May 12, 2010

BANDARI YA ITUNGI; maji yamepungua


Wiki mbili zilizopita tumehabarishwa wkamba bandari ya Itungi iliyopo wilayani Kyela, imepungua maji kiasi ambacho Meli za MV IRINGA NA SONGEA zimeshindwa kutia nanga hapo.

Kwahiyo habari zilizonifikia hivi punde kumelazimika kutumiwa bandari Kiwira ambayo mara nyigi huokoa jahazi kutokana na kuwa na kina kirefu cha maji.

Hata hivyo kwa mwaka huu hali imekuwa tofauti kwani hata bandari ya Kiwira inakabiliwa na uhaba wa maji. Hali hiyo inatokana na kina cha maji kupungua katika ziwa nyasa.

Bandari ya Itungi Location of Itungi ipo katika Latitudo 9° 34' 60 kusini, na Longitudo: 33° 55' 60 mashariki. Hutumiwa sana kwa usafiri wa ziwa nyasa. Kwa sasa hata bandari ya Kiwira inatakiwa matumizi ya boti zinazokwenda moja kwa moja kilindini kuwapeleka abiria. Yaani meli haiwezi kutia nanga hivyo inasimama umbali kidogo kutoka bandarini hapo.

May 10, 2010

NDOA ZA MITALA

YANAYOJIRI KWA WANYASA, MALAWI
WIKI hii ndugu zangu wa Malawi wana mjadala mzito, na majadala huo umedumu kwa majuma kadhaa kuhusiana na uamuzi wa serikali kukomesha suala la ndoa za mitala.

Serikali ya Malawi inadhamiri kupiga marufuku suala la ndoa za mitala katika jamii za nchini humo. Sijui zaidi ya hapo kuna nini ila kwa hakika hili ni suala la kuongelea kila mara kuhusiana na mwenendo wa binadamu.
Watetezi wa ndoa za mitala wanadai hiyo ni haki yao na kitendo cha serikali kuingilia kati kutaka kuwapiga marufuku kutooa wanawake zaidi ya mmoja au kuolewa na wanaume zaidi ya mmoja, ni kuingilia uhuru wao wa kuishi.

Tunakumbuka katika baadhi ya mila na desturi za India wanawake wanaweza kutoa mahali na kuoa, pia kutoa mahali ya kuolewa na zaidi ya wanaume wawili. Hivyo mwanamke ndiye anayepanga hilo, na kulichagua ni namna gani aishi na wanaume wake.

Ndoa za mitala kwa Malawi inaambana na mila na desturi ya makabila yao, kwa kiasi kikubwa kwao ndoa za aina hii ni fahali na kuonyesha ukubwa wa familia n.k, sifa moja kubwa ni kuzaa watoto wengi, na kuwaozesha endapo wapo wanawake au kuwa na watoto wengi na kusifiwa.
Mara nyingi wanawake katika jamii za kabila la Wanyanja na Wachewa hawana kauli sana kuhusiana na maisha ya ndoa hususan wale wanaoishi katika mazingira ya kitamaduni. Au kufanya uchaguzi wa kuolewa na mume gani

Maana wapo wengine nasema hawana utamaduni kwakuwa wanaishi katika mazingira ambayo ni vigumu kuyafafanua kwa utamaduni wao halisi(rejea jamii zilizozuka zamani huko Venice, Italia, na uchambuzi wa Karl Marx.

Hivyo wiki hili katika jiji la Blantyre mjadala siyo haba, na sijui mwelekeo wake utafikia wapi ila serikali imesisitiza kukomesha suala hilo.
Tukienda kwa kabila la Watumbuka, hali nayo siyo tofauti sana sawa na Wahyao.
Hili ni suala ambalo jamii nyingi za Malawi lineendekeza na kuamini kuwa ni uhalali wa maisha yao. Ni wazi wanaamuni kutokana na kurithi tangu enzi za mababu, lakini kama kuna umuhimu wa kuliendeleza ni vema kuangalia nafasi ya maisha halisi kuliko kushadadia tu.
Hata hivyo serikali imefafanua kwamba uwezekano wa kuenea maambukiz ya ukimwi kunatokana na ndoa hizi, inaelezwa wkamba wengi wanaolewa/kuoa kisha kuachwa/kuachana na kujikuta wakiwa wameathiriwa na magonjwa mbalimbali ikiwemo ukimwi.
Na zaidi inaelezwa kuwa kunakuwa na ongezeko la wajane au watu walioathiriwa kisaikolojia kutokana na ndoa hizo. Wengine ni mabinti wadogo ambao huozeshwa kulingana na mila na desturi.
Ni matumaini yangu Usia Nkhoma utachangia hapa, Vincent Kumwenda, Alley Kapito.... Lol! nchito ilipo bambo..... just for u Sophie Moyo.

TUJIULIZE
Ndoa za mitala ni hatari sana?
Kuna athari za ndoa za mitala?
serikali inaingilia uhuru wa kuishi?
Binadamu tunao uhuru kiasi gani?

May 06, 2010

KAZI UKIIPENDA,ITAKUPENDA

                                             Kazi ni kuipenda
Maisha ndivyo yalivyo lakini mpangaji ni wewe. Ukiipenda kazi yako nayo itakupenda. Ukiithamini kazi yako nayo itakuthamini, ukiheshimu kazi yako nayo itakuheshimu.
Kazi ni kazi bora mkono kwenda kinywani, lakini siyo kazi yenye dhuluma ukadai bora mkono unakwenda kinywani, bali kazi ni ile halali na uifanye kwa uhalali.


Kazi yoyote ni kuipangilia, na zingine hazina ofisi ambayo utakaa kuandika kwa kalamu ya wino. Kwetu hapa nyasa kazi yetu na ofisi yetu ni mtumbwi ambao kalamu yake ni ngalawa/kafia.
Kazi hii ni ngumu lakini ndiyo inayoweza kutupatia kipato na kupanga maisha.
Kazi ukiipenda nayo itakupenda, hata kama ni ndogo aghalabu inakupa heshima.
Ndipo unapomkumbuka Vilfredo Pareto, mchumi wa kitaliano katika '2080 Theory', kwamb asilimia 20 ya mipango yako ni sawa na asilimia 80 ya matokeo'.


Ukiifanya kazi kwa bidii,maarifa na kwa asilimia zote, itakuletea ufanisi. Ufanisi unatokana na juhudi ndiyo maana hatuachi KUVUA SAMAKI. Najua jamaa zangu wa pale bandarini Chilumba, Malawi hawaachi na serikali yao imewaletea zana mpya. Hongereni. Lakini sisi tunatumia mitumbwi ya zamani na tuna uhakika wa kufanikiwa labda.