October 22, 2012

MGANDA LIULI

Mganda ni moja ya ngoma zinazopendwa sana katika wilaya ya Nyasa. mganda ni sehemu ya ushirikiano wa kijamii kwani hutumika kuwaunganisha na kufurahia utamaduni wetu. 
Hapo ni boma la Mganda la Liuli wakati wa sherehe za kila mwaka za mganda katika vijiji mbalimbali.

Picha na James Zotto, UDSM

MABADILIKO YA TAREHE YA USAILI

  MABADILIKO YA TAREHE ZA USAILI
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma anawatarifu waombaji kazi kuwa tarehe za usaili zimebadilika kutokana na mabadiliko ya tarehe ya sikukuu ya Eid el Hadjj.

 AIDHA, UKAGUZI WA VYETI UTAANZA SAA 1:00 HADI 1:45 ASUBUHI SIKU YA MTIHANI WA MCHUJO.

HIVYO USAILI UTAFANYIKA KAMA IFUATAYO:

1. USAILI WA MCHUJO KWA MIKOA YA MOROGORO, MANYARA, PWANI, ARUSHA, KILIMANJARO NA TANGA UTAFANYIKA TAREHE 29/10/2012.

2. USAILI WA MAHOJIANO KWA MIKOA YA MOROGORO, MANYARA, PWANI, ARUSHA, KILIMANJARO NA TANGA UTAFANYIKA TAREHE 30/10/2012.

3. USAILI WA MCHUJO KWA MKOA WA DAR ES SALAAM UTAFANYIKA TAREHE 27/10/2012 CHUO KIKUU KISHIRIKI CHA ELIMU (DUCE) - CHANG’OMBE

4. USAILI WA MAHOJIANO KWA MKOA WA DAR ES SALAAM UTAFANYIKA TAREHE ZILIZOPANGWA AWALI (01/11/2012 NA 02/11/2012) NA

UTAFANYIKA KATIKA OFISI ZA SEKRETARIETI YA AJIRA ZILIZOKO MAKTABA YA TAIFA BARABARA YA BIBI TITI MOHAMED

TUNAOMBA RADHI KWA USUMBUFU WOWOTE UTAKAOJITOKEZA.

NAFASI YA KAZI OKTOBA 18, MWISHO OKTOBA 31, 2012

Kwa wale wanaohitaji nafasi za kazi katika Sekretarieti ya AJIRA nchini. Wanaweza kuangalia nafasi ya kazi katika tovuti ya sekretarieti hiyo kwa ku-dowloand tangazo zima;

SOMA HAPA

KILIMO CHA KISASA CHA MPUNGA LWIKA KATIKA VIKUNDI VYA WAKULIMA

Bonde la mto Lwika lipo katika kijiji cha Lundo na linatengenisha vijji viwili, Lundo na Ngindo. Bonde la mto Lwika linafaa sana kwa kilimo cha Mpunga na Miwa. Katika kuboresha maisha ya wananchi kilimo cha miwa kimekuwa na nafasi kubwa kama ilivyo kwa kilimo cha Mpunga. kwa sasa wakulima wanaweza kutumia zana za kisasa ikiwemo Matreka. Pichani Trekta la Kikundi cha Umwagiliaji cha LWIKA. Treka hilo limenunuliwa kupitia Mpngo wa Uendelezaji wa Sekta ya Kilimo katika Wilaya ya Nyasa(DADPS). Kilimo ni uti wa mgongo kwa wakazi wengi wa Wilaya ya Nyasa ikiwemo Mahindi, Mtama, Ulezi, uvuvi na mengineyo. Kikundi cha wakulima wa eneo hilo kimepewa ekari 2200. 

Picha ya Hoops Kamanga idara ya maendeleo Wilaya ya Nyasa.

Huyu ni mzee Mputa, ambaye alikuwa afisa Uvuvi, kwa sasa ameshastaafu. Hapo alikuwa katika ukaguzi wa kilimo cha Mpunga katika bonde la mto Lwika.


UZURI WA FUKWE ZA ZIWA NYASA, MABADILIKO YA TABIA NCHI

Hapa ni ufukwe wa Ziwa Nyasa katika eneo la Matenje (Matenje Beach). Kijiji cha Matenje kipo kilomita chache sana kutoka makao makuu ya wilaya ya Nyasa, yaliyoko mji wa Mbamba Bay.
Fukwe nyingi zimejaa uzuri na haitakuwa maajabu kuona wimbi la watalii kandokando ya ziwa nyasa pindi miundombinu itakapoimarishwa. Na hakuna shaka nchi yetu ni nzuri na harakati za kuboresha ni nzuri kwa kiwango chake.

KARIBUNI SANA NYASA
Picha: Hoops Kamanga, ambaye alikuwa katika utafiti wa MABADILIKO YA TABIA NCHI kwa muda wa majuma matatu wilaya ya Nyasa.

UPIMAJI WA MRADI WA MAJI LUNDU

MTAALAM WA MAJI, EGBERT JEREMY AKIANGALIA RAMANI YA MITARO YA MAJI KATIKA KIJIJI CHA LUNDU KANDOKANDO YA ZIWA NYASA.

UJENZI WA ZAHANATI KATIKA WILAYA YA NYASA

Jengo la hapo chini ni Zahanati ya ya Kijiji cha Mbaha baada ya kukamilika kwa ukaratabati wake. Kijiji chicho kipo katika Kata ya Mbaha, kwenye Tarafa ya Ruhuhu iliyopo wilaya mpya ya Nyasa. Juhudi za usambazaji wa huduma za afya zimekuwa kubwa ili kusogeza huduma kwa wananchi wa maeneo hayo na kupata huduma za afya kwa usahihi. Hii ni harakati mojawapo ya maendeleo, kama inavyosemwa MTU NI AFYA.

Jengo la hapo chini ni Zahanati ya ya Kijiji cha Luhindo likiwa katika awamu ya kwanza ya kukamilisha kuwa kituo kidogo cha afya. Juhudi za usambazaji wa huduma za afya zimekuwa kubwa ili kusogeza huduma kwa wananchi wa maeneo hayo na kupata huduma za afya kwa usahihi. Hii ni harakati mojawapo ya maendeleo katika wilaya ya Nyasa

Jengo linalofuata hapo chini  ni Zahanati ya ya Kijiji cha Mitawa baada ya kukamilika kwa ujenzi wake. Kijiji chicho kipo katika  wilaya mpya ya Nyasa. Hii ni harakati ya kusogeza huduma  za afya kwa usahihi. Hii ni harakati mojawapo ya maendeleo kwa wananchi, ingawa juhudi zinahitajika. 
 Ujenzi wa Zahanati ya ya Kijiji cha Mkali kilichopo katika Kata ya Lipingo, kwenye Tarafa ya Ruhekei iliyopo wilaya mpya ya Nyasa.  Ujenzi wa kituo hicho unaendelea.


Katika jamii yoyote suala la kupiga hatua ni muhimu sana. Na jamii haiwezi kupiga hatua kama haijaanza kutengeneza hatua husika. ili mafanikio yapatikane ni lazima juhudi zifanyike, ni muhimu kutunza kile kinachoanza kutengenezwa ili tuweze kuboresha. Pengine Zahanati hizi zisiwe na kiwango bora cha huduma za afya. lakini ni heri kuanza kwa hatua hiyo kuliko kutokuwepo kabisa. Nchi yako kwnaza.
PCIHA ZOTE NA Hoops Kamanga, Nyasa

October 18, 2012

TANGAZO LA USAILI KWA WAOMBAJI WA KAZI SEKRETARIETI YA AJIRA NCHINI

Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania inawatangazia wote walioomba nafasi za kazi wanatakiwa kwenye USAILI ifikapo tarehe 25 oktoba hadi tarehe 02 Novemba, hizo zitakuwa siku za usaili kwa waombaji nafasi za kazi.

TAARIFA ZAIDI SOMA HAPA

AJALI YA LORI BARABARA YA MBINGA-SONGEA


Ajali ya lori la ujenzi la kampuni ya Wachina inayojenga barabara ya Mbinga-Songea ambayo imetokea leo asubuhi saa tatu. Ajali hiyo imetokea katika kijiji cha Lipumba ambacho kipo kilometa chache tu kutoka Mbinga mjini.

Hata hivyo hakuna mtu aliyeruhiwa katika ajali hii. Soma zaidi Hapa

October 17, 2012

HARAKATI ZA MAENDELEO WILAYA YA NYASA, KARIBU KUWEKEZA


Wilaya ya Nyasa ni miongoni mwa Wilaya mpya zilizoanzishwa na serikali ya awamu ya nne. Habari za kuundwa wilaya ya Nyasa nilianza kuzisikia mwaka 1993 nikiwa shule ya msingi. Lakini mwaka huu Wilaya ya Nyasa imezinduliwa rasmi na shughuli za maendeleo zinaendelea ili kukidhi mahitaji ya wananchi. Katika harakati hizo ni pamoja na huduma ya Maji ambayo ni muhimu sana kwa wananchi wa Wilaya hiyo. Hapa ni picha mbalimbali ambazo zinaonyesha suala la upatikanaji wa maji katika vijiji mbalimbali wilayani humu.  Bila shaka wageni na wenyeji watavutiwa kuwekeza katika wilaya mpya ambayo fursa mbalimbali zinajitokeza. karibuni. Picha zote na Hoops Kamanga
 Chanzo cha Mradi wa maji kikifanyiwa ukaguzi.
 Tenki la Maji katika mradi wa maji katika kijiji cha Ng'ombo wilaya ya Nyasa
 Mradi wa Maji katika kijiji cha Kindimba Juu ambao umekamilika na wananchi wanategemea kutumia siku chache zijazo. Hapo fundi anamalizia marekebisho katika tenki.

THOMAS ULIMWENGU NA MBWANA SAMATTA

Thomas Ulimwengu(kushoto) na Mbwana Samatta(kulia) wakiwa katika picha ya utani(kuchekesha), muda mfupi kabla ya kupanda ndege kuelekea Tunis, nchini Tunisia.

HABARI; Shirikisho la soka barani afrika(CAF) limeteua waamuzi wapya wa kuchezesha mechi ya marudiano ya nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya mabingwa watetezi ESPERANCE ya Tunisia dhidi ya TP Mazembe a.k.a Nguvu ya Mamba ya DRC. Soma hapa zaidi

Dakika chache zilizopita nimezungumza na Mbwana Samatta, ameniambia lazima waing'oe Esperance. Tumuombee na mwenzake Thomas iliw wawakilishe vema. 

MITI NI UHAI, KILIMO NI UHAI

Picha ya 1: mradi wa umwagiliaji maji katika kijiji cha Lundo. mradi huo umekamilika kadiri ya mkataba baina ya Wakulima na wawezeshaji. mradi huo umeanza kutumika ili kuwezesha zao la kilimo cha Mpunga kufanyika kwa urahisi. Mavuno ya zao hilo huwawezesha wakulima kupata faida kiuchumi na kujiongezea kipato. Mpunga ni zao linalotegemewa kwa kiwango kikubwa katika wilaya mpya ya Nyasa.

Picha ya 2 chini: miche ya miti katika kijiji cha Kitanda. Wilaya zote za mkoa wa Ruvuma zipo kwenye harakati za kuhakikisha mkoa huo unakuwa na mandhari mazuri na mazingira yanalindwa kwa kuhimiza upandaji miti.
Kilimo cha umwagiliaji kimeendelea kushika aksi katika vijiji mbalimbali katika wilaya ya Nyasa. hapa ni moja ya mifereji ya kupitishia maji ili yaingie shambani.
PICHA na Hoops Kamanga

KILIMO CHA MITI KIYAHA

MRADI wa mali asili na bustani ya miche ya miti katika kijiji cha kiyaha, Mbinga. 
Hii ni miongoni mwa harakati za upandaji miti katika mkoa wa Ruvuma, hivyo kila Wilaya inahusika katika kuyalinda mazingira na kutengeneza mji wa kijani(green city) kama jiji la Mbeya linavyojulikana kwa jina mashuhuri Green city. Hivyo harakati za upandaji miti Wilaya ya Mbinga na Nyasa zimepamba moto, na hapa mdau wetu anatuletea taarifa hizo.

Picha ya: Hoops Kamanga

October 16, 2012

FRESH FARMS(T) YATEMBELEWA NA MHADHIRI WA CHUO KIKUU CHA MOSHI

Siku tatu zilizopita; Fresh Farms (T) tulitembelewa na mgeni Mr. Emmanuel Lulandala ambaye ni mhadhiri wa chuo kikuu cha Ushirika Moshi. Tulimzungusha kwenye baadhi ya mashamba yetu ya miti ya mbao na karatasi na alijifunza mengi. Katika picha hii: tulikuwa katika bustani ya miche ya miti ya mbao na karatasi, ambayo tunatazamia kuipanda kwenye ekari mpya 340 kwenye msimu huu unaoanza Novemba. Kutoka kushoto: Emmanuel Lulandala, Katikati: Albert Nyaluke Sanga (C.E.O- Fresh Farms (T), Kulia: Jadili Kaguo (Farm Mager-Fresh Farms (T). Fresh Farms (T) ni biashara iliyopo chini ya NYALUKE GROUP LTD (Nyaluke Business Empire)