June 02, 2009

KUSOMA> Mkononi ninaye YASSER ARAFAT

Pamoja na harakati au mchakamchaka wa maisha na shule kunibana kwa mitihani miiiiiiiiingiiiiii, lakini sijaweka kando jambo hili. Ninaye mkononi Yasser Arafat nakula nondo zake, najielimisha. Lakini bado kitabu cha Prof Mbele ninahamu nacho sana tena sana.
Sasa nadhani mambo ya mzee wangu Freddy Macha na semina za ujuzi zimekwisha, nimefaidika nimejifunza, tunmeongea mengi, tukafurahi na kupiga gumzo la hapa na pale. Vilevile mkononi ninaye TOM CLANCY katika THE CARDINAL OF THE KREMLIN. haya msije mkasema nimeacha kuvua samaki na kuvamia kusoma. Mimi na samaki ni kama mizizi na ardhi. KOERO mwana wa MKUNDI upo hai au umekumbwa na KIDELI maana siku hizi duuuh! haya mambo ya aiseh! ha ha ha ha

BURIANI> wana PAN AFRICANISM na PAN LOCALISATION

Tangu juma lililopita nilijulishwa na rafiki tangu wa karibu aliyeko nchini Kenya. Alinidokeza saa chache baada ya ajali iliyomwondoa mwanamapinduzi huyu na mwezeshaji wa MDs pale jijini Nairobi. Ni TAJUDEEN ABDUL-RAHEEM. kwa hakika nitazikosa kazi zake nyingi katika medani za uchambuzi wa mambo ya kiafrika, nitakosa na na kusikitika kama nilivyosikitika kwa muda wa juma zima huku nikitafakari kuwa kifo ni kitu gani. Lakini mwanafalsafa Socrates anatuonya kuhusu kuogopa kifo ni ujinga kwa kudhani tuna busara kuliko mungu.
Juma zima nilikuwa najaribu kuwaza kuhusu mwanamapinduzi huyu na ajali iliyomtoa duniani. Mungu mkubwa yupo nasi, kama ajali ni majaliwa yake basi hatuna neno,lakini kama siyo majaliwa yake basi tunazidi kumwombea mema. AMEN