February 23, 2010
HUJAMSOMA 'SUN TZU' KAZI KWAKO
Nafuta jasho, lakini bado linatililika tu, nahaha huko na huko kwenye maduka rasmi na yale ya wamachinga kuona kama naweza kupata. Lakini sijakata tamaa naendelea kusaka, ili kujifaliji nikaamua kununu kijitabu kidogo cha 100 THINGS TO DO BEFORE YOU DIE, napitisha mistari yake kidogo lakini kiu yangu ni kusaka kitabu cha SUN TZU cha THE ART OF WAR, ghafla najikuta nipo mitaaya Samora, naingia dukani natumbua mimacho kama nimebanwa na mlango, ..... na sasa najisikia fahari kwa raha najisomea aya kali na nadharia maridadi za huyu mtu. We acha tu THE ART OF WAR ni zaidi ya burudani waungwana.
Madhumuni
falsafa,
kumbukumbu,
maisha,
mapumziko
February 22, 2010
BARUA YA PAPII KOCHA KWA RAISI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
SHUKRANI KWA DADA SUBI SABATO, KURUHUSU KUSAMBAZA BARUA HII
Barua ya Papii Kocha kwenda kwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano Tanzania 02/21/2010
Barua hii ametumiwa Judith Wambura (Jide) LadyJayDee na ameruhusu itumike katika vyombo vya habari na mawasiliano ila shukrani na taratibu za kunakili zizingatiwe. Tafadhali zingatia hilo.
MF/NA: 836'04 Johnson Nguza (Papii Kocha)
Gereza Kuu Ukonga
S.L.P 9091
Dar es Salaam
Mh. Rais Jamuhuri ya Muungano Tanzania
YAH: MAOMBI YA KUPEWA MSAADA (MSAMAHA) WA KUFUTIWA ADHABU YA KIFUNGO NILIYOPEWA NA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU.
Husika na somo hilo hapo juu. Mimi ni mfungwa katika gereza kuu Ukonga.
Kwa heshma na taadhima na kwa kutambua utu na huruma yako ya ki MUNGU ulionayo dhidi ya binadamu wenzako pamoja na mamlaka uliokabidhiwa na jamuhuri ya muungano wa Tanzania.
Naanguka na kushika miguu yako mitukufu muheshimiwa rais.
Na kuomba msaada (msamaha) kwako muheshimiwa rais
Kwa njia hii ya maandishi kusudi niweze kuondolewa adhabu ya kifungo cha maisha gerezani, niliyohukumiwa na mahakama tajwa hapo juu.
Mh.Rais mimi nimefungwa nikiwa bado kijana mwenye umri mdogo. Mpaka sasa natambua wazi hatima pamoja na dhamana ya maisha yangu ipo katika mikono yako mitukufu Mh. Rais.
Naomba huruma yako muheshimiwa Rais maana mimi ni mtoto wako ninaehitaji huruma yako wewe mzazi.
Natumaini kauli yako ya mwisho ndio itakayoleta pumzi ya uhai nafsini mwangu
Nakutakia kazi njema, afya njema na maisha marefu.
Mungu akubariki
Wako mtiifu
NO:836'04JOHNSON NGUZA (PAPII KOCHA)
Madhumuni
habari,
Hisia za moyo,
kumbukumbu,
maisha
Subscribe to:
Posts (Atom)
