04 December 2009

HELLOW1 WAUNGWANA MU HALI GANI?


Jamani waungwana, wasomaji, wanablogu mu hali gani? Mwajiandaaje na El Nino ijayo? Najua mwashangazwa na ujio wa asiyejulikana, lakini najulikana kwa huyu mwenye kibaraza chake mwenyewe hupenda kuita nyumba yake ya kujidai.

Mwashangaa nini? Leo nimevamia hapa tena kiungwana kabisaa na kusababisha mada iliyotakiwa kuweka hapa ikatupwa kando.... jamani ilikuwa mada nzuri kuwahusu wenye ukoo wao ulikotoka, ulianzia wapi, ulikwenda wapi, wahusika, koo zilizojigawa kutoka ukoo huo, na mengineye mengi.

Lakini nikaona hebu nifanye fujo hapa dada yenu napenda sana haya mambo lakini MUDA unakula mengi ambayo ningeweza hili. Lakini sisemi kama siwezi naweza sana, kwanza tangu Blogu hii inazaliwa niliona, siku ya mwanzo hadi ilipoendelezwa. Ilizaliwa na huyu kijana ambaye nimeamua leo kumnyang'anya mada zake.

Ujue msomaji na mwanablogu huyu kijana anaweza akatumia muda mwingi anasoma blogu, au mtandaoni..huko mitaani haoni jipya...mwache atapitwa na historia si unajua wabongo vijistori vimejazana? Nimeona tangu akianza kublogu halafu anapendelea blogu ya dada mmoja hivi, mwanzo sikumfahamu ila sasa nafahamu kuwa ni mwanablogu mahiri. kumbe ni mngoni mwenzake jamani..... ujue huyu kijana ni mkimya kama kobe lakini jeuri kama fisi maji.

Jamani nataka tu kusema endelezeni kazi zenu za kublogu ni jambo zuri, najua huyu jamaa akifika kuona haya niyaandikayo ataanza zake sababu anamsimamo kama papasi. Jamani nataka kusema dunia hii ni watu na watu ndiyo sisi. Nawasalimia tu leo kwani nimepeewa nafasi ya kujimwaga hapa.... aku! ninakazi zangu nashindwa kupata muda wa kublogu. Namwachia dogo huyu ajifurahishe maana ameoa mtandao na mtandao umemwoa.

haya Wikendi njema waungwana, na wale wapenzi wa kunywa nafahamu mtakuwa mnajua wapi leo iko siku na mwisho wa wiki..........., he sijataja jina langu? Mtanisamehe sana naitwa Dada H.

5 comments:

  1. Ya leo kali. Usengwili dada H kwa ujumbi wabwina.Na chilawu mewawa.

    ReplyDelete
  2. Ya leo kali, huyu dada kazunguka zunguka mwisho katusalimia tu, lakini nahisi kuna kitu anataka kusema............tusubiri

    ReplyDelete
  3. Monile! eeh, chinyaee. te tipala kumanya uloweka wa nani? Kun'hanga kola uhumii kwako?

    ReplyDelete

Maoni yako