Hii nayo ni kama vile ujuavyo kula na kulala au kupenda na kupendwa. Pengine unajua kuwa tunajua haya mambo. Jamani sijui unawaza nini, au mimi ndiyo nawaza nini. Sijui labda UA alangu, thubutu mmhh pengine. Lakini Koero aliuliza kuhusu picha fulani kuhusu mimi. Eti hii nayo vipi, kweli mimi nipo au? Sijui, lakini haya ndiyo maisha yetu tunatafuta shibe, furaha na pumziko. karibu sana.January 24, 2009
ndiyo kazi zetu, ndiyo utamduni wetu
Hii nayo ni kama vile ujuavyo kula na kulala au kupenda na kupendwa. Pengine unajua kuwa tunajua haya mambo. Jamani sijui unawaza nini, au mimi ndiyo nawaza nini. Sijui labda UA alangu, thubutu mmhh pengine. Lakini Koero aliuliza kuhusu picha fulani kuhusu mimi. Eti hii nayo vipi, kweli mimi nipo au? Sijui, lakini haya ndiyo maisha yetu tunatafuta shibe, furaha na pumziko. karibu sana.
Madhumuni
kumbukumbu,
maisha,
Nyasa,
urafiki,
wageni
January 22, 2009
tunaweza, ndiyo mapenzi yetu

hapa hakuna kuremba wala kuleta utata. Vipi unatuonaje tulivyo? Tunafanana na wengie au siyo, lakini kweli si unajua maisha ni tofauti au? poa basi angalia sana tena mpaka picha itoboke halafu nipe jawabu
Madhumuni
kumbukumbu,
maisha
January 21, 2009
nimepoteza ua langu,nalia
Nimepoteza UA nilipendalo, nilisudulo daima. Nimepoteza UA langu kipenzi cha MOYO wangu, upepo wenye nguvu umenipora, wenye harara wamechukua kwa madai nilishindwa kulipenda UA na kulitunza. Najua nalipenda UA langu tena sina mfanowe lakini najuta mimi mwana wa nyasa, mhafidhina, Mnyasa aishie maisha ya kizamani, fikra za kale. Si wajua mahaba ya sasa, uwe kama kumbikumbi, UA langu nalia niwazapo nakonda, sijui nifanye nini waungwana nipeni pole, nishikeni mkono, nitaanguka.
Najua nalia, najua naumia, najua nakonda, najua chakula kibaya kwangu na mwili wangu watetereka, nahojiwa maswali, muungwana kulikoni? Mbona uso umejaa soni kama siyo huzuni? Najuta sana mimi, nalia sana mimi, najua ukimya wangu na mwenendo wangu hauna faida kwa maisha ya kisasa. Kweli nina kasoro zitajwazo, kweli najua ninazo lakini UA langu lijualo limepotea, UA lijualo udhaifu wangu limekwenda mbali nami kwa yule nimjuaye.
Ua langu lijualo kasoro hizo limekwenda ughaibuni, wengine wenye vipawa vya kuonjesha asali za huba wamenyakua bila suluba kwa tiketi ya mateso ili waepukane na maumivu. UA langu linaondoka leo ni siku ya pili, nakiri nilibaini kitambo ila ukimya kwangu silaha, nilijipa moyo licha ya kujua nimebaini. UA langu limetoweka, moyoni nasononeka.
Kwa hali hii, binadamu gani asoweza kurutubisha UA lake alipendalo? Kwanini ujualo ni kosa usilipatie tiba ikiwa yawezekana? Tiba ni kupeperuka, kuniswaga kondeni kwa mafarisayo na wayahudi waua wenzao? Tiba ya kidonda ni kukata mguu au kutibu kidonda, Aaaaaah nakumbuka maeneo ya wahenga, walotujuza kale kwamba ISHI kwaajili yako, furahia maisha yako. UA langu linanipa furaha lakini leo napata simanzi, sioni raha, najua sababu lakini kinywa kinapiga KITE wala AFANALEKI sizihitaji bali nataka UA langu, kikohozi changu. SWALI: Ukiwa na kidonda mguuni unakata MGUU au unatibu kidonda?
Ooooooooooohhhh UA langu limeponyoka, limekwenda mbali limechukuliwa na wenye uwezo wa kushaini HUBA, wenye vipawa vya HAMU. masikini mimi, nalia mwenyewe sina msaidizi UA langu limetoweka. Ukijua una homa, unafanyaje? Utajiua kwakuwa hutaki homa au utapata TIBA? Nakulilia UA langu, rudi kwangu, rudi nyumbani!
Natulia kidogo na wimbo wa IT'S NOT EASY
Jamani ile makala ya 'DINI INAPOTUMIWA KAMA KITEGA UCHUMI' imetoka jana jumanne januari 20./2009 katika gazeti la TAZAMA Tanzania

amani na upendo,
Hisia za moyo,
maisha,
mapenzi
January 19, 2009
naona upo karibu yangu
upo karibu au mbali, umewahi kufanya haya tufanyayo? Si mengine ni kuvua tu samaki na kuoposha vindongo hapa nyasa. Karibu nyasa, uwe nasi daima, unatuonaje sasa
Subscribe to:
Posts (Atom)