September 25, 2012

Tunaomba kambi ya JWTZ, Katiba itamke mipaka



Wakazi wa Wilaya mpya ya Nyasa wameiomba serikali kuanzisha kambi za Jeshi la Wananchi nchini katika makao makuu ya wilaya hiyo, Mbamba Bay ili kukabiliana na hali mbaya inayoweza kujitokeza hapo baadaye.

Wakizungumza katika kongamano la Usalama wa raia, wakazi wa Wilaya ya Nyasa, wameiomba serikali kuangalia uwezekano huo ili  kuimarisha ulinzi wa mji wa Mbamba Bay ambao ni lango kuu la kuingilia kwa upande wa Tanzania kutokea kusini.

Wamesema kuwa ingawa serikali imepiga hatua katika mazungumzo yake na serikali ya Malawi, bado wakazi wa wilaya hiyo mpya wanaishi kwa hofu na wasiwasi mkubwa.

“Sisi wakazi wa mpakani hasa hapa Nyasa tunaishi kwa wasiwasi, tunaomba Jeshi la Ulinzi lije kuweka kambi maalumu hapa, tunafahamu wapo polisi, lakini wenyewe hawatoshi kwani tunahitaji ulinzi zaidi,” alisema mkazi mmoja wa Mbamba Bay

Kaika hatua nyingine, baadhi ya wakazi wa wilaya Nyasa wamebainisha maoni yao kuwa ni vema Katiba Mpya itakayopatikana hapo baadaye baada ya kuidhinishwa na Bunge la Katiba, itamke waziwazi mipoaka ya nchi yetu.

Wakazi hao wanasema kuwa pamoja na uhuru walionao kuingia nchi za Msumbiji au  Malawi bado kunahitajika uwazi zaidi na Katiba ya nchi yetu inalazimika kutaja mipaka ya nchi yetu ili kulinda mipaka na kuwa mwongozo wake.

Wamesema Katiba inatakiwa kuchukua nyaraka zote za mipaka na kubainisha mipakaya ndani ya nchi, na nje ambako tunapakana na nchi mbalimbali.

Wakitolea mifano Namanga, Sirari, Kasumulu, Tunduma, Mbamba Bay na mingine mkoani Kagera. Aidha, walisema kuwa ni lazima Katiba itamke kuwepo kwa Vituo vya kudumu vya Polisi katika vijiji vyote katika jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

NB: maoni ya wakazi wa vijiji vya Tingi, Kingirikiti, Chiwanda, Kilosa, Mtipwili, Peramiho, na Mbamba Bay

September 24, 2012

ORODHAYA MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI OKTOBA NA SEKRETARIETI YA AJIRA

Sekretarieti ya AJIRA ya utumishi wa UMMA imatangaza majini ya waombaji kazi ambao wanatakiwa kuripoti katika vituo vyao ili wafanyiwe USAILI ifikapo mwezi Oktoba(ujao).

Hivyo kwa wakazi wa Mkoa wa RUVUMA wanatakiwa kuangalia taarifa zaidi ili kujua kama majina yao yamechaguliwa. Aidha kwa wale ambao hawataona majina yao ina maana hawakufainikiwa kuchaguliwa na inawezekana nikiwemo mimi MARKUS MPANGALA ambaye nilitajaria kurudi mkoani kwangu.

Majina hayo yametolewa hapa BONYEZA

UWEKEZAJI KATIKA KILIMO CHA MITI-MUFINDI, IRINGA


KILIMO CHA MITI YA MBAO, NGUZO NA KARATASI mjini MUFINDI.
FRESH FARM(T) inakuhakikishia UAMINIFU wa hali ya juu. Tayari wapo waliowasilisha taarifa zao kuhitaji MASHAMBA ili wafanye uwekezaji katika kilimo cha miti ya nguzo, karatasi na mbao. 


FRESH FARM(T); Wanauza mashamba yenye miti (ardhi pamoja na miti); maeneo ya Mufindi-Iringa kilomita 75 kutoka Iringa mjini). Bei ni tsh 600,000 hadi 1,000,000 kwa ekari. 

MAMLAKA: Taratibu za umilikaji/umilikishwaji wa ardhi/ununuzi/upangaji tunazingatia SHERIA YA ARDHI YA MWAKA 1999, SHERIA NAMBA 5. wahi sasa.


Fresh Farms (T)-Albert Sanga (Director) 0766 742414/0719 127 901

e-mail; stepwiseexpert@googlemail.com
Markus Mpangala (Advertising Officer)- 0764936655
e-mail: mwanazuoni27@gmail.com

KIJIJI CHA LIWIHI WILAYANI MBINGA

Nchi yetu ina mazingira mazuri sana ambayo yanaashiria kuwa msingi wa maeneeleo ya wananchi wetu ni ARDHI. Tukiwa na Ardhi yenye rutuba ama maeneo tu kama haya ni lazima kutakuwa mafanikio kwa jamii zetu. Kwa msingi huo hakuna njia nzuri kama kuitumia ardhi kwa manufaa ya familia na jamii nzima kwa ujumla kwa maendeleo ya taifa.

Hapa ni kijiji cha LIWIHI katika KATA ya MATIRI wilayani MBINGA.

Picha: Dennis Komba.