14 September 2010

MARKUS UTAOA LINI?, SIYO LEO WALA KESHO.....labda KOERO MKUNDI

Najua wadau nimeadimika hapa. Lakini ukweli ni kwamba MONEY NEVER SLEEP, jamani hakika nawaambieni. Si mnakumbuka tarehe 24 mwezi huu wale jamaa wa kule WALL STREET wanatuletea simulizi zao? Heeee!!! hujui kuwa filamu ya WALL STREET; MONEY NEVER SLEEP inakujia? Hata hivyo haina maana sana lakini umaana ni MONEY NEVER SLEEP au siyo.

Nimeibuka na kaujumbe haka leo baada ya kuulizwa swali na mzee mmoja a.k.a bosi wangu wa MONEY NEVER SLEEP, mahali ambapo najaribu kuandika upuuzi wangu wa vi-makala fulani.

Swali lake juu yangu kwamba nitaoa lini, nikamjibu SIYO LEO WALA KESHO. Na ninazo sababu kadhaa kukushirikisha mdau wangu. Kumbuka wakati wa siku yangu ya KUZALIWA nilidokeza JIKO nililoliomba tuwe tunapika pamoja na kuoga pamoja. Jibu ni kweli hilo JIKO lipo na 'in gods name',  itakuwa leo na kesho. Hapo sina jingine zaidi ya kuamini hivyo kwani nathubutu kuamini zaidi, nitakuwa na JIKO hilo.

SASA wakati najaribu kujibu swali hilo, nilijikuta nikitoa vigezo vipya ambavyo nimegundua bila hivyo kuna tabu huko mbele. Lakini vigezo vya JIKO langu lile vimebaki na atabaki yeye hadi akili itakapofyatuka.......

NIMEGUNDUA NDOA ninayoitaka ni ile ya mwanamke Jeuri,shujaa,mkorofi,mtukutu,mbabe,mbishi, anayejua haki za wanawake wenzake na zake ngangari, yaani mwanamke mwenye picha na taswira ya kibabe babe tu. Mwanamke mwenye jambo jipya kila mara.

Napenda sana mwanamke yule anayeishi kiubishi na kuthubutu, ambaye kwake kuhoji hakuna shida. Nataka mwanamke ambaye akiona wala hatishiki walau kuogopa KIDUME CHAKE nimeingia ndani ya nyumba. Yaani akiona awe vilevile amekunja sura kama yuko lindoni.

NIMEGUNDUA NDOA YANGU na NAOTA KUFUNGA NDOA NA KOERO MKUNDI. Anazosifa za kijabali yaani mwanamke ngangari,shujaa,jeuri,mbishi na zaidi ni mtetezi wa haki za wanawake. NIMEGUNDUA Koero Mkundi ni bonge la mwanamke hodari maana anaweza kunishikia konde a.k.a ngumi jiwe. Napenda mwanamke wa aina hii ambaye anajisimamia hataki kusimamiwa pekee.

SITANII naota kufunga pingu za MAISHA na KOERO MKUNDI na kuanzia leo namtangazia sitamwita dada hata kidogo bali nitamwambia 'naomba TUOANE'. Sijali atajibu nini kwani najua anavyopenda kufikiria atasema NIPE MUDA.

Nina uhakika atakubali jamaniiiiiii eeeeeeh simpi mtu kitochi wala nini NAOTA KUFUNGA NDOA NA KOERO BINTI MKUNDI. Kwanza nimeangalia mengi tu, sasa  nataka rasmi hata kama nilimtaka kwa kificho, si unakumbuka alisema wamtakao wengi ma-annon???

Sasa NAJA kwa mzee Japhet bin Mkundi, samahani mzee nikikuosea adabu ila MWANAO NI BONGE LA DHAHABU ambayo ni adimu kupata ila najua ana kawaida ya kukasirika tu. Na akisoma ajue hizi siyo NDOTO bali UKWELI na yupi atakuwa bi mkubwa, najua mimi. UKINUNA POAAA TU lakini rasmi nifunga ndoa na KOERO BINTI MKUNDI. Hii siyo nia bali dhamira ya dhati MAANANI.

5 comments:

 1. watu weweeeeeeee...

  ila shemeji kwa kuwa nimekutonya nanunua ndoano ya kumnasa Koero ndo umeamua kuniovateki? anyway kwa kuwa watangaza nia tupo wengi....inabidi atangaze rasmi tarehe ya kuanza kampeni kisha tarehe ya uchaguzi

  ReplyDelete
 2. aga gangi mwenga! na sasa naona mashemeji wanaanza kugombana kumgombania mdogo wangu wa hiari. Raha kweli ha ha ha ha ha kaaaazi kwelikweli

  ReplyDelete
 3. wakikubwaga njoo Mara, kuna mademu wababe pia....lol! Ila ujiandaye kumbwenga magumi kwa kuwa usipombwenga mwaka mzima ataenda kwao akidai hmpendi....lol!

  na mwisho jiandaye kupata ngeu...lol!

  ReplyDelete
 4. Mama Mchungaji na ujeuri/utukutu wapi na wapi???

  ReplyDelete

Maoni yako