February 06, 2009

ndiyo maana nakupenda sana

Daima nawaza, nakumbuka enzi za uvuvi bwana,kabla sijajua kubonyeza niandikacho. Mmmmhh Koero aliagiza samaki, akadai anahitaji Kamongo, DUH! Pengine sijui hawa samaki wapo wapi lakini sijui kama ziwa letu lina Kamongo. Mmmhh labda nimesahau mambo yetu. Haya weeeeee tayarisha ugali mimi naandaa mboga, wala usilete kitu tofauti na ugali tena wa muhogo.

February 04, 2009

Rahaaaa sanaaaaa

Sijui labda unatupenda ila husemi.

Pengine unaweza kutuambia lolote, unaweza kutafsiri chochote lakini sisi ni kama wewe, tupo pamoja nawe daima! Vipi unawaza nini utuonapo, au kuna lolote unajifunza? Tulia mwenzetu ule kwa raha, usafiri kwa raha wala usitie shaka, kwani ile gari yako unaweka mafuta lita ngapi na kwa shilingi ngapi?
Maana hapa tunakula kwa dola moja siku nzima. Si unaijui BUKU au elfu moja, wenzio tunatumia kwa siku mpaka inabaki kwaajili ya kesho, siku ambayo tutaongezea nyingine ili itimie kama ile. Tunafurahi, tunaridhia maisha yetu, wala hatutaki kukaa eneo lenye maandishi '"mbwa wakali" au "eneo hili linalindwa kwa mitambo maalumu".
Wala kwetu hatuna walinzi tuwalipao kwa miezi 12. Pengine unadhani siye wanyonge! unajidanganya, tunauwezo kuliko wewe unavyodhani, tunaweza kutenda na kuenenda kama wewe lakini tumetulia kwa raha na tabasamu utuone kwanza! Vipi unaonaje!

February 03, 2009

Ukishiba, msome Richard Wright

Kama utashiba bila mboga au kama imekwisha basi msome Richard Wright maneno yake haya " Hatari inayoukabili ulimwengu wa leo ni kusahau kile kiainishacho ubinadamu wetu. Maana halisi ya mahusiano, maana halisi ya mapenzi, hata ile heshima na hadhi ya maisha ya binadamu inaelekea kusahaulika. Kipimo cha utu si utu tena bali mienendo na tabia za kikatili na ufisadi.
Leo hivi mapenzi ni neno lililobadilika maana yake, sasa mapenzi ni uhusiano wa mtu na gari au mali yake.
Neno utu limebadilika kabisa maana yake na kuwa utukufu na ubinadamu ukawa ubwana damu hata damu imekosa thamani ya asili na utakatifu!

wale wasomi wetu vipi,inapendeza eeehee!!!

Vipi waungwana mwadhani nimepotea kilingeni kwangu? Duh1 nipo nipo sana, yaani nipo nipo kama vile ujuavyo nipo1 Lakini sijui unaonaje hii kitu, au nisme unaonaje haya maudhui ya picha. Haya weeeeee!!!