21 December 2010

KAMA HUKUJUA KUHUSU MIYE MARKUS MPANGALA

Unajua miye siwezi kujielezea ati kwa kuogopa taarifa zangu kuzagaa mitandaoni? Ha ha ha labda nina wazimu kuwaogopa wasojua kuwa siwajui, lakini najua wananijua. Labda hukujua siku zote nakimbia kujikweza hata kama ni muhimu kujiumbia ushujaa bandia.
Ndiyo maana nakataa sana kuufikiria ukweli, bali nataka kuishi katika misingi ya ukweli. Na mara nyingi napenda ukweli uwepo katika lugha yoyote iwe kali ama imepozwa na vimiminika vya mdomo kwa kuongeza lugha tamu anuai kama limtu linalobembeleza mkewe.

Labda nikielezeya zaidi na uzeya wa fikra za maisha huria ati niogope matapeli wanasulubu kwa kutumia lukuma kama tu singeli peni. Nakumbuka Padri Jordan Nyenyembe alinijuza CHAGUA LAKO UTUNZE. Na ikawa hatua mwanana kuandikiya kitabu. Nami nachagu langu nalitunza.....
Na katika siku za karibuni hata tarakimu yangu ya simu imevamiwa,inasikilizwa,inafuatiliwa na kdhalika. Nimehama tarakimu za simu, na hata baruapepe yangu niitumiayo daima siitumii sana. Nimeifungua nyingine walau niwe najaribu kujifunza UNAFIKI wa maisha ya siku hizi.

KAMA hukujua, Mie Markus Mpangala sina mahusiano na kabila la WANGONI kinasaba zaidi ya sisi wanadamu KUPENDANA NA KUJALIANA.

HUKUJUA......
Babu yangu aliyemzaa baba hakuzaliwa Tanzania, alitokea Malawi wenyewe tunaiita CHIDYA. Babu huyu ambaye ni kabila la Wanyanja wa pale Lilongwe(kama umefika mji ule niupendao anuai na penzi la tashititi), ndipo asili ya UKOO wa MPANGALALA. Usishangae jina MPANGALALA, hiyo ndiyo asili yao ambapo walipoingia Tanzania walijiita MPANGALA yaani wakiondoa LA moja.
Walipoamia Tanzania wakatua mji wa KIHAGARA ua NJAMBE. Jina la mji huu linatokana na ukoo wa MPANGALA ambao kwa wanawake huitwa NJAMBE. Basi wakasambaa mwambao wa Nyasa hadi Mbeya.
Babu yangu huyu aitwaye HONORIUS alioa binti wa Kitanzania kabla ya uhuru, yapata miaka ya kale. Nao wakamzaa baba yangu pale kijiji Lundu, mwambao wa nyasa, na sasa kuna wilaya mpya inatwa Nyasa.

HUKUJUA......
Mama yangu alitokana na mama yake aliyetoka MSUMBIJI.Yaani Babu aliyemzaa mama alioa binti kutoka Msumbiji na kuingia Tanzania wakati akitokea Johannesburg, kwa mzee Madiba. Mkewe huyo akawa mali ya nchi ya Tanzania.
SASA....... baba yangu na mama yangu wakakutana, wakatongozana,wachumbiana, wakaoana na kisha wakazaa watoto kadhaa NIKIWEMO MIYE MARKUS. Na kwa hamu kaka yangu mpenda historia anaishi Lilongwe kwa raha zake.
Wazazi wangu hawa wakaniandikisha shule kwa jina la babu, Honorius, lakini nikumbie msomaji wa blogu hii, miye nipo katika KUHAMA kutoka HONORIUS iliyozoeleka na kuulizwa kama ni kweli raia wa nchi hii, nakwenda zangu katika MPANGALA....

Naam, utaona miye MNYASA, wazazi WANYASA wala hawana nasaba na WANGONI zaidi ya ubinadamu na makutano ya uwepo wao. Utaona nimetokana na kabila la Wanyanja ambao huku TZ tunaita WANYASA.
Na katika kuishi nimeisha pale mji ulionikuza wa MBINGA na kabila la Wamatengo(unajua asili ya wamtengo? nitakueleza siku moja).

FALSAFA...
Walimu walionijuza darasani tangu enzi, nawapenda sana. Sijali kama baadhi yao walitoka Bavaria, wamisionari,wachaga,wahaya,wakinga,wamatengo,wangoni,wasambaa,wapare,wangazija,wamanyema na kadhalika. Utaona mimi ni Mtanzania mwenye asili ya Tanzania. Sijawahi kufundishwa ubaguzi au utengano. Nilifundishwa kuwapenda wato wote, ndiyo maana pamoja na 20+7= kokotoa miaka yangu NAONYWA sana na baba yangu ninayempenda kuliko binadamu yeyote chini ya JUA, aniambiapo "MARKUS USIJIONE KUWA WEWE NI BORA KULIKO WATANZANIA WENGINE".

Baba yangu bwana we acha tu, kama lugha alinijuza alizojijuza ni nyingi. alinifundisha lugha za makabila mbalimbali anuai. Akaniambia "DAIMA UISHI KAMA WEWE NA UWE WEWE". Nakumbuka nilipoahidi sitotaka kigawo chochote cha mali ya familia. Nikasema nasaka yangu. Ingekuwa kuridhika kuishi kwakuwa mali zipo za wazazi basi ninaweza kuirejesha hali ile kwa wazazi. Lakini sitohitaji hata kikombe cha chai. Nitanunua kikombe cha chai mwenyewe.

VIPI BLOGU ?
Wapo wanaoonyesha upendo wao kwenye mablog, ni safi kwa lugha za mseto. Wapo marafiki wengi wanaoishi kwasababu ya blogu na maisha mengine.
ndiyo blogu inanipa NOTI, na ikanipa kazi. Labda ndiyo maana nina kiu ya kuwafikia wale wote walioko.

KWANINI NAANDIKA
Ni kwasababu napenda watu wanijue nilivyo,wapate wasaa wa kujiuziliza vificho vyao havitokani na kutopenda kujiandika bali kuishi kwa KUUFIKIRIA UKWELI. ama zile habari kuwa siyo BUSARA KUANDIKA KILA KITU mitandao. Miye naandika, yeyote mwenye kukwiba na akwibe. NAKUPENDENI SANA RAFIKI ZANGU vyovyote iwavyo mimi ndiye, nitabaki kuwa miye

NILIKUWA NA NAFIKIRIA NINI? .......labda ninakichaa, mwendawazimu, juha,mshamba,wakale, kujionesha. ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha TO DARE IS TO DO.

5 comments:

 1. shemeji aka mtani kwanza za masiku mengi? unajua si vema mwaka ukimalizika hatujaonana....tuachane na hilo....

  shemeji unajua una kipaji sana cha kushusha maandishi....walahi vile....

  ReplyDelete
 2. Lelu nga lelu niwone mlongo ukiti cha bwina kujova veve va yani!!

  ReplyDelete
 3. Tumekupata mkuu, umejielezea vyema, na nshukuru wewe ni wacheche wanaopenda kutoa bila uchoyo. Hongera sana na Mungu atakuzzidishia

  ReplyDelete
 4. kaka ukiingia kwenye siasa umekwisha, maana utazushiwa kuwa sio raia...LOL

  Habari za siku kaka....maan naona umekaa kimya mno.
  Basi ukipata muda na wasaa, karibu kijiweni kwangu tupata khahawa..

  ReplyDelete
 5. Nimependa ulivyojidadavua bila kujichakachua hata kidogo,sikujui lakin nafikiri ndivyo ulivyo,......napenda kuwa na kufanya kila kitu kama mtu ulivyo i.e bila ku-fake(walk the talk).....na hapo ndipo penye hekima/akili

  ReplyDelete

Maoni yako