Ukisoma blogu ya Mtani wangu Fadhy Mtanga a.k.a Shemeji mtarajiwa, utaelewa kwanini nasema sijatulia. Yeye anatuhabarisha sana kuhusu WOZA 2010 pale Afrika kusini. Sasa na mimi nina jukumu kidogo kuchambua fainali hizi katika tasnia ya habari, ni kazi maalum hii. Halafu jumlisha na shule, jumlsiha na kaofis kangu........ utaona bonge la KUTOTULIA.
LEO nimekuja kiduchu tu.... maana utaanza kuwaza heee mzee wa Lundunyasa imekuwaje kapotea saaaaaannaa. Usijali lakini hata Mama Mchungaji Koero amekuwa Mkulima STADI huko vijijini Miamba n.k.
SASA kuna shairi moja nimelipenda sana, lilitungwa na WILLIAM ERNEST HENLEY wa Uingereza, nimependa mistari hii jamaniiiiiiiiii
"I am the master of my Fate",
"I am the Captain of my soul"