April 09, 2010

HERI WAZAZI WANAOKULEA CAMILLA T.K!

CAMILLA T.K
Umekaa umetuliya,
kazi zako jifanyiya,
mafunzo shikiliya,
Camilla nakushangliya,
mwana kujifuniya
baba na mama fikiriya,
malezi kushikiliya,
mema kujivuniya,
makuzi yasikurabiya.

Heri baba alinaekulea na heri mama anayekulea

Camilla, bado kazi moja ya kulima maana sijui (?) kama umeshaanza. Ila usilalamike sana, ungekuwa kipindi hiki Bongo kuna kiubaridi ambacho kingekufanya uache kushinda ndani ya maji kama samaki...Lol..
Heri wazazi wanaokulea, heri kwao kukupatia malezi bora,kazi kujifunzia na mengineyo mema. Love you Baby Gal

April 05, 2010

NADHARIA YA PROFESA ZAKARIA MOCHIWA

Wakati mwingine najilazimisha tu kufikiri hata kama silazimiki kufikiria hicho ninachokifikiria.

Natambua umuhimu wa kufikiri kwa wanadamu. Ni busara kujiuliza matatizo mangapi yanapaswa kutatuliwa na mwenyezi Mungu? Ni muhimu kujiuliza hivi sisi ni nani?

Na kwanini basi tupo hivi tulivyo na siyo vile walivyo? Kuna nini, na kwanini wengine wana uwezo wa kubaini kile kinachoweza kubainishwa na wengine pia?

Dunia imejaa mapambano, watu wanafurahia kuishi kwayo na wengine wanalalamika dunia mbaya. Tatizo ni sisi wenye ubaya na maudhi lakini dunia haina ubaya, na tabia mbaya siyo za dunia bali ni mali ya bindamu.
Kumbe ni UTAMBUZI.

*********Ngoja PROFESA ZAKARIA MOCHIWA ATUJUZE ZAIDI*****

NADHARIA YA PROFESA ZAKARIA MOCHIWA


Binadamu yeyote ni matokeo ya ajali tatu.

1).AJALI YA KWANZA NI KUZALIWA

Kila mtu hakupanga kuzaliwa hivyo hakuna aliyepanga kwamba sasa anataka kuzaliwa. Kila mtu alijikuta tu kazaliwa,akalelewa,akakua na kadhalika.

2).AJALI YA PILI NI JINSIA

Profesa Mochiwa alisema ni kwamba hakuna aliyechagua awe na jinsia Fulani,sura Fulani,maumbile Fulani, au rangi Fulani ya ngozi. Ni vitu ambayvo kila mtu anazaliwa anajikuta anavyo.

Katika dunia ya leo tunafahamu wapo wanaobadili jinsia,maumbile,rangi ya ngozi, lakini linathibitisha kwamba hawajivunii hali walizozaliwa nayo.

3).AJALI YA TATU HAKUNA ALIYECHAGUA KUZALIWA MAZINGIRA FULANI

Hii iwe ni nchi nzuri yenye amani,katika nchi au familia yenye utajiri mwingi n.k Kila mtu hujikuta kazaliwa kakulia katika nchi na katika familia Fulani bila utashi wake binafsi. Bila kuchagua kwa vile binadamu huzaliwa katika mazingira ya ajali hizo tatu basi utakuwa ni ujinga kwa mtu kujiona wa maana kwasababu ya faida zilizotokana na ajali hizo huku akiwadharau au kuwacheka wale ambao ajali hizo ziliwaweka katika hasara.

Profesa Mochiwa anasema hivyo sababu ni ujuha kuwatambia wengine kwa kitu ambacho hukukitengeneza wewe, huku ukiwakashifu na kuwadharau wengine kwa kitu ambacho wao pia hawakukitengeza.

Pia ni ujuha kujutia kuzaliwa katika mazingira ambayo ajali zile zimekuweka katika hasara.

Anasema binadamu ni kiumbe anaeongoza duniani kwa uwezo wa kiakili wa kubadilisha hasara za ajali za kuzaliwa kwake zikawa faida pia.

Mfano kutumia uwezo wa kiakili uliozaliwa nao kubadilisha hasara iliyotokana na ajali ya wewe kuzaliwa katika nchi masikini ikawa faida kwako.
********************

NATUMAINI UMEELEWA JAMBO

NATUMIA HUDUMA HII

Baada ya kipindi fulani kutumia huduma za Zantel ambazo kidogo zilikuwa zikikasirisha kwa mambo kadhaa ikiwemo usumbufu fulani. Nilivumilia lakini yakanishinda.

Nakubali hudma ya Zantel katika mtandao wa Tarakilishi ni nzuri na rahisi unaweza kusafiri nayo kwenda popote huku tukuwa na Tarakilishi ndogo.

Lakini sasa natumia huduma hiyo hapo juu, huduma hii unaweza kupata mtandao wa Tarakilishi kwa njia ya simu ya mezani,simu na Flash diski, haya ni mapinduzi katika teknolojia.

Ni huduma poa, ikinusumbua tu nawafuata katika ofisi zao na kufaytuka kwa huduma mbovu sitaki utani tena. Lakini niseme tu ukweli ni huduma ambayo imeniridhisha sana, nimeikubali naiona poaaaaa kabisa. Je wewe unangoja nini? Usipitweeeeeeeeeeeeee

April 04, 2010

YALE MAISHA YETU

Nikitazama nyumba kama hizi zinanikumbusha wale wanaoishi katika mazingira haya. Na kwakuwa nayakumbuka mazingira yaliyonizunguka kijijini kwetu nyasa nathubutu kusema najivunia kuishi katika mazingira ya aina hii ambayo yananipa USONGO zaidi wa kuishi kadiri niwezavyo.

Maisha ya aina hii yanasema,hayagombi,hayadanganyi,hayajutii,hayaogopi,hayakatai,hayaingilii uhuru wa mtu,hayasemi zadi ya kile kilichopo. Najivunia hili, najivuni kuyajua na kuendelea kuyaona, yananipa USONGO.Ingawaje kuna tofauti kubwa kati ya WIVU na USONGO. Lakini naamini safari inaweza kuwa na kona.

Je unajua kuwa unajua namna maisha ya binadamu wenzetu wanajua kuwa unaishi katika mazingira gani? Nitazamapo na kukumbuka nyumbani kwetu, nikiyaona haya, napata USONGO. Ni hayo tu.