09 March 2011

Camilla mwanangu mpenzi

Februari 21 sikupa salamu zangu zangu. Naomba usifikirie kama nimekutenga mwanangu. Mie mjomba wako siku hizi ni balaa tupu maana wenye viofisi vyao wananifanya niwe nawatumikia wao muda wote. Pia usisahau zile harakati nilizomwambia mama yako ambaye mimi ni dada yangu ukipenda ni rafiki yangu kama samaki na maji.
Mwanangu Camilla najua ulishanisamehe. Na leo nakuambia kuwa nakuombea maisha marefu na yenye kila aina ya raha. Lakini kumbuka wazazi ni kila kitu kwani wao walikupa mwangaza na uendako ukumbuke hilo. Mimi mjomba wako unaweza hata kunisahau kidogo lakini najua utakumbuka kuwa mjomba ana harakati nyingi ambazo zinamweka mbali na jamii yetu.

Niseme nini mwanangu, lakini ukweli ni kwamba nakupenda sana. Nakuhitaji sana maana wewe ni muhimu kama neno lenyewe lilivyo muhimu. Amani iwe kwako mwanangu na siku yako ya kuzaliwa ilikuwa poa sana. Ila usije bongo mwezi huu hadi wa tano maana kuna joto lilelile uliloniambia nitakaa kwenye maji kama samaki sababu kuna joto sana

6 comments:

 1. Nimetumwa na mjombao niandika haya. Mjomba Markus wala usijali kabisa. Kwani kazi ni msingi wa maisha. Nafurahi kwa kunikumbuka na ndio siku yangu ilikuwa pouwa kabisa. N kuhusu ile ahadi wala usiwe na shaka kabisa mjomba. Na mjomba wote hapa nyumbani wanakusalimu. Ahsante sana. UPENDO DAIMA!!

  ReplyDelete
 2. Marcus nikuabie kitu kaka?? Unampenda sana mjomba wako, unampenda mno majukumu kaka ndio yantufanya tuonekane kama hatuna mioyo ya upendo lakin Marcus tunamioyo ya upendo sana kaka tunampenda mjomba wetu pia tunampenda sana na tutaendelea kumpenda daima.

  ReplyDelete
 3. Naongeza kwa mjomba wetu, Camila kuwa huku sasa hivi nauli za daladala zimepanda, labda usubiri kama serikali itatufikiri na sisi baadaye kutupandishia mshahara, ili ukija niweze kukutembeza kule feri ukaone samaki,...najua labda kipindi hicho samaki watakuwepo, kwani sasa hivi wamekuwa adimu, kwasababu wavuvi wanapata hasara, wakileta samaki hakuna sehemu ya kuwahifadhia kwasababu ya tatizo la umeme. Majokofu yapo likizo...
  Labda kipindi hicho umeme utakuwepo , na huenda TV , yangu itakuwa imepona, kwani iliharibika na ukienda kwa fundi anakuambia umeme hakuna nitakutengenezea na nini!
  Camila, nakupenda sana mjomba wangu, sipendi ukija huku upate shida, ...sasa hivi sukari bei juu, maharage ambayo mnayalima huko na kuuza kwa bei poa huku wanatulangua kwa shilingi 1600/- bei yake inakimbizana na dola ya Wamarekani.
  Dsm ni nzuri, lakini ukitaka kwenda mjini unaweza ukatumia masaa matatu , na ukitaka kwenda Msasani au Kunduchi beach ukitokea Mbagala au Gongolamboto utatumia masaa matatu hadi manne, mtu aliyekwenda Morogoro anafika na kupumzika wewe hujafika .
  Oh, mkuu nilidhania natunga kisa kwenye blog yangu !
  Ni hayo tu mkuu

  ReplyDelete
 4. Mjomba, ni kweli maisha ya yamekuwa yakipoteza maana kiasi cha kufikia kuchuja kutokana na wapenzi wenyewe kuwa na mawazo ya ubinafsi.

  Utakuta watu wameoana lakini kila mmoja anakabili changamoto za maisha peke yake, hali ambayo humfanya atumie nguvu kubwa kutafuta ushindi wa matatizo yake.

  Mjomba, nimeshuhudia wengi ambao hawajui umuhimu wa kuheshimiana mbele za watu. Utakuta mwanamke/mwanaume akimwaibisha mwenzake mbele za watu kwa kumfokea, kumwita jina baya, kumtusi, kumtoa kasoro na hata kumdhalilisha.

  Kitendo hiki ni kibaya na maumivu yake hudumu kwa muda mrefu akilini mwa mtendewa...nikwambie jambo lingine mjomba:

  Wakati mwingine harakati za maisha huleta huzuni, kwa mfano, kama wanandoa watafiwa, kuuguza, kufukuzwa kazi, kupoteza mali kwa kuibiwa na matukio kama hayo huondoa furaha.

  Ukimuona mwenzako anakwenda nje ya mstari wa jamii mrejeshe na kuzidi kumkumbusha kila siku wajibu wake, hii inasaidia kumuweka sawa mahali anapokosea.

  UMENIPATA MJOMBA??

  ReplyDelete
 5. - She is cute, nimetekewa na nimekosa lugha ya kuongea. mungu amtangulie na kumfunika na utukufu wake kila afanyacho

  ReplyDelete

Andika maoni yako