06 April 2010

ZAMANI na SASA

Unajua zamani ilikuwa burudani yangu ya kwanza kuogelea katika hali hii. Na burudani ya pili ni kandanda  na ya tatu ni Muziki.

SASA..... burudani ya kwanza kandanda, ya pili JAMES BOND paleeeeeee TOMORROW NEVER DIES. Ndiyo nini? Ziwa nyasa lina sifa kuu moja. MAWIMBI MAKALI.

Na shirika la meli linaleewa hili na mara nyingi linaweka manahodha maalum wa siku za mawimbi. Na kwa kipindi kama hii hali ya mawimbi ni kali sana hususani eneo la makonde punde ukitoka bandari ya Lupingu.
Hapo pana simulizi ambayo niliishudia baada ya kaka yangu Marehemu HENRICH MPANGALA kufanya kazi katika shirika hilo.

Ni kwamba katika eneo la makonde pana sifa kuu moja kila meli hiyo inapopita eneo hili huwa wafanyakazi au wahusika wa meli hiyo humwaga unga kwa kunyunyiza na kusema maneo fulani hata siyaelewi.

Eneo hilo mawimbi yanagonga katika ubavu wa kulia na kushoto yaani mawimbi yanapiga pande zote mbili, ni mawimbi ambayo huwashangaza watu. Wakati fulani niliona hali hiyo nilingazwa ikabidi nimuulize mzee BUKULU ni mzoefu sana kwa ziwa hili.

Akanieleza uwe msomi nenda zako, usiwe msomi nenda zako, na usiamini wanachokifanya nenda zako, lakini eneo la MAKONDE ni habari nyingine na suala la kumwaga unga yaani kunyunyizia ni suala nyeti.

Eneo lingine ni kutoka bandari ya LUNDU ambapo punde inapoondoka bandari hiyo kuelekea Mkili kuna jiwe moja linaitwa STIMA usawa wa jiwe hilo yaani kuna eneo fulani la mraba kuna mawimbi makali sana, kisha eneo la bandari ya Liuli, kwa kipindi hiki ni mawimbi maarufu kama LULENGA mkifumwa na aina ya mawimbi haya, kisha mkifanikiwa kufika Mbamba Bay bila nahodha kukataa kuendlea na safari muombeni Mungu wenu.

Lakini ZAMANI zile nilikuwa nimeizoea meli kama kitanda cha kulala tu, siku hizi eti napanda magari ajali nje nje roho mononi. ZAMANI zile nilikuwa nikipanda meli sina shaka naamini nitafika LUNDU kwetu salama. SASA nikipanda gari, nakumbana na foleni n.k

ZAMANI zile ilikuwa safi tu unaiona meli kama kikombe cha chai isiyo na sukari. Wimbi likipiga wale wasiozoea wanatapika lakini unawaangalia unacheka. SASA eti nikiangalia pale kivukoni watu wanaogopa kuzama... sijui wanaogopa nini eneo dogo kama lile pamoja na kina chake hakimtishi toto la kinyasa a.k.a mzee wa lundunyasa.

SASA badala ya kwenda katika ziara za kuhesabu abiria walioshuka kwenye meli katika bandari yetu pale LUNDU hata kama sijafanya safari eti namwangilia james bond na midude yake ya kijasusi halafu nijikuta swadakta.

Halafu nisikilize nyimbo za bongo fleva. ZAMANI zile nilikuwa nasikiliza fleva za ndugu zangu wa damu wa Malawi, na kutega sikio redio free africa kwa bongo. SASA nisikilize viredio uchwara vilivyopo Dar es salaam. ZAMANI nilikuwa nasikiliza sana CHANNEL AFRIKA, RADIO TWO, KISS FM,RTD,RADIO MARIA SONGEA,SAUTI YA IRANI,CHINA,AMERIKA,BBC,DW,SAUTI YA ZAMBIA,RWANDA n.k

SASA nakesha katika Tarakilishi kama hivi naandika mambo ya ZAMANI na SASA. ZAMANI sikujua kama kuna kuvaa kucha za bandia na nywele/mawigi, ZAMANI nilinunua muwa kwa shilingi 7/=, SASA nanunua kwa shilingi 50/=.

ZAMANI nilikuwa nakula sana kisamvu, mabumunda,mpuchulela,kunde, mbasa, embe ng'ong'o kwetu tunaita HIRONGO.

 ZAMANI zile nilikuwa na marafiki wengi wamisionari, iwe mapadre au mabruda ama ndugu zao tu. ZAMANI Kornelia alipotuona pale LUNDU watoto tunatembea pekupeku aliiga akazoea toto lile la kizingu, alipoona tunacheza ligambusa aliingia dimbani huku kaufunga kanga kiunoni.

Wamisonari wale walinipenda lakini nilipogoma kuwa minislanti kanisani wakanikasirikia na wengine wakanitenga. Na nilipoondolewa seminari waliudhika zaidi..lakini mimi niliuliza tu lile swali wala sikutaka kujua zaidi.

ZAMANI nilikuwa napenda sana kuwa mwanamuziki, lakini sasa nataka kuwa gwiji wa teknolojia cha ajabu sijui ubunifu....ZAMANI ilikuwa raha sana mambo ya ndombolo, Kwaito, aaah nimemkumbuka rafiki yangu na  ule wimbo wake wa NIBWEZELENI NDALAMA ZANGA=mnirudishie hela zangu. Aliimba yule rafiki yangu akiwaimbia makonda ma madereva wa daladala. ZAMANI baba tulimwita NDULI kutokana na kuiendesha familia kijeshi ndiyo maana leo ninakiburi labda.

ZAMANI ilikuwa starehe kuoposha samaki, kuwinda,kulima,kutega nyavu,kupalaza mitumbwi na kuwinda ndege,kuogelea mtoni n.k.... NAKUMBUKA ZAMANI


HIVI ZAMANI na SASA KITU GANI KINATOFAUTISHA??

3 comments:

 1. Umenikumbusha mbali. ni historia nzuri, Muda si mrefu ya sasa pia yatakuwa ya zamani. ili mradi historia iendelee kuandikika.

  ReplyDelete
 2. Mzee Unanitamanisha sana zamani! ila ndio hivyo tena imeshakwenda! lakini pia acha mchezo wako wa kututamanisha tamanisha vitu ambavyo Hapa Bongo havipatikani! Mbasa!, tena umenikumbusha Likungu, mbufu na Mbelele, Ligambusa angalau huwa naliambulia ambaulia nikihudhuria Harusi fuani fulani hapa jijini, Mganda mpaka kuwa na sherehe fulani ambayo kunakuwepo na ngama za Asili.

  Lakini pia sasa ni wakati wa hawa wa sasa kuyafaidi yazamani waliyonayo wao sasa, ambayo nao watayakumbuka, lakini inasikitisha hawawezi kuyafaidi kama tulivyofaidi sisi, tumewamalizia mengi, na tunawaharibia pia ambayo wangepaswa wakati wao wa kukumbuka zamani unapofika wayakumbuke! miti tumekata, samaki hawawezi kuwa bwelele kama wakati wao huu ulipokuwa wetu, matunda angalau masuku (mapotopoto) yanaonekana, ndege hali kadhalika, wanatoweka miti inapopungua, mabwawa ya kuopeshea samaki yanatoweka, na .. ah basi bwana wacha nikwamie hapo! .. nitazusha mengine bure!

  ReplyDelete
 3. Nyumbani ni nyumbani na zamani ni safi sana. Markus kwanini kutamanishana hivyo hata wewe mwenyewe umetamani vidongo, magege aahhhhh we acha tu !!

  ReplyDelete

Maoni yako