05 January 2010

KILA LA HERI, ELEWA NIKO NAWE


Nimerudi jiji la Joto, nimerudi huku nikikumbuka mikasa niliyokutana nayo jamani we acha tu. Honera Yasinta, hongera zaidi ya maneno ninayoandika.....ni zaidi ya unachokisoma hapa. Na daima tutakuwa sote hata katika majilio ya matatizo, kwa maana mwana wa adamu wa wkristo alisema Torati hatalivunja, atakuwa nao daima. Nakupongeza kwa miaka kadhaa uliyonayo, tatizo husemi una miaka mingapi wewe binti! Lol na cha ajabu unatukumbusha enzi za picha za kucheza kombolela, rede> Mweee iko kazi.
Unapokumbuka siku ya kuzaliwa unakumbuka pia mateso ya mama yako, unakumbuka namna alivyokutunza kwa upendo, ujasiri na matumaini kuwa utakuwa mtu kama ulivyo leo na wengine walivyo ingawaje wanatofautiana busara ama hekima ingawa sote tuna ubongo uleule.
unapokumbuka siku ya kuzaliwa unakumbuka na kuyatazama maisha yako kwa mtindo ambao labda unakufurahisha ama hufurahii. Na kama unaona mtindo fulani wa maisha hufurahii basi unatakiwa kutouwazia sana, unatakiwa kuukwepa kuutundika akili mwako maana matokeo yake kuna ugonjwa wa kuhuzunika ambao wahuzunikaji hawajui chanzo chake ama kujikuta unachukia bila kujua kwanini unachukia. Tafakari na sahau yote yaliyopita, yaliyokukwaza kwani wao ni wao na wewe ni wewe ulizaliwa peke yako kisha nduzo wakafuata.
Unachotakiwa ni kuwakumbuka sana ndugu zako ambao ni wadogo zako na dada zako kama wapo.....lakini usimkumbuke sana Baba na Mama yako kwani hao siyo ndugu zako. Nadhani huwezi kuelewa falsafa hii ya kuwa wazazi wako siyo ndugu zako. Kumbuka ndugu zako siyo bidhaa kwamba unaweza kununua dukani. Siku yako ijenge na familia yako lakini usiogope kila mtu ukadhani ni adui. je kwani Torati ni dhambi? jibu unalo.
KILA LA HERI SIKU YAKO YA KUZALIWA LEO, KILA LA HERI KWA YOTE ULIYOFANIKIWA NA YALE UNAYOCHUKIZWA AU KUYAFURAHI....NATUMBUA HAYO NI SEHEMU YA JAMII ZETU YANATUHUSU SOTE.....KWA WAKUBWA NA WADOGO, MASIKINI NA MATAJIRI.

Mungu mkubwa, na uwe na nyongeza ya miaka kadhaa ya siri yako? Mhh au unalingana na mzee Nelson Mandela???????? ha ha ha ha ha ha kwaheri kwa leo

3 comments:

  1. Usengwili mlongo kunivika hapa. Ila namuyaku ninogela somba. Ahsante

    ReplyDelete

Maoni yako