13 April 2010

NDOA NI NINI?? SWALI KATI YA MASWALI

Nimekaa nimewaza sana, lakini sina jawabu, labda waungwana mtanijuza hasa wale walioko katika ndoa. Bado natafakri kuwa ndoa ni nini? Ni kitu gani kinatufanya tufunge ndo?

Ndoa ni upendo? Je huwezi kupata upendo kwa marafiki na ndugu? Ndoa ni kitu gani hasa sina jawabu. Kitu gani kinawafanya watu wafunge ndoa na kusema pingu za maisha?

Kwanini wanasema alichounganisha mungu binadamu asitenganishe? Je ni kweli hakuna binadamu asiyeweza kutenganisha ndoa ya mtu mwingine?
Ni kitu gani kinawafanya watu waamini ni lazima kufunga ndoa?

Nani alianza kufunga ndoa? Na kwanini alimua kufunga ndoa? Ndoa ni kuzaa watoto? Ndoa ni kuishi na mke/mume halali? Je ukiwa na li-mpenzi lako halali nayo ni ndoa?

Je kwanini watu hufunga ndoa kanisani/msikitini/wilayani n.k? Je kuishi mume/mke ni lazima wafunge ndoa? Kila mtu aishi na mkewe, je ilimaanisha afunge ndoa?

Sababu gani ilikufanya ukafunga ndoa? Je ndoa ngapi zimevunjika wakati zilikuwa zimeunganishiwa na mungu lakini binadamu aitwaye nyumba ndogo alitenganisha?

Kwanini ndoa ni ajira ya kudmu? Je ni ajira ya kudumu kweli? Kwanini watu huachana wakati waliapa mbele ya madhabahu kuwa hawatengana? Kwanini waliapa kwa vitabu vitakatifu lakini wameachana?

Nini kinachokufanya ufikirie ndoa? Na kama kuishi ndani ya ndoa ni jibu, kwanini ulalamikie ndoa yako nje ya ndoa? Je ndoa itakuletea furaha maishani?

Je ndoa na furaha ni vitu sawa? Lakini tunajua kuwa furaha na ndoa ni vitu viwili tofauti, kwanini watu waseme ndoa zao zina furaha wakati furaha haina ndoa?

Je unafunga ndoa kwa msukumo wako au kuiga tu kwakuwa watu hufunga ndoa? Ndoa zenye furaha ni zipi? Ni maswali najiuliza, sina jibu naomba jibu.

Maswali yananisonga hayana majibu naomba jawabu. Ndoa ni nini/kitu gani na kwanini iwe ndoa? Nani alipanga tufunge ndoa, ni sisi au tulipangiwa kufunga ndoa? Mababu zetu walifunga ndoa za aina gani na kwanini? Je vitabu vitakatifu vinaweza kulinda ndoa?....

Ooooopppssiiiiii maswali yamenisonga ngoja nimsikilize LUCKY DUBE katika wimbo wake wa IT'S NOT EASY, labda unalo jibu

No comments:

Post a Comment

Maoni yako