Mioyo yenu imo Moyoni mwangu daima
Daima nasadiki, blogu ni amani kwanu.
Nimekubali kwamba blogu imenipa mengi maishani. Nimepata marafiki wengi na daima nimwenzi mwalimu wangu Ndesanjo Macha. Nilijifunza takribani mwaka mzima kabla ya kuanzisha blogu yangu hii.

Na wakati naamua kuanzisha nawashukuru watu wote waliokuwa nami tangu zamani. Wenye kiu ya kujua namna blogu inavyotupatia wasaa wa kujifunza. Nimejifunza mengi kwa kweli. Miaka 4 nilitimiza mnamo Agosti 31 mwaka huu, ila sikupata fursa ya kuandika hapa kutokana na kukabiliwa na harakati kadhaa.
Ndipo nikaamua kutumia mikono yangu salama kutengeneza hiki. Blogu hii ilianza Agosti 2007, eneo la Sinza Kijweni,lakini wazo lilianzia kwetu nyasa ndani ya Gheto langu,mitaa ya Maliwa/Mission, eneo wanaloishi wamisionari na sisi akina kajamba nani ambao wazazi wetu walikuwa watumishi wao. Ni mtaa niupendao daima umenikuza kwa mengi jamani.
Ni mtaa ambao wazo la Upadri lilimea na kustawi kabla halijawa kimeo, kisha nikalichakachua. lakini baba ananiita Paroko hadi kesho.
nikiwa nasoma maandiko ya Ndesanjo Macha kisha niliporudi mjini nikawasiliana naye. tukapeana mbinu na mengine. hakika ikawa mwalimu mzuri, hadi enzi za kusome uandishi wa raia. nakushukuru mkubwa kwa ushauri wako.
Namshuruku rafiki yangu mtani wangu au shemeji yangu Fadhy Mtanga kunitembelea ndani ya wiki niliyotimiza siku hii. Nawashukuru sana wanablogu wote. Wale walioapata kukasirishwa na maoni yangu kwao, au andiko langu hapa basi wajue kuwa AMANI IWE KWAO DAIMA.
Nilifanya hivyo kutokana na wasaa wa kujifunza. Pia napenda sana uhalisi kuliko kujivika sura nisiyokuwa nayo, kwamba shujaa pengine ni mwoga tu niliyeshindwa kupambana na woga. Namshukuru rafiki yangu kipenzi Yasinta Ngonyani kwa kuwa nami daima kisha hata kukubali wazo langu la kuanzisha blogu ya pili ambayo kwa hakika, ilinipa ongezeko la akiba ya akaunti. Amani ya iwe nawe Yasinta Ngonyani. a.k.a mama maswali magumu. Niwashukuru nyoooteeee,
Lakini naweka ................................................................
naomba ujaze jina lako manaa sina upendeleo. Na ndugu zangu wanyasa walioniandikia baruapepe zao kuifurahi na kushauri basi nawaambia. 'Siku mapigo yangu yatakapokoma basi mjue nitakufa kwa misingi na imani niliyojiwekea. Daima nitakuwa yuleyule na ukipenda niite tu Mcharuko mwema..
Nikwambie KITU? NAWAPENDA SANA TU. ila msije mjini, kisha mtasikiliza Mandoza katika bonge la kwaito la Nkhalakatha.

