Jamani mnaonaje kuhusu hili nalo??? ,,,,,....... Ngoja unajua nipo kwenye kaofisi kangu hapa??? Unajua mimi huwa sina siku ya mapumziko katika siku 7 za wiki? Labda niamue tu kupumzika, lakini ukweli siku ipo ila sitaki kupumzika..... kwani naamini nitapumzika nikioza nikiwa kaburini... AU?
JAMANI nimekaa hapa nawaza, maana Mtani Fadhy anajua kaofisi kangu kalivyo bwana..... eeeeh Hapa nawaza eti HAYA MAPENZI inakuwaje mtu unakuwa na muwasho au HISIA za kimapenzi na mtu?? Inakuwaje kwanza mtu ukawa katika hali hii jamani. Nawaza kwasababu unaweza kuwatazama WANAWAKE/WANAUME wengine yaani unaweza kumwona MWANAMKE/MWANAUME lakini usiwe na hisia naye........ LAKINI kati ya hao anaweza kutokea mtu ambaye WEWE unaamini kuwa UNA HISIA ZA KIMAPENZI KWAKE. Eti jamani mnalionaje hili. Kwanini kwa wengine huna HISIA hizo lakini unazo kwa mtu fulani. Halafu inatokea mtu anaonyesha MAPENZI kwelikweli LAKINI baada ya EMCHEKU anacharuka bin MCHARUKO huyooooooo 'hit and run' AU?
Yaani inamaana hisia hizo ni za kumchungulia mwenzio UVUNGUNI kisha ufute vumbi miguuni utimue zako bila kugeuka nyuma? Najaribu tu kuwaza haya mambo. ETI fikiria kuna watu wanaimbiana NAKUPENDA SANA NAKUPENDA SANA NAKUPENDA SANA lakini baada ya muda HAWATAZAMANI kila mtu kashika hamsa zake huyoooooo tena huko aendako anapata mtu mwingine wimbo uleule NAKUPENDA SANA NAKUPENDA SANA. inakuwaje haya? Ha ha ha ha ha SIJATINGWA ila najaribu kujenga taswira........ ha ha ha Lol..........
Huyu unamwambia NAKUPENDA SANA halafu baada ya miezi au miaka kadhaa upo na mwingine unaimba wimbo uleule NAKUPENDA SANA..... hivi mwisho wake itakuwaje mimi sina jibu sielewi. Hata kama umefunga ndoa lakini mnaachana na wimbo wa NAKUPENDA SANA unahamia kwingine AISEHHHH!!!!!!
Sawa msikose kusikiliza KWAITO, mtafute MANDOZA katika hili bonge la myuziki NKHALAKATA
June 12, 2010
MAPENZI NAYO..........
Madhumuni
maswali magumu
June 09, 2010
BADO MFULULIZO WA MAWAZO
Jamani, sasa hivi ndiyo nataka kufunga haka kaofisi kangu niende nami nyumbani. Lakini najua nikifika tu kitu cha kwanza ni kuifungua kompyuta yangu ili niendeleza mambo yangu ya kukaa na tarakilishi. Na zaidi basi nitakaa nyuma ya DSTV niangalie soka au marudio ya Tenisi au vipi, na zaidi ule muziki wa Kwaito mtamu...... Nadhani mtani anajua utamu wa soka. TUACHE HILO.....
KUNA hili jambo nilikuwa najaribu kuwaza dakika chache hizi na hadi sasa naandika naendelea kuwaza. HIVI WEWE UNAMWAMINI NANI HASA KATIKA MAISHA YAKO? Yaani UNAVYOISHI KILA SIKU KUNA MTU UNAMWAMINI SANA? KWANINI?
Unajua katika maisha yetu haya kuna wakati unakuwa na marafiki wengi sana, na wengine wanaweza kukupotosha halafu ukajuta hapo baadaye. Labda utaniuliza mimi namwamini nani. Mwenzangu yupo mtu namwamini anaitwa Yasinta Ngonyani, ni sababu nyingi na ukweli NAMWAMINI SANA. Lakini ukiniambia nikwambia sababu za KUMWAMINI, sitakwambia....
Hebu jiulize wewe unayesoma hapa UNAYEMWAMINI NA KUMWAMBIA MAMBO YAKO, HASEMI KWA WENGINE MAMBO HAYO? au UNAMWAMINI KIASI GANI? Bado mfululizo wa MAWAZO TU. ok naenda nyumbani, nimeimiss tarakilishi yangu aiseh
KUNA hili jambo nilikuwa najaribu kuwaza dakika chache hizi na hadi sasa naandika naendelea kuwaza. HIVI WEWE UNAMWAMINI NANI HASA KATIKA MAISHA YAKO? Yaani UNAVYOISHI KILA SIKU KUNA MTU UNAMWAMINI SANA? KWANINI?
Unajua katika maisha yetu haya kuna wakati unakuwa na marafiki wengi sana, na wengine wanaweza kukupotosha halafu ukajuta hapo baadaye. Labda utaniuliza mimi namwamini nani. Mwenzangu yupo mtu namwamini anaitwa Yasinta Ngonyani, ni sababu nyingi na ukweli NAMWAMINI SANA. Lakini ukiniambia nikwambia sababu za KUMWAMINI, sitakwambia....
Hebu jiulize wewe unayesoma hapa UNAYEMWAMINI NA KUMWAMBIA MAMBO YAKO, HASEMI KWA WENGINE MAMBO HAYO? au UNAMWAMINI KIASI GANI? Bado mfululizo wa MAWAZO TU. ok naenda nyumbani, nimeimiss tarakilishi yangu aiseh
Madhumuni
maisha,
mapumziko,
maswali magumu
UNAONAJE HILI katika MAISHA YAKO
Nimekaa katika kaofisi kangu lakini nikajikuta kicha kinakataa kufanya kazi. Najiona waziwazi nimesongwa na mawazo. Ingawaje wapo wanaweza kusongwa na mawazo kiasi hata wakaugua mgandamizo wake kutokana na kuwaza kwa muda mrefu, lakini kwangu ni tofauti. Nimekwisha kuugua sana suala la msongo wa mawazo lakini tiba zangu ni mazoezi, na kufanya kazi mbalimbali, kifupi mwili wangu unahimili vihoma vya kijinga kama hivi.
Ila nawaza sana leo. Nikiwazacho pengine kwasababu tu nawaza kutokana na nilivyo labda, ingawa sijui nipoje Lol... Hapo ndipo nikamkumbuka WILLIAM SHAKESPEARE. Nikakumbuka maandiko yake fulani hivi.
Yaap! Ukisoma kitabu chake cha TIMMOTH OF ATHENS(samahani jina la kwanza lina kawaida ya kunikwepa kulijua, sijui ni TIMMOTH au TIMMON maana ni muda mrefu sijakitia machoni tena. Si unajua cha kuazima hakisitiri wowowo??.....Ngoja tu).
Sasa katika maandiko yale anasema hivi HAKUNA KINACHOCHOCHEA DHAMBI KAMA HURUMA. eti mwenzangu unaonaje hii hoja. Inakuingia kichwani kweli? UKIWA NA HURUMA SANA INACHOCHEA DHAMBI wanungwana? Mimi sijui ila nilizama katika tafakuri anuai, nikajikuta nawaza hiki kipengere.
Madhumuni
maswali magumu
June 08, 2010
TANZIA; Mungu amlaze mahali pema!
Nilikuwa nimekaa nimechoka hata sikuwa na hamu ya kublogu leo, lakini kitu ninachokipenda ni lazima angalau nisome rafiki yangu Yasinta alichoandika angalau kujipendelea na kuchangamsha kichwa.
Na kweli wakati nikisoma, ghafla umeingia ujumbe wa simu ya kiganjani kutoka kwa rafiki yangu Joe Pardley, akaniuliza nina habari gani za afrika leo ambayo inanigusa.
Kwakuwa anajua kuwa maswali yake yananighadhibisha. Nitafakari kuna nini. Ndipo akaniambia Nisome kwa dada Chemi Che Mponda..
MASIKINI nilitetemeka kidogo, maana kwa wanautambuzi wanaelewa kuwa ni jambo la kawaida sana. Ndipo nikafahamu mwanamuziki ninaye mpenda na kumsikiliza tungo zake hata kama sielewi lugha yake kiasi fulani, lakini miridhimo ya kimuziki inanikolohua nafsi.
Ndipo nikabainia kuwa OLIVER N'GOMA hatunaye duniani. Nikakumbuka nyimbo nyingi sana. Kwa shukrani maridhawa kwa dada Chemi Che Mponda kwa kutuletea habari hii, kwa hakika sina mengi ya kunena, na labda niseme MUNGU AMEMPENDA ZAIDI. LAKINI NAMI NILIMPENDA PIA.
Madhumuni
habari,
Hisia za moyo,
kumbukumbu
Subscribe to:
Posts (Atom)
