13 May 2010

BLOGU YA IKULU YA TANZANIA

Janamni wanablogu wenzangu, USIKU huu nimetembelea blogu ya IKULU ya TANZANIA ambayo inaendeshwa na idara ya mawasiliano ya IKULU. Nimejaribu kuisoma na kuangalia kitu gani kipo, lakini nasema NAONA KICHEFUCHEFU NATAKA KUTAPIKA, kama siyo KUHARISHA bin UHARO wa nini sijui.

Hapa ni FULL MCHARUKO. kwanza blogu lenyewe lugha ya kikoloni, sijui hawa watu wanajua wanachokifanya au la. Halafu wanatumia huduma za GOOGLE kwa masuala ya nchi.

Labda ndiyo maana Rais Bingu wa Mutharika ameamua kufunga blogu yake. Maana nilimwuliza rafiki yangu mmoja kwanini blogu hiyo haipatikani au ipo katika matengenezo lakini niliambiwa imefungwa. SINA HAKIKA.

sasa nimekasirishwa na mwenendo wenyewe hakuna JIPYA hakuna taarifa. NINA HASIRA ZANGU kila kitu kinafanywa kwa mzaha tu. Ngoja NITAWAPONGEZA KWA KUWA WANABLOGU.

Haya hii hapa jamani oneni wanaogopa hata WASIO NA MAJINA/ANONYMOUS, yaani maoni hadi yachapishwe au kupitiwa na wahusika ndipo yawekwe. KICHEFUCHEFU tu. Hiki ni kitu cha wazi kuhusu nchi siyo mali ya mtu vinginevyo waifunge tu HAKUNA JIPYA

No comments:

Post a Comment

Andika maoni yako