Nikupe nini ewe rafiki? Nifanye nini kwako rafiki mwema, usiyeficha msimamo wako na kukataa kile kisichokuwa chema? hakika wajua thamani ya urafiki, wajua thamani ya ukweli na upendo kwangu, Nitakupa nini rafiki yangu? Mangapi yangu yamesemwa na ukaambiwa lakini hujanificha?
Nifanye nini maana bado najiuliza kila siku? Najua tumetofautiana mara kadhaa lakini uzuri tunajadili yanakwisha. Najua habari kadhaa zangu umezipata na pengine unashindwa kunielewa misimamo yangu kadhaa. Lakini uzuri wajua tabia,mwenendo,misimamo,mitazamo na hadidu zangu za rejea.
NIKUPE nini ewe rafiki yangu? Sema sasa nijuwe maana kusubiri nishachoka nisije nikawa MVUMILIVU HULA MBOVU. Wajua ni kwanini tumekuwa hivi, wajua ni ukweli,bila simanzi, ni upendo na uwazi. Aaah! nitakupa nini ewe mwema. Naamini mungu ajua yakuwa twajua kwamba kiasi cha mambo tuyajuayo ni sehemu ya kujua tu ingawa pia hakutoshi kuyajua.
Asante rafiki kujibu hata maswali yaelekezwayo kwako lakini yanihusu mimi. Yote tisa naweza kukuita hakimu mzuri kwa kuhukumu vizuri bila upendeleo Lol.... You know what it is rafiki. Daima umesimamia ukweli. Nakupenda sana rafiki yangu. Hivi ni nani atakaye tutenganisha? au huyu Mungu? ataweza kweli maana ananiogopa kila siku...... Lol
Napenda staili ya urafiki wetu mama, naamini ni ndugu sana kwa mengi mema. Zaidi nimeipenda picha inanikuna sana. JE URAFIKI UNASOMEWA DARASANI AU CHUO KIKUU? Thamani yeru ya urafiki ni pale tunapotazamwa kwa tofauti kumbe walaaaaaaa! Mungu mkubwa! THE SAME DRAMA