Binadamu tuliumbwa kwa kusudi maalumu. Na kila mmoja yupo duniani kwa kusudio maalumu. Na kila mmoja analojukumu lake hapa duniani. Lakini binadamu tunajua kuwa Mungu anatupenda sana, ingawa hajawahi kutueleza moja kwa moja. Kwa imani twaenenda kwamba Mungu yupo nasi muda wote kwa shida na raha. Na wapo wanaojiuliza wakati wa shida kwamba Mungu yuko wapi na kwanini hawasikii?
Lakini wapo wengine wanajiuliza ni kweli UPENDO wa Mungu unafanana na ule ambao wanadamu wanaweza kuutoa. Je ni kweli binadamu wanakupenda wewe hapo ulipo? Ili ujue wanakupenda ungependa wakufanyie nini? Na kwasababu gani wakufanyie hilo unalodhani ni upendo wao kwako? Je ni kwanini unampenda Mungu usiyemuona wakati unashindwa kuamini kuwa RAFIKI yako anakupenda? Je wema wa mungu huonekanaje na wema wa RAFIKI huonekanaje?
LABDA
Ni kwani binadamu tunaingiwa na HISIA za KUTAMANI KUFA? je maisha yetu tunahitaji yawe na furaha kila wakati?Au ni kitu gani kinatufanya uwaze hilo jambo la kusema NATAMANI KUFA? wangapi wanatamani wanatamani KUFA lakini hawajafa? Ni wangapi hawatamini KUFA lakini wamekufa? NAWAZA KWANINI WANAOTAMANI KUFA HAWAFI na wale WASIOTAMANI KUFA wanakufa?
