October 13, 2010

SUBI SABATO!!!

Subi binti Sabato,
Subi binti wa leo,
Subi dada'ngu
wapi mahala pangu;
nianze kulizala wangu,
kulilia wako utaalamu,
nini swahiba wangu,
kimekusibu mwenzangu,
wajua nakudai,
yale maandiko anuai?
ya tiba mwilini,
Subi Kwanza Jamii,
magonjwa ya jamii,
Subi a.k.a Subiraga binti,
u binti safi muwali,
magonjwa tufafanulia,
walai elimu tulijipatia,
 vipi Subi a.k.a Subiraga,
mwana wa Iringa ya Ilula?
sijui makwenu wapi,
ila Iringa anuai

NIMEKUMBUKA MAANDIKO YA DADA SUBI SABATO wakati ule pale katika jarida la KWANZA JAMII
nimekumbuka sana, ngoja niingie maktabani nisome maelezo yale. Dada Subi natumaini hujambo.

October 10, 2010

KAZI + SHULE= RATIBA NGUMU

Kwa kweli nimebanwa sina jinsi nalazimiika kukubali kwamba ratiba imekaa katika mantiki iliyopinda. Lakini jukumu hilo nitaliweza tu. Blogu ipo sana siyo lile wazo la mzee wa Nyegerage kwamba itakufa lini. Nipo sana waungwana

WASOMI NA WANASIASA WANATUREJESHA UTUMWANI?

KOLE OMOTOSO ameibua mjadala mkali kwa baadhi ya watu barani afrika. Mnamo septemba 10, mwaka huu aliandika makala iliyochapishwa na Mail&Guardian, la nchini Afrika Kusini.

Katika makala hiyo mwandishi huyo anaeleza mambo mengi juu ya demokrasia ya bara la afrika na namna uongozi wa nchi mbalimbali ikiwemo Afrika Kusini namna wanavyoshindwa kuziendesha nchi zao.
 SOMA MAKALA NZIMA USIPITWE