27 June 2010

OFISI IMEJAA, SIPUMUI

                                     ofisini a.k.a kijiweni
Unajua kuna wakati binadamu unahitaji utulivu kupindukia, lakini wakati ukifanya hivyo kumbuka marafiki ndiyo wanaokupa muda mzuri wa kupumzika na kujadili haya na yale. Nashukuru mtani wangu Fadhy Mtanga anakuja kunijulia hali, maana anajua mawazo yangu yako WOZA 2010 huko afrika kusini nashuhudia JABULANI linavyowahenyesha walinda milano. Anajua hapa ninalo VUVUZELA na MAKARAPA lile kofia lenye mikogo kibao. Pamoja na hayo lakini kaofisi kamejaa makabrasha hata sipumui. Yaani kila nikigeuka naona karatasi yaani sina hata sehemu ya kutolea USHUZI upenye kwenda nje, maana hewa yoooote itaishia hapahapa. Mmmh kweli kuna binadamu asiyepasua USHUZI? Jamani hili kombe linatupatia fursa wengine huwezi kuamini, Haya nipo sana tu leo nimewakumbuka marafiki zangu wooooooteee wanablogu na wasomaji. karibuni nyasa


1 comment:

 1. Anonymous29 June, 2010

  mtani shemeji wacha kabisa...hii Woza imenifanya kuwa mtu wa kufanya mambo kwa kufuata ratiba vibaya mno maana najitahidi kutunza muda ili nisikose kutazama wanaume wanavyokimbizana na watoto wa kiume.

  pole sana kwa kushindwa kupumua kwa hayo makabrasha hapo kwa ofisi.

  salamu zifike mtani.

  fadhy lumuliko mtanga.

  ReplyDelete

Maoni yako