February 11, 2009

Shindano! KITENDAWILI........

KITENDAWILI........................................., "Ni CHEUPE kama barafu na ni CHEUSI kama giza, KULIWA ni HARAMU na kunywa ni HALALI, kina herufi 5 na kinaanza na herfi M.
Kinatumiwa na WANAWAKE mara moja katika UMRI wao, na kinatumiwa na WANAUME mara tatu kwa siku.
Je, ni kitu gani hicho? Ukipata jawabu lake.

NB: ZAWADI NONO kwa mshindi

Hakuna kulala hapa

Vipi, unaonaje ukijiunga nao! Unaweza kweli mauno ya viuno kama Fifimoto wa Enomizizi au wewe ni laini yaani nyororo! Utaweza wewe mtoto wa geti kali mambo haya? Mtoto umekulia wapi kama siyo ndani kutazama kideo na propaganda za seleka za walami ughaibuni.
Nakumbusha umuhimuwa kunengua mitindo ya kwetu, hakuna kulala aiseh

February 06, 2009

ndiyo maana nakupenda sana

Daima nawaza, nakumbuka enzi za uvuvi bwana,kabla sijajua kubonyeza niandikacho. Mmmmhh Koero aliagiza samaki, akadai anahitaji Kamongo, DUH! Pengine sijui hawa samaki wapo wapi lakini sijui kama ziwa letu lina Kamongo. Mmmhh labda nimesahau mambo yetu. Haya weeeeee tayarisha ugali mimi naandaa mboga, wala usilete kitu tofauti na ugali tena wa muhogo.