June 03, 2010

HAPPY BIRHDAY ERICK T.K

Wazazi wema,
wanakulea vema,
hekima njema,
malezi mema.
Mungu ni mwema
akulinde vema

Nipo nawe daima
kwa mbio au muziki.
HAPPY BIRTHDATE ERICK@10 ni pazuri, kuwa na wazazi wema na wenye hakima na akili. Ubarikiwe mwana, usiache kukimbia, uwe kama mama na baba walivyo wema.

NIKUPE NINI??

Moja ya wasanii wa Mukirikiri, ila samahani nimeshindwa kutamka kwa ufasaha jina lao. Jamani ugonjwa wangu wa utamaduni ulinifanya nitulize 'boli' hapa kwa kujinufaisha na kujipendelea kutazama tu aina ya mvao wa kitamaduni.
Angalia na hapa chini kidogo iko vipi kadiri utazamazpo?
Mimi naona vizuri a.k.a African Bantu hadi nimemkumbuka Bambuu, yule mwanamuziki wa Kenya. Mwenye namba yake ya simu au anuani pepe naomba tafadhali..............Lol

May 31, 2010

Mv Ilala, kazini, bandarini MBAMBA BAY

Hii ni meli kutoka Malawi, hapa ilikuwa pale bandarini Mbamba Bay. Hii ni bandari salama sana KARIBU SANA NYASA, karibuni unufaike na biashara zako na maisha kwa ujumla

PENDEKEZO LA WASTANI LA MFUMO MFUMO WETU WA UTAWALA

Pendekezo la wastani la mfumo wetu wa utawala.

Na Markus Honorius Mpangala, Mbinga-Ruvuma

Msingi mkubwa wa kujitawala ni maamuzi ambao yanasimamia madhumuni yaliyomo katika makabrasha yetu. Maamuzi haya yanawalenga watu wetu waliomo bila kujari kabila,nasaba na uenyeji wao. Ilimradi walengwa ni raia halali wa Tanzania.

Ziko njia nyingi za maamuzi ambayo humaanisha muundo wa utawala. Njia hizi hushirikisha pamoja kati ya wananchi,serikali yao na wawakilisha wa majimbo,kata na kadhalika. Mfumo huu unajikitia kuonyesha kuwa taifa letu linaoubunifu wake kiutawala.

Tunaweza kuunda mifumo mipya au kuikarabati ile ya zamani katika ngazi za mikoa,wilaya,tarafa, kata na vijiji. Maeneo haya ndiyo huunda taifa ambalo leo tunajivunia na kujiita Watanzania wenye Jamhuri ya Tanzania.
Usipitwe Isome