01 March 2010

HERI TUMBO LILILOKUZAA

Nimeipata picha hii VUKANI imeniskitisha sanaaaa, mosi nilishtuka kutokana na masuala ya jinsia, pili labda ushamba wangu wa kutopenda kuona akina mama katika mazingira ya kuzaa LAKINI, nilimwambia Koero kuwa huo ni UKWELI MCHUNGU, ni hali ambayo inawakuta akina mama wengi, na kwakweli anastahili PONGEZI kwa kutuletea yale anayoana.
Kwakweli inashtusha kidogo hadi matumbo yanatikisika na kucheza ndombolo. Lakini huu ni UKWELI MCHUNGU ambao unauma sana lakini hali ndiyo hii, TUTANYEJE WANAJAMII?

4 comments:

 1. Bwana Mpangala. Mi sijaelewa. Kwa nini picha hii inakustusha? Akina mama kujifungulia nyumbani ni jambo geni kwa Waafrika?

  ReplyDelete
 2. Wanawake kazi tunayo jamani.

  ReplyDelete
 3. wanaume wote na ujanja wao wakiambiwa kuzaa itakuwa zamu yao walah watatimua mbio balaa.

  ReplyDelete
 4. Kilichonishtua ni kwamba huwa napenda sana kuheshimu hili suala la uzazi kwani kuonyesha hadharani kama hivi kwangu inanishtua, lakini ingawaje ni muhimu kueleza kilichopo lakini inafaa pia kuangalia ni kitu gani kinatakiwa wekwe moja kwa moja au kisiwekwe.
  Mmmh najua blogu ni waasi wa habari na ndiyo maana tunaitwa CITIZEN JOURNALISM.

  najua ni jambo la kawaida lakini tusizoee ikazidi kawaida.

  ReplyDelete

Andika maoni yako