October 13, 2010

SUBI SABATO!!!

Subi binti Sabato,
Subi binti wa leo,
Subi dada'ngu
wapi mahala pangu;
nianze kulizala wangu,
kulilia wako utaalamu,
nini swahiba wangu,
kimekusibu mwenzangu,
wajua nakudai,
yale maandiko anuai?
ya tiba mwilini,
Subi Kwanza Jamii,
magonjwa ya jamii,
Subi a.k.a Subiraga binti,
u binti safi muwali,
magonjwa tufafanulia,
walai elimu tulijipatia,
 vipi Subi a.k.a Subiraga,
mwana wa Iringa ya Ilula?
sijui makwenu wapi,
ila Iringa anuai

NIMEKUMBUKA MAANDIKO YA DADA SUBI SABATO wakati ule pale katika jarida la KWANZA JAMII
nimekumbuka sana, ngoja niingie maktabani nisome maelezo yale. Dada Subi natumaini hujambo.