February 20, 2009

Kikwete acha kupiga Mayowe


Nimetulia wala sijaandika maoni yangu kuhusu ujio wa Hu Jintao wa China. Nimtumiwa sms nyingi na waraka pepe kwamba ninaonaje ujio huo na kauli zako kuhusu Mkapa. Wengi wanadhani nimebadilika kimtazamo kwani kuna mambo siyajadili,sipendekezi au kuongoza njia.BADO NIPO SANA!
Wapo wanaolalamika kwamba nimeacha kujadili mada zangu za kuhusu bara la afrika, wanadai ninapwaya katika mada za nyumbani bongo. Lakini nasema kuna mambo yanaingiliana, kwasasa nakula darasa kali sana kuhusu mashariki ya kati na yanayowahusu, pia na shughuli zangu za maisha.
Sasa ninaandika hapa kama mwanzo tu kwani natarajia kuandika wazi zaidi. Sikubaliani na mtazamo au porojo za Rais Kikwete kwamba uwanja taifa ni juhudi za Mkapa na uzuri wake. Mimi nasema ni juhudi za watanzania, kwani hakubuni bali aliahidi kwasababu ni wajibu wake kuteda hivyo.
Sasa basi kutwambia kwamba hayo ni mazuri yake ni kutulazimika kunya mavi jamvini huku msosi upo tayari kwa kuliwa. Sikubali kwamba mambo machafu ayaliyoyatenda eti yamekuwa mazuri na kupakwa rangi au marumaru. Kwanza nitakumbusha BOT ujenzi wake.
Bodi ya wahandisi nakumbuka ilifanya tathmini na kusema kwamba ni bilioni 56 zingtosha kujenga BOT tena bila msaada wa nchi yeyote, lakini uwongo ukatungwa halafu tukaambiwa BOT imejengwa kwa milioni 700 huku mjenzi wake alitaka milioni 70. Je nini kilichofanywa hadi ikapandishwa bei kiasi hicho? Au unadhani uzuri wa mtu husemwa tu kama ufanywavyo wewe?
Huo uwanja wa soka nani amekwambia Watanzania hawajui uzuri wa mtu? Watakula uwanja na kunya uwanja? Ingawa kwa wapenda soka tunafurahi, lakini nguvu ya kushangilia tutoe wapi? Ni kweli kulikuwa na umuhimu wa kumpamba tena Benjamini? kwa sababu naamini ni jukumu lake na tulimtuma kufanya kazi kwa ajili yetu full stop! Sasa unapopiga mayowe eti jamaniiii mkapaaaa alijenga uwanja huuuuuuuu.
Nini thamani ya mgodi wa Kiwira ambao ulikuwa na Milioni 700 halafu wakijiuzia na Yona Milioni 70? Au unadhani kila mtu kipofu, haoni anakubali kuchekewa na kulishwa porojo kama zile ulizozitoa uwanja wa taifa. Unafikiri wenye kiona mbali tunajali kwamba eti Hu Jintao alikuja kuzindua uwanja? thubutu labda wajinga wajinga watachekelea mpaka kupasuka misamba ya midomo halafu wasijipe muda wa kufanya tafakuri.
Kwani nani hajui mashtaka mengi yaliyopo ni porojo na ngebe za uchaguzi? Unafikiri tunafundishwa uzuri wa mtu kwa hotuba au matamko? Sikiliza wahenga walisema 'mtoto acha kupiga mayowe, acha watu waone wenyewe'
'usiseme sana kwani tusiposema hatumaanishi hatuna ila tunakutazama tu ili tujue umahiri wako wa kuchanganua hoja.
Amka, hujasikia kama ni kizazi cha dhahabu cha Nyerere kinakuja, hujui. Zubaa uchekwe. Nitajadili zaidi nje ya blogu.