January 26, 2009

Baridi sana, Nipo Mbeya

Duh! Hii hali bwana we acha tu! Nipo Mbeya jamani, mapumziko ya siku saba hivi lakini naamini kila kitu kinakwenda kama ninavyopanga na ninavyotaka bila kujali ni namna gani nakarahishwa na hii hali. Baridi inanikamata halafu hakuna hata chembe ya faraja, duh! labda kama alivyonipatia wimbo Keoro kuwa niskilize wimbo wa Ziggy Marley.
Jana nilikuwa njiani kuja hapa, mvua, kumbukumbu za maisha yangu ya shule, mitikasi na vioja vya hapa na pale. Mji umekuwa na mabadiliko ambayo naamini kama jiji limepiga hatua kiasi fulani tofauti na mwenendo wa maeneno ya Dar kwenu.
Vipi wanablogu mnaonaje kadiri siku ziendavyo mnafikiria nini kuhusu blogu. Najua wapo wajuaji wa blogu na wale wajuao mchanganuo wa hoja, huku wakipendacho kiwepo ndicho wafanyacho kwakuwa wanajua wafumbacho ni huishia ubongoni mwao! Aiseh!
Tafadhali usiwaaambie uhamiaji kama kesho naingia zangu Malawi kwanza kwa rafiki yangu. Duh! Hii inakuwa ngumu sijui lakini uhamiaji usiwaambie kwani nina kitambulisho cha maktaba tu sina kitu kingine.
Haya, lakini bado nawaza mambo ya mlimani akili imekufa ganzi. Kwaheri kwa leo jamani ila usiwaambie uhamiaji kama kesho navizia kuingia Kalonga kisha ndani ya nchi kabisa.
Pamoja daima! Baridi sana, mapumziko safi-nasonga kwa wajomba unyanjani.

January 24, 2009

ndiyo kazi zetu, ndiyo utamduni wetu

Hii nayo ni kama vile ujuavyo kula na kulala au kupenda na kupendwa. Pengine unajua kuwa tunajua haya mambo. Jamani sijui unawaza nini, au mimi ndiyo nawaza nini. Sijui labda UA alangu, thubutu mmhh pengine. Lakini Koero aliuliza kuhusu picha fulani kuhusu mimi. Eti hii nayo vipi, kweli mimi nipo au? Sijui, lakini haya ndiyo maisha yetu tunatafuta shibe, furaha na pumziko. karibu sana.

January 22, 2009

tunaweza, ndiyo mapenzi yetu


hapa hakuna kuremba wala kuleta utata. Vipi unatuonaje tulivyo? Tunafanana na wengie au siyo, lakini kweli si unajua maisha ni tofauti au? poa basi angalia sana tena mpaka picha itoboke halafu nipe jawabu

January 21, 2009

nimepoteza ua langu,nalia

Nimepoteza UA nilipendalo, nilisudulo daima. Nimepoteza UA langu kipenzi cha MOYO wangu, upepo wenye nguvu umenipora, wenye harara wamechukua kwa madai nilishindwa kulipenda UA na kulitunza. Najua nalipenda UA langu tena sina mfanowe lakini najuta mimi mwana wa nyasa, mhafidhina, Mnyasa aishie maisha ya kizamani, fikra za kale. Si wajua mahaba ya sasa, uwe kama kumbikumbi, UA langu nalia niwazapo nakonda, sijui nifanye nini waungwana nipeni pole, nishikeni mkono, nitaanguka.

Najua nalia, najua naumia, najua nakonda, najua chakula kibaya kwangu na mwili wangu watetereka, nahojiwa maswali, muungwana kulikoni? Mbona uso umejaa soni kama siyo huzuni? Najuta sana mimi, nalia sana mimi, najua ukimya wangu na mwenendo wangu hauna faida kwa maisha ya kisasa. Kweli nina kasoro zitajwazo, kweli najua ninazo lakini UA langu lijualo limepotea, UA lijualo udhaifu wangu limekwenda mbali nami kwa yule nimjuaye.

Ua langu lijualo kasoro hizo limekwenda ughaibuni, wengine wenye vipawa vya kuonjesha asali za huba wamenyakua bila suluba kwa tiketi ya mateso ili waepukane na maumivu. UA langu linaondoka leo ni siku ya pili, nakiri nilibaini kitambo ila ukimya kwangu silaha, nilijipa moyo licha ya kujua nimebaini. UA langu limetoweka, moyoni nasononeka.

Kwa hali hii, binadamu gani asoweza kurutubisha UA lake alipendalo? Kwanini ujualo ni kosa usilipatie tiba ikiwa yawezekana? Tiba ni kupeperuka, kuniswaga kondeni kwa mafarisayo na wayahudi waua wenzao? Tiba ya kidonda ni kukata mguu au kutibu kidonda, Aaaaaah nakumbuka maeneo ya wahenga, walotujuza kale kwamba ISHI kwaajili yako, furahia maisha yako. UA langu linanipa furaha lakini leo napata simanzi, sioni raha, najua sababu lakini kinywa kinapiga KITE wala AFANALEKI sizihitaji bali nataka UA langu, kikohozi changu. SWALI: Ukiwa na kidonda mguuni unakata MGUU au unatibu kidonda?

Ooooooooooohhhh UA langu limeponyoka, limekwenda mbali limechukuliwa na wenye uwezo wa kushaini HUBA, wenye vipawa vya HAMU. masikini mimi, nalia mwenyewe sina msaidizi UA langu limetoweka. Ukijua una homa, unafanyaje? Utajiua kwakuwa hutaki homa au utapata TIBA? Nakulilia UA langu, rudi kwangu, rudi nyumbani!
Natulia kidogo na wimbo wa IT'S NOT EASY

Jamani ile makala ya 'DINI INAPOTUMIWA KAMA KITEGA UCHUMI' imetoka jana jumanne januari 20./2009 katika gazeti la TAZAMA Tanzania