapo.
Blogu yangu inaitwa FANANINYASA(FANANI+NYASA=FANANINYASA) Yaani msimulizi kutoka nyasa. Nakusudia kuweka makala hizo ili zitumike na wale tu ambao ninakubaliana nao kwamba wanaouhuru kuchukua makala yoyote na kuweka katika magazeti yao.
Sina mengi ya kusema kwani dada Yasinta alikwisha kusema kuhusu juio huo, nami nasisistiza kuwa karibu hapo MITINDO HURU-Mpe Maneno yake. Hapo naweza kwenda mstari kwa mstari bila kuvuruga kanuni zangu. Hapo najipambanua zaid namna nilivyo, uwezo wangu wa kuandishi na kuangali masuala mbalimbali ya jamii na dunia nzima. Nashukuru sana baba yangu kunifundisha siasa kabala sijaanza kusoma sayansi ya siasa.
Nawakaribisha nyote karbuni sana www.fananinyasa.blogspot.com, natarajia michango yenu katika kujenga tanuri la fikra. Dhima yangu ni kujifunza mapya toka kwa wengine, nasadiki mnayo mengi. Mzee wa Changamoto, nipe changamoto, na mungu wa wapare mtakatifu mkuu Kitururu. ASANTENI, AMANIIWE NANYI.

2 comments:

Andika maoni yako