May 21, 2009

Kikao cha Dharura kuhusu NYASA

nilipotea kidogo, lakini nilikabiliwa na kikao kizito na muhimu zaidi kuhusu NYASA. Nambukuka mwanzoni mwa mwaka huu mzee wangu Profesa Joseph L.Mbele alinishauri kuhusu kuandika kitabu kuhusu nyasa. Nililipokea wazo lake kwa mikono miwili huku rafiki yangu koero akisisitiza jambo hilo.

Hata hivyo naweka wazi kwasasa kuna kikao kizito kuhusu nyasa, kikao ambacho kinaendeshwa na wanafunzi wa vyuo vikuu ambao wametoka katika ukanda wa nyasa. Kikao hicho kinazungumziaq maendeleo ya maeneo hayo na namna ya kuanzisha umoja ambao utawezesha jamii za nyasa kielimu,siasa, na uchumi. Jambo hili nashukuru linafanyika huku wazo la mzee Mbele likiwa mezani kwangu.

Jumapili iliyopita kulikuwa na kikao hicho, tulijaribu kuweka ama kuorodhesha kero na mambo mazuri ambayo nyasa tunayo na tunaweza kuwafaidisha wakazi wake. kikao hicho naweza kukiita NYASA DEVELOPMENT ORGANISATION. ni wazo ambalo tumeamua kwa moyo mmoja kujitolea kwa kuanzisha kikundi hiki kwa nia ya kuendeleza wananchi wa amaeneo yetu.

Kikao hiki cha kwanza kimefanyika huku wahudhuriaji wake ni BARAKA WANDAWANDA, HELLEN LOCHI. LAWRENCE EMANUEL, BONIFACE MNDALA, EMMANUEL NAMINGA, RICHARD MWANJA, VENANT KATOPOLANGA, SIMON HARRISON, FRANK NDOMBA, FRANK MAPUNDA, na LIBADA MAPUNDA pamoja na MARKUS HONORIUD MPANGALA.

Sisi siyo mwsho bali wenzetu wengine walikabiliwa na majukumu ya chuo, kwahiyo tunaamini kikao kijacho cha jumapili wiki hii kitakwenda katika mpangalio uleule. jitihada ni kubwa na ari yetu ni kubwa sana kwani kikundi hiki kinaundwa na vijana ambao wastani wa umri wetu ni chini ya 25. Tumedhamiria na tunahakika lengo letu litafanikiwa.

Mipango yetu ikiwa katika njia sahihi nitawahabarisha zaidi ili mjue dhamira yetu watoto wa kinyasa kuwa tunataka kufanya nini katika ukanda wetu na watu wetu. Kundi hili linakaribisha mwanachama yeyote ambaye anaweza kukiboresha na kusaidia mambo mbalimbali hususan mchango wa mawazo ambao ni muhimu sana. Vilevile ingawa ni suala binafsi sana lakini nawaomba Raiton Mbele(Ukraine), Robert Ngalomba(UK) na mzee wangu Mbele kuwa mchango wenu ni muhimu sana. Yasinta Ngonyani(sweden) nawe pia tunaamini kuwa upo pamoja nasi. Pia Mzee wangu Prof Mbele ningependa na nitakupendekeza uwe mlezi wetu iwapo nafasi itakuruhusu kwani mchango wako ni muhimu sana. Jumapili iyajo(juma hili) tunakikao cha pili ili kufikia maazimio yetu.
Tunakaribisha kila ya aina ya mawazo yenu wanablogu wote bila kujali ukanda wala mahali ulipotolea bali tunachofanya ni kujaribu kuwezesha jamii zetu. Sasa ninajikita katika kujitolea kwa jamii rasmi bila malipo. Tunawakaribisha sana nyasa.

May 16, 2009

HAPPY BIRTHDAY MARKUS II

Nawashukuru wanablogu wenzangu, nawashukuru kwa kila namna yaani hadi chozi linadondoka, nawakumbuka zaidi ninyi kwani mnanifanya nijue kwamba wapo watu wanaonijali zaidi. Koero Mkundi uko wapi mziwanda wangu?, u hali gani huko mafichoni??????
Amini upendo mtamu
kama salamu tamu
kwakoFadhy wangu
Wanipa hamu hamu
Mtanga wangu, asante daima
Uso wapwita chozi,rabana ajua
Nionacho, u mwanamalenga
Hakika nakusujudia
Dhima yako idumu,milele
Maisha yangu kama tetere
Naishi bila kelele,nisonge mbele
U wapi koero wangu
U wapi pacha wangu
Kilio waona humu?
Nione kwa tonge au saumu.
Asante Changamoto, nipo mjini
jogoo la shamba mie,siwiki mjini
mtandaoni nipo,mjini nyingi dili
asilani sitokwacha,niamini
Nawasalimu kwa hamu
sina simile wala gubu
Nawapenda ninyi,mdumu
sijafunga kufuli,mlango u wazi
Jasho la majukumu, lakula muda bloguni
Wape hi Marekani na mashariki ya mbali
Waambie bongo twaishi mambo ni shwari
Asante Yasinta,kwa siku yangu
Kumbukumbu najivunia wangu
Usijali tupo sawi,tudumu
Asantedada weshi, ukarimu udumu
Usumbufu ulokubali,kunikirimu
Ahadi yetu itadumu,daima idumu
mungu mkubwa waungwana
Nimetembelea maduka ya vitabu pale Afrikasana kwa dada Weshi Lema kisha akanipeleka Mikocheni pale mtaa wa Regent, nikajipatia kitabu cha "PESA NA MAWE" kitabu kizuri nimekipenda, nashukuru kwa wote mliopo nami kwa kila dakika, kaka Simon mkodo Kitururu naamini tuko pamoja daima.
Nawashukuru nyote nawapendeni sana, hata kama sijakutaja najua hapa ................................. utaandika jina lako.
Dada Yasinta kwa kila dakika ya kunijulia hali na kujua siku yangu nashukuru sana. Digna, Manka na wengine. Nawapenda sana, upendo utadumu kama samaki na maji ingawa malaria yalinisumbua lakini sikuacha kwenda dukani kujinunulia kitabu. nitaandika kile nilichojifunza baada ya kwenda katika maduka hayo na ukweli wetu watanzania.

May 15, 2009

"HAPPY BIRTHDAY MARKUS"


Hongera MARKUS HONORIUS MPANGALA, mwana wa nyasa umpendaye MALCOM X kila leo au JENERALI ULIMWENGU na JULIUS NYERERE, amani kwao watu hawa!
UPENDO UWE NANYI
Nashukuru baba na mama
Kwa kunileta hapa duniani
Nami najivunia kuishi ndani
Nashukuru sana wangu maanani
Kwani yupo nami kwa shida na raha
Kama machozi na majonzi naamini yanapita
Nashukuru ndugu waliopo hai
Na wale wasiohai, nawapenda kikweli
Upendo wangu, zaidi ya mshumaa
Nitawaangzia kwa uwezo wangu daima
Ningali nawajali, upendo usiopimika
Kwani ni tunu yake maulana
nawashukuru marafiki zangu nyote
Bila ninyi nikiri siyo mwenyewe
Najua imani yangu nimejaza kibaba
Naamini mola yupo nasi daima
Anajali,kutulinda na kutuhusudu
Ndiyo maana avumilia wetu utundu
Nawashukuru enyi wapenzi mlokuwa nami
Nawapenda kama amri ya mola
Kwani ni agizo la thamani daima
Nipo nanyi kwa mapenzi ya maulana
Nawashukuru maadui wote
Kwani mnanifanya niwe kama nilivyo
Bila ninyi sitokamilika, nawapa upendo
Mungu mkubwa.
Ni siku yangu ya kufurahia kuzaliwa kwangu, nashukuru wanablogu wote mliopo karibu nami. kwa pamoja tuseme waweke upanga au shoka au kufa ama kupona-mtaani tutabanana kwa pamoja tutafanikiwa kile kinachotakiwa kufanikiwa.
Na kwa yule mke/mchumba/mpenzi/demu n.k, ingawa nanua hujui kama wewqe ndiwe ninayekuhitaji. Labda hujui kama wewe ndiwe ninayependa uwqe demu/mchumba/mke wangu, lakini leo ujue ni siku yangu ya kuzaliwa.
Ingawa leo malaria yamenibana lakini nashukuru manesi ingawa wameshika matako yangu na kunidunga sindano. Najua kwa nia njema nitapona ndiyo maana ukichomwa sindano takoni unaambiwa poleeeeeee, ingawa nilisahau kumjambia ili nimwambia nami poleeeeee.
Najua kila mmoja anayozawadi yake lakini Koero Mkundi sijaona zawadi yako, unabifu na mimi au? Nashukuru Yasinta Ngonyani, zawadi yako nimeipenda sana1 daima tupo pamoja! OOOOhhh kwa wazee wangu nawaambia mjue mtoto wenu ni mwingi wa utani, mnivumilie ninaposema nesi amechezea TAKO langu. nadhani mnajua mambo ya kutaka uzima
LAKINI
atakayeweza anitunuku kitabu cha THE WORLD IS FLAT cha Thomas Friedman, nimtafuta hadi najamba. Mwenyewe ninacho mknoni JULIUS KAIZARI na CRYSTAL RAPTURE pia nakwenda duku la vitabu sasa kujinunulia zawadi. Bwaya, Kaluse,Kamala, na wengine naweka ..................................... ili ujaze jina lako kama nimesahau.
upendo daima, salama kwa mchumbangu usiyejijua kama ni wewe, naweka ........ andika jina lako