Duh! Hii hali bwana we acha tu! Nipo Mbeya jamani, mapumziko ya siku saba hivi lakini naamini kila kitu kinakwenda kama ninavyopanga na ninavyotaka bila kujali ni namna gani nakarahishwa na hii hali. Baridi inanikamata halafu hakuna hata chembe ya faraja, duh! labda kama alivyonipatia wimbo Keoro kuwa niskilize wimbo wa Ziggy Marley.
Jana nilikuwa njiani kuja hapa, mvua, kumbukumbu za maisha yangu ya shule, mitikasi na vioja vya hapa na pale. Mji umekuwa na mabadiliko ambayo naamini kama jiji limepiga hatua kiasi fulani tofauti na mwenendo wa maeneno ya Dar kwenu.
Vipi wanablogu mnaonaje kadiri siku ziendavyo mnafikiria nini kuhusu blogu. Najua wapo wajuaji wa blogu na wale wajuao mchanganuo wa hoja, huku wakipendacho kiwepo ndicho wafanyacho kwakuwa wanajua wafumbacho ni huishia ubongoni mwao! Aiseh!
Tafadhali usiwaaambie uhamiaji kama kesho naingia zangu Malawi kwanza kwa rafiki yangu. Duh! Hii inakuwa ngumu sijui lakini uhamiaji usiwaambie kwani nina kitambulisho cha maktaba tu sina kitu kingine.
Haya, lakini bado nawaza mambo ya mlimani akili imekufa ganzi. Kwaheri kwa leo jamani ila usiwaambie uhamiaji kama kesho navizia kuingia Kalonga kisha ndani ya nchi kabisa.
Pamoja daima! Baridi sana, mapumziko safi-nasonga kwa wajomba unyanjani.