May 31, 2010

Mv Ilala, kazini, bandarini MBAMBA BAY

Hii ni meli kutoka Malawi, hapa ilikuwa pale bandarini Mbamba Bay. Hii ni bandari salama sana KARIBU SANA NYASA, karibuni unufaike na biashara zako na maisha kwa ujumla

PENDEKEZO LA WASTANI LA MFUMO MFUMO WETU WA UTAWALA

Pendekezo la wastani la mfumo wetu wa utawala.

Na Markus Honorius Mpangala, Mbinga-Ruvuma

Msingi mkubwa wa kujitawala ni maamuzi ambao yanasimamia madhumuni yaliyomo katika makabrasha yetu. Maamuzi haya yanawalenga watu wetu waliomo bila kujari kabila,nasaba na uenyeji wao. Ilimradi walengwa ni raia halali wa Tanzania.

Ziko njia nyingi za maamuzi ambayo humaanisha muundo wa utawala. Njia hizi hushirikisha pamoja kati ya wananchi,serikali yao na wawakilisha wa majimbo,kata na kadhalika. Mfumo huu unajikitia kuonyesha kuwa taifa letu linaoubunifu wake kiutawala.

Tunaweza kuunda mifumo mipya au kuikarabati ile ya zamani katika ngazi za mikoa,wilaya,tarafa, kata na vijiji. Maeneo haya ndiyo huunda taifa ambalo leo tunajivunia na kujiita Watanzania wenye Jamhuri ya Tanzania.
Usipitwe Isome

May 30, 2010

UMEWAHI KUFIKIRIA HILI KUHUSU SISI WANADAMU????/

KUNA MTU UMEWAHI KUMCHUKIA?? UNADHANI KUNA WATU WAMECHAGULIWA NA MUNGU??
......Ndiyo wapo wanaofikiria hilo,,,
Ndiyo maana wanaona wako karibu na Mungu.......... NINACHOJUA na kukiamini ni kuwa kila kiumbe duniani ni CHAGUO LA MUNGU, maana bila Mungu hakuna kitu kinachoweza kuwepo. Ndiyo maana hata SHETANI ni chaguo la Mungu, kama siyo chaguo la Mungu basi asingeumbwa.

SASA......... Mungu alitupatia akili na utashi ili tujue mema na mabaya kati yetu ili tumpendeze yeye tu. Twaweza kuishi hata bila chakula katika mazingira fulani lakini bila Mungu hatuwezi kuishi. Najua kila mtu duniani hata wewe unayesoma hapa ni CHAGUO LA MUNGU.
Waungwana nimeipenda hii kitu ya kutoka kwa FALSAFA YA ISANGO inayoandikwa na Josephat Isango au Misango.
Stori ya kipengele cha kukosoa dini leo nimeweka kando aiseeeee., lakini hata hii imekuwa poa. Mtani Fadhy upo hapo???? Da Mija, unasemaje, mtakatifu mungu wa wapare.... Ruksa kubishia Lol.....

May 29, 2010

SAFARI NJEMA DADA Diesmal

Kwanza nashukuru kunitumia picha hii baada ya kutua mjini Mbinga. Nadhani umekumbuka Frankfurt au uwongo ha ha ha na kiswahili chako kibovu eti 'nim'pika mbinga' badala ya kusema 'nimefika mbinga'. Usijali kazana safari ni ndefu hadi kuifikia Litembo dada halafu unasema una usongo wa kujimwaga kwetu nyasa.

Haya yangu mie macho tu, nakusubiri kwa hamu nadhani umeiona Mbinga sasa kazana tu mana hapo ndipo palipo nikuza na kunijuza ukiacha nyasa kwetu. Safari njema.

Hey mnasemaje kikwetu Diesmal? ha ha ha ha nimekumbuka ile lugha ngumu mweeeeeeeeeee, ha ha ha ha haya najaribu
   Gut sein reise madchen, i liebe du Diesmal......
           Ein kind bekommen....... lol

Diesmal natisha siku hizi naijua hii lugha, ha ha ha ha ha ha kideuctland chenu siyo? nami nimo eboooo! Dada Yasinta upo hapo? toto linajimwaga nyasa,litembo,kindimba na kadhalika, hebu mtakie safari njema au? Lol

May 27, 2010

HAPO VIPI?