26 August 2010

Mr. II a.k.a SUGU

Nimekwambia zamani ningekuwa mwanamuziki wa bongofleva. uwezo wa kuandika mashairi bado upo. Ninaweza hata kuandika kitabu juu ya historia ya Bongofleva. Lakini siku hizi nachoka naona Bongofleva imevamiwa, hadi nahisi kinyaa. Unakumbuka zama za akina D ROB, SALEH JABIR, TERRY MSIAGI a.k.a FANANI au Mr TEACHER? aaah we acha tuuuu
Siku hizo vitoto vya mafisadi navyo vinaimba Bongofleva, vinashinda Mbezi Beach na kulala kwa raha vinajifanya vinajua GHETO. Vimechakachua Bongofleva kabisa, halafu vinajiita GANGSTARS. Vimekulia MASAKI vinajiita GANGSTARS. Vikivaa suruwali hadi matako kunaonekana, halafu vinajifanya wagumu kama ICE CUBE au Dr Dre. Vinakulia Oysterbay vinajifanya vinajua RAP. Vinakulia UHINDINI mbeya vinajifanya vinajua RAP. Vinaimba nyimbo chafu chafu zenye matusi halafu vinasema vigumu vya hip hop. Na siku hizi kuna vinyimbo vya DINI vichafu na vya kifisadi eti vinamwimbia MUNGU, uchafu mtupu kinyaa kuona.

Lakini SUGU anagombea ubunge, halafu angalia rekodi yake ndipo utasema huyu ndiye mgumu wa Gheto anaujua msoto, siyo watoto waliokulia kupanda mikoko mipya mipya inajiita wagumu wa gheto. NAWAKILISHA HIP HOP mzee wa lundunyasa, nawakilisha KWAITO daima. Nawakilisha bolingo. Nimemis mistari ya SOLO THANG ulamaa aliyekomaa.

PICHANI; Joseph Mbilinyi a.k.a SUGU a.k.a 2PROUD akiwa na Mkoloni na G SOLO. wakiwa na John Mnyika ndani CHADEMA na ndugu zangu wa mbeya wanasema KYADEMA

3 comments:

  1. yangu kapata, ya rafiki zangu kama kumi keshapata

    ReplyDelete
  2. bahati mbaya sipo huko angepata yangu pia. Lakini namtakia kila la kheri.

    ReplyDelete
  3. Nyia ambao hampo tutawapigia kura zenu, kuna wakati tunapigiana, hiyo siri yenu, tutawapigaaa...

    ReplyDelete

Maoni yako