Moja ya mambo yanayonisumbua ni wasomi kuendeshwa kiimani na kuondoka katika uhalisia wao(siyo woteeeeeee jamani). Jambo linalonipa shida ni pale ninapomsoma msomi kwa njia ambayo tunaamini anatuelemisha. Kila kona ya dunia unakutaka na sifa ya mtu aitwaye msomi, lakini nimekuwa muumini sana wa jamaa mmoja wa China anayitwa SUN TZU kwanza naamini hakuwa msomi walau kuwa Porofesa aaaahhh samahani Profesa au Mwalimu.... mmmmmh labda nimekosea, waama!
Kuufikia Uprofesa kuna kanuni zake. Kufikia Udaktari wa Falsafa kuna kanuni zake. Kuufikia sijui utaalamu wa fizikia au kemia kuna kanuni na utaalamu wake. Na je ni nani anaweza kubainisha sifa halisi za Msomi. Na anatumia vigezo gani. Ipo imani ambayo imeenea kidogo kwa baadhi ya watu kwamba ukiwa mjuvi wa vijimambo vingi walau si haba nchini mwetu unaweza kuonekana karaha au kero naam, utakuwa sijui naniiiii
Lakini jambo linalosumbua akili zangu ni kujua kwanini naweza kuishi bila kuwategemea wasomi. Bado najiuliza kwanini Barefoot College kina sifa ambazo wasomi hawatakiwi. Wasomi ni magwiji ni mafundi wa mambo mengi. Lakini sifa hii inaweza kumweka msomi huyu kutojifunza kwa WAPUMBAVU? Na hapo ninajiuliza njia ya kwanza ya kujifunza ni ipi kati ya kuona na kusimuliwa. Maana hata Mpumbavu anaweza kukusimulia na ukaamini na kujifunza.
Naamini labda kinachonisumbua akili yangu ni kutokubaliana na mambo ya kishabiki tu bila kupima na kuamini ndivyo ipasavyo. Ndiyo maana kwa muda mrefu nimetukanwa sana niliposimama na kusema sihitaji kelele kutoka Washington na London ziseme Rais Mugabe ni dikteta na mhuni, nikasema wale waliomwita Mandela gaidi wako wapi, na walipoanza kutengeneza suala hili na kuuvika ulimwengu kuwa dunia inasumbuliwa na ugaidi walidhani sote tuwe watumwa.
Hapana, ndiyo maana nasema endapo suala la kujifunza misemo au kunukuu falsafa za WAPUMBAVU ni UJINGa basi UPUMBAVU na UJINGA wa kwanza utakuwa ni KUZALIWA kwa binadamu maana yapo matendo mengi sana yanayoambatana na BAHATI MBAYA. Lakini kanuni hii inatokana na nini? Na kwanini usipoelewa kitu ukihitimisha haraka bila kujipima umeelewa? Na kwanini usiwekeza kuelewa? naacha nimetingwa kibingwa......
Basi ni uzembe, basi ni ushabiki ambao sitokuwamo na sitoukubali kwakuwa watu wote wanaamini vuguvugu(kumbuka hawaamini bali wanashabikia kama tupo dimbani). Sifa za wasomi zinajulikana na sifa ya WAPUMBAVU NI ZIPI? Maana kama tunakubali kuwa UJINGA ni jambo baya basi huenda kuamini WASOMI ndiyo wanajua kila kitu ama wao kujiweka katika daraja la juu kwamba wanaweza kufahamu mengi nao ni ubaya zaidi, basi hakuna haja ya kuwepo kwa WAPUMBAVU.
Ninapenda mijadala mitamu inayoumiza kichwa kwa tafakuri hasa pale tunapowaona magwiji wa kufikiri wakijaribu kuibua hisia na hasira za dhahania, kuliko uhalisi. Basi tukishafika hapo tunaweza kujihoji tena kipi kilianza kati ya UPUMBAVU na KUZALIWA? Na kama WAPUMBAVU ni sehemu ambayo mabingwa wa kusoma wanaweza kujifunza kwao, basi hitimisho kwangu halitokwisha kuamini KUNA UHABA WA FALSAFA na labda neno langu baya ni UMASIKINI WA FALSAFA, Kile unachoamini
Ndiyo, siyo kila FALSAFA inatakiwa kutokana na msomi maana kuna matusi mengine ni FALSAFA. Na siamini falsafa ni zile zitolewazo na wagwiji wake wanaoitwa wasomi ama wale wa kale. Je unaamini nini katika harakati hizi zinazoshabikiwa na watu kama hujapima na kujiridhisha kwamba ndivyo ilivyo? Endapo unajiingiza tu na kudhani ndivyo, basi wewe hustahili kuwepo hapo kwani HUNA FALSAFA, na la zaidi inakata roho na kurudi upya. Je nani anaweza kutupatia SIFA ZA WAPUMBAVU?
Naendelea kutafakari..... nitarudi kinyasa nyasa tu..... najiuliza ZIKO WAPI SIFA ZA WAPUMBAVU
CHANZO;
MARKUS, MWALIMU NYERERE ALIANDALIWA NA NANI? isome hapa
>
maoni ya kaka John Mwaipopo na Kaka Matondo
Tujadiliane......................