July 24, 2010

KUTOKA BAGAMOYO waungwana

                                                                      DARASANI
DARASA
Nipo hapa mjini huu wa watu wetu. Wakati nimetoka chumbani na kuingia chumba cha kupumzika nikaona nichezea Kompyuta kidogo tu. Nimekaa katika hii kompyua nimefanya ukaguzi nimeona picha hizi, hivyo siyo vibaya tukashirikishana katika KUWAZA na KUJADILI MUSTAKABALI wa vijana hawana...........,...

July 21, 2010

KARIBUNI NYASA- jamani!

Ukitokea kijiji cha Mbaha kuelekea Ndumbi utakutana Pwani hizi zinazokuonyesha uelekeo wa Lituhi.
Hapa unaona mlima kwa mbaliiiiii, ambako ndiyo Lituhi. Lakini ardhi iliyoingia ziwani inaitwa Folk Land ni eneo la Lituhi. Pna historia sana hapa kwa uvuvi wa MBASA
Karibuni

MAKALA MPYA; TANZANIA; Azimio la Arusha na miluzi ya ubepari

TANZANIA; Azimio la Arusha na miluzi ya ubepari (1)

Nmesoma mara nyingi hoja za madai kwamba sera za Ubepari ni nguzo ya uchumi wa dunia. Katika kupitia hoja hizo, nakubaliana nao kwa kiwango fulani lakini iko haja ya kuchanganua zaidi na namna ya kuinua kiwango cha hoja zao. Dai lao la kukumbatia ubepari linatokana na mfumo wa soko huria uliobuniwa na kupigiwa mbiu sana na Adam Smith ambaye aliandika katika kitabu chake cha Wealth of the Nation.

Baada ya kukaa kimya kwa kipindi kirefu licha ya kushawishiwa na wale wanaoniamini kuwa ninaweza kuzichambua sera hizo- nilipanga kunyamaza na kuangalia mustakabali wa uchumi wa dunia. Niliamini muda utasema, na sasa nimeamua kusema kwamba Miluzi mingi ya Ubepari inampoteza Mbwa mwelekeo’. ...................

                   Usipitwe, isome yote

MAKALA MPYA; Je Waafrika tunapenda sana ngono?

Je Waafrika tunapenda sana ngono?


MWAKA 2003, katika Gazeti la The Guardian la Uingereza, Mwanasafu wake Hanif Kureishi alipata kuandika ‘Huwezi kujua kamwe uliyoyatamka yataleta maana gani kwako mwenyewe au kwa mtu mwingine ama ulimwengu wa maneno utakayoyaumba utakuwaje. Lolote lile laweza kutokea. Tatizo la kukaa kimya ni kwamba tunajua nini kitatokea’.(mwisho wa kunukuu).
                      
                       usipitwe, isome

HARUNA MOSHI YUKO SAHIHI?

Ukiniambia nimlaumu HARUNA MOSHI kuamua kuondoka nchini Sweden katika klabu ya Gefle nitakwambia, kosa lake ni lipi? Ukiniambia alikuwa akilipwa kwanini kaondoka nitakwambia acha afanye anachoona bora. JE YUKO SAHIHI AU HAYUKO SAHIHI?