23 December 2010

SWALI USILIVALIE MIWANI

Moja ya mawazo yangu ni kujiuliza maswali. Mara nyingi najiona mwehu kwa kasumba hii. Labda wajua kuwa miye ni mzeya wa kufikiria uzeya kwakuwa tu ninayo maswali.
WALA SWALI LANGU USILIVALIE MIWANI.
Labda ni moja tu ya kufikiria namna ya kuwarejeshea wanyasa ladha ya blogu yao.

USIDHANI KUNA KUISHI MARA MBILI DUNIANI.
Ndiyo maana wenye kasumba za kupendelea kujiona wazuri kwakuwa wameumbwa vizuri basi wanaweza kuwavutiwa hata akina Markus.

UZURI NI SILAHA BWANA USIPIME.

Labda mie HUKUJUA nimezaliwa kijijini,likizo zangu zilikuwa kijijini, tangu enzi za vidudu,seko,High,Koleji na Ya Juu. Likizo kijijini.

NINA UHAKIKA MWENYE DHAMBI NI MUNGU ALIYEUMBA DHAMBI, UNABISHA? nijibu swali.
Kila siku ugomvi wangu ni mama yangu, ati wewe mtoto unataka kumwona muumba mbingu na nchi yote ya watani,wapare,wachaga,wakurya na wandengereko.

UKICHEKEWA USIDHANI UNAPENDWA.
Ndiyo maana mimi mkulima,mwanakijiji. Nakiri maisha yangu yametawaliwa na falsafa za kijijini kwetu Lundu. Tena nilikuwa najiona mjanja sana kule kijijini lakini huku mjini kuna wenye vinyonyo na vifua vya kubadikiza na vyuma halafu wanaitwa mabaunsa ati wana nguvu.

HALAFU NIKAFUNDISHWA KUCHOMOKEA.

Udhaifu niliona ni kushindwa kuchomekea shati ndani ya suluwali. Udhaifu wangu ni woga wa kukutana na watu mara ya kwanza, udhaifu wangu ni kupoteza hali ya kujiamini, udhaifu wangu ni kushindwa kuwa mbunifu,udhaifu wangu ni kushindwa kujiondoa katika lindi la umasikini ambao kila siku nakuwa kajamba nani anayegomea  ughaibuni.

SWALI MUHIMU KWAKO MSOMAJI, FIKIRIA TU.

 KWANI UNAFUGA VIROBOTO HALAFU UNAOGOPA KUTOA FUNZA?

No comments:

Post a Comment

Maoni yako