15 May 2010

HAPPY BIRTHDAY MARKUS MPANGALA@27

Pichani nikiwa Lundo Sekondari nje ya bweni la wavulana
Nashukuru BABA na MAMA kwa kunileta duniani. Nashukuru binadamu wote duniani kwani mnanifanya kama nilivyo. Leo ni siku yangu namkumbuka mama yangu na baba yangu. ASANTE mama kwa kunifundisha neno hili ingawaje ulisema ni dogo lenye maana kubwa. ASANTE miezi tisa uliyokubali kunitunza.

Pichani mambo ya TAI nikiwa high skul Meta sekondari. BABA na MAMA kunilipia elimu, kidato cha juu kujiongezea. ASANTE wazazi wangu.

MV Songea hapo chini, meli niliyoiamini daima kutoka Mbamba Bay hadi kijijini Lundu. Kutoka Lundu hadi Itungi Kyela. Safarini kidato.

Usafiri wangu nikiwa Lundo sekondari, nilivumilia mengi kwa ujasiri wa MAMA na BABA. Niliipenda shule, nilipenda kazi ya kuvua, lakini BABA akasema shule kwanza. Nashukuru sijaacha kuvua samaki. Ingawa zile ndoto za awali kwenda Seminari, Ule upadre kuota mbaya. Nimesahau sana, nimekubalia ingawa napenda kwa macho, ila nafsi imegoma, kwa yale yaliyojiri. Ila nina furaha sana kwayo.

MLIMANI masomoni, elimu kuijaza kichwani, kutumikia jamii

Nilipomaliza Meta, safari MLIMANI, hapa MAWAZONI, mgomo ukajili 2007 nikarejea nyumbani. Nilipandisha Sayansi ya Siasa na Utawala pamoja na Historia. ulioje najisikia amani moyoni kile ninchopenda badala ya utawa ule uleeeeee

Wakati jasiri haachi asili
ASANTENI

15 comments:

 1. Hongera sana kwa siku yako hii tukufu umekuwa kijana mkubwa sana miaka 27. Nakutakia kila la heri na pia mafanikio mema kwa kila ufanyalo.
  HONGERA SANA. UPENDO DAIMA!!!!

  ReplyDelete
 2. Mtani nakupa pongezi sana kwa siku hii muhimu kwako.

  Ninachofurahi leo nimepata nafasi ya kuwa pamoja nawe.

  Ninakuombea maisha marefu sana yenye furaha, amani na mafanikio.

  Happy Birthday mtani!

  ReplyDelete
 3. Yasinta, hakuna cha kututenganisha, ni ngumu ewe binti gervas.

  Mkuu!! Kitururu leo imekufaraja kubwa kulonga nawe a.k.a uhuru wa kuongea. Bonge la Taralila hili

  Mtani Fadhy! bonge la MICHANO mawazo tukayaweka sawa, wadau wangu TUKO PA+ yaani PAMOJA. Chip nimekukosa bro!

  Kaka Chacha, raha sana kuongea nawe leo ni raha sana na hii ni nguvu ya blog, nitaandika michano hapo. ASANTENI SANA

  ReplyDelete
 4. @ KALUSE sijakusahau kaka, wewe ndiye kiungo mkuu leo umewakutanaisha wanablogu katika anga zingine, SITASAHAU SUPRISE YAKO LEO imeniwazisha na kuingia MAWAZONI kwamba mimi ni nani? TUKOP PA+ yaani pamoja kaka!

  ReplyDelete
 5. Safi sana, sasa vipi suala la kutafuta JIKO? Miaka inaenda shauri yako, huu ndo wakati muafaka.

  Happy birthdate.

  ReplyDelete
 6. Happy Birthday nakutakia maisha marefu mema yenye furaha na afya tele kwako na kwa familia kwa ujumla

  ReplyDelete
 7. Da Mija kutafuta jiko ni shughuli pevu, lakini kwakuwa napenda mambo ya zamani hiyo kazi nmwachia dada yangu Yasinta namwamini atanibulia kimwana mnono mpenda mazoezi kama yeye.
  Nitaondokana na huu UKAPERA Lol

  Mumyhery, SHUKRANI SANA

  ReplyDelete
 8. HA HA HA HA! eti unaniachia mimi Yasinta, mie ntajuaje kama huyo nimpendekezaye ndiye wewe unampenda na utaishi naye milele hii ni kazi yako na Da Mija amesema kweli kabisa huu ni muda mzuri kutafuta JIKO au mama msapu. Upendo daima.

  ReplyDelete
 9. Happy Belated Birthday Markus, sorry nimechelewa I was away but I hope you had a great day, blessings! xx

  ReplyDelete
 10. napenda Mamsapu tatizo nimeomba Mchungaji Koero anitafutie kwanza wa kutia EMCHEKU upareni ila tatizo ana kiburi anataka sijui iweje.

  Ngoja najaribu kufikiria sasa nisake kimwana ila naamini nakuachia wewe Yasinta unisakie kigoli huyo. Lol

  ReplyDelete
 11. HONGERA KWA SIKU YA KUZALIWA MKUU. TUPO PAMOJA

  ReplyDelete

Andika maoni yako