October 27, 2012

ELIMU: SEKONDARI ZA WILAYA YA NYASA ZAENDELEA KUBORESHWA

Wengi wanafahamu kuwa Wilaya ya Nyasa ni miongoni mwa Wilaya zilizoundwa na kuzinduliwa mwaka huu. Kila wilaya inapoundwa basi masuala mengi yanahitaji kufanyiwa kazi. Moja ya masuala hayo ni elimu. Wilaya Nyasa kwa sasa kuna mengi yanafanyika yenye lengo la kuongeza maendeleo na kuboresha zaidi. Shule zinajengwa au kuboreshwa ili kuweka mazingira mazuri ya kusomea. Kufuatia suala hilo, Nyasa inaelekea kuhimiza ujenzi wa shule mpya na zile za zamani kurekebishwa kwa manufaa wa wananchi wote. Hapa ni baadhi ya shule ambazo zinafanyiwa marekebisho na zilizokamilika. Elimu ni Uhai, kama Misitu ni Uhai.
Picha ya juu inaonyesha sehemu ya majengo la shule ya Sekondari ya Mkwaya baada ya kukamilika kwa ujenzi wake na kuboresha mazingira ya shule hiyo.
Picha ya pili inaonyesha nyumba ya Mwalimu katika shule ya Sekondari ya Mkwaya. Hii ni moja ya mikakati ya kuweka mazingira mazuri kwa walimu wa sekondari katika wilaya ya Nyasa.

Picha inaonyesha majengo mawili ya madarasa katika Sekondari ya Kipololo. Ujenzi wa Sekondari hiyo unatokana na fedha za mradi wa serikali kuboresha Elimu ya Sekondari(MMES) kwa kushirikiana na LGCDG kwa mwaka wa fedha 2006/2007 
Picha ya mwisho inaonyesha jengo la shule ya Sekondari ya Ruanda. Jengo hilo ni miongoni mwa majengo yanayotakiwa kukarabatiwa ili kuboresha hali yake na kuweka mazingira mazuri ya kusomea.

PICHA ZOTE na Hoops Kamanga, Nyasa

NYUMBANI LUNDU

Picha hii inaonyesha maeneo ya kijiji cha Lundu. Maeneo hayo ni mtaa wa Maliwa au Missionari, na wka upande wa magharibi kushoto unaonekana mlima ambao unaitwa Chipyaghela. Kisha maji ya ziwa Nyasa yanaonekana. Huu ndio mji ulionikuza na kunilea, katika mitaa yangu ya Maliwa, au missionari.
Picha hii imepigwa na kaka Egbert Jeremy aliyeko wilaya ya Nyasa katika shughuli za ujenzi wa miundo mbinu. Lundu ni miongoni mwa vijiji ambavyo anaendelea kujenga miundombinu ya wilaya hiyo. Karibuni kuwekeza wilaya ya Nyasa ambayo imeanza kutoa fursa mbalimbali. KARIBUNI NYASA

October 22, 2012

MGANDA LIULI

Mganda ni moja ya ngoma zinazopendwa sana katika wilaya ya Nyasa. mganda ni sehemu ya ushirikiano wa kijamii kwani hutumika kuwaunganisha na kufurahia utamaduni wetu. 
Hapo ni boma la Mganda la Liuli wakati wa sherehe za kila mwaka za mganda katika vijiji mbalimbali.

Picha na James Zotto, UDSM

MABADILIKO YA TAREHE YA USAILI

  MABADILIKO YA TAREHE ZA USAILI
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma anawatarifu waombaji kazi kuwa tarehe za usaili zimebadilika kutokana na mabadiliko ya tarehe ya sikukuu ya Eid el Hadjj.

 AIDHA, UKAGUZI WA VYETI UTAANZA SAA 1:00 HADI 1:45 ASUBUHI SIKU YA MTIHANI WA MCHUJO.

HIVYO USAILI UTAFANYIKA KAMA IFUATAYO:

1. USAILI WA MCHUJO KWA MIKOA YA MOROGORO, MANYARA, PWANI, ARUSHA, KILIMANJARO NA TANGA UTAFANYIKA TAREHE 29/10/2012.

2. USAILI WA MAHOJIANO KWA MIKOA YA MOROGORO, MANYARA, PWANI, ARUSHA, KILIMANJARO NA TANGA UTAFANYIKA TAREHE 30/10/2012.

3. USAILI WA MCHUJO KWA MKOA WA DAR ES SALAAM UTAFANYIKA TAREHE 27/10/2012 CHUO KIKUU KISHIRIKI CHA ELIMU (DUCE) - CHANG’OMBE

4. USAILI WA MAHOJIANO KWA MKOA WA DAR ES SALAAM UTAFANYIKA TAREHE ZILIZOPANGWA AWALI (01/11/2012 NA 02/11/2012) NA

UTAFANYIKA KATIKA OFISI ZA SEKRETARIETI YA AJIRA ZILIZOKO MAKTABA YA TAIFA BARABARA YA BIBI TITI MOHAMED

TUNAOMBA RADHI KWA USUMBUFU WOWOTE UTAKAOJITOKEZA.

NAFASI YA KAZI OKTOBA 18, MWISHO OKTOBA 31, 2012

Kwa wale wanaohitaji nafasi za kazi katika Sekretarieti ya AJIRA nchini. Wanaweza kuangalia nafasi ya kazi katika tovuti ya sekretarieti hiyo kwa ku-dowloand tangazo zima;

SOMA HAPA

KILIMO CHA KISASA CHA MPUNGA LWIKA KATIKA VIKUNDI VYA WAKULIMA

Bonde la mto Lwika lipo katika kijiji cha Lundo na linatengenisha vijji viwili, Lundo na Ngindo. Bonde la mto Lwika linafaa sana kwa kilimo cha Mpunga na Miwa. Katika kuboresha maisha ya wananchi kilimo cha miwa kimekuwa na nafasi kubwa kama ilivyo kwa kilimo cha Mpunga. kwa sasa wakulima wanaweza kutumia zana za kisasa ikiwemo Matreka. Pichani Trekta la Kikundi cha Umwagiliaji cha LWIKA. Treka hilo limenunuliwa kupitia Mpngo wa Uendelezaji wa Sekta ya Kilimo katika Wilaya ya Nyasa(DADPS). Kilimo ni uti wa mgongo kwa wakazi wengi wa Wilaya ya Nyasa ikiwemo Mahindi, Mtama, Ulezi, uvuvi na mengineyo. Kikundi cha wakulima wa eneo hilo kimepewa ekari 2200. 

Picha ya Hoops Kamanga idara ya maendeleo Wilaya ya Nyasa.

Huyu ni mzee Mputa, ambaye alikuwa afisa Uvuvi, kwa sasa ameshastaafu. Hapo alikuwa katika ukaguzi wa kilimo cha Mpunga katika bonde la mto Lwika.


UZURI WA FUKWE ZA ZIWA NYASA, MABADILIKO YA TABIA NCHI

Hapa ni ufukwe wa Ziwa Nyasa katika eneo la Matenje (Matenje Beach). Kijiji cha Matenje kipo kilomita chache sana kutoka makao makuu ya wilaya ya Nyasa, yaliyoko mji wa Mbamba Bay.
Fukwe nyingi zimejaa uzuri na haitakuwa maajabu kuona wimbi la watalii kandokando ya ziwa nyasa pindi miundombinu itakapoimarishwa. Na hakuna shaka nchi yetu ni nzuri na harakati za kuboresha ni nzuri kwa kiwango chake.

KARIBUNI SANA NYASA
Picha: Hoops Kamanga, ambaye alikuwa katika utafiti wa MABADILIKO YA TABIA NCHI kwa muda wa majuma matatu wilaya ya Nyasa.

UPIMAJI WA MRADI WA MAJI LUNDU

MTAALAM WA MAJI, EGBERT JEREMY AKIANGALIA RAMANI YA MITARO YA MAJI KATIKA KIJIJI CHA LUNDU KANDOKANDO YA ZIWA NYASA.

UJENZI WA ZAHANATI KATIKA WILAYA YA NYASA

Jengo la hapo chini ni Zahanati ya ya Kijiji cha Mbaha baada ya kukamilika kwa ukaratabati wake. Kijiji chicho kipo katika Kata ya Mbaha, kwenye Tarafa ya Ruhuhu iliyopo wilaya mpya ya Nyasa. Juhudi za usambazaji wa huduma za afya zimekuwa kubwa ili kusogeza huduma kwa wananchi wa maeneo hayo na kupata huduma za afya kwa usahihi. Hii ni harakati mojawapo ya maendeleo, kama inavyosemwa MTU NI AFYA.

Jengo la hapo chini ni Zahanati ya ya Kijiji cha Luhindo likiwa katika awamu ya kwanza ya kukamilisha kuwa kituo kidogo cha afya. Juhudi za usambazaji wa huduma za afya zimekuwa kubwa ili kusogeza huduma kwa wananchi wa maeneo hayo na kupata huduma za afya kwa usahihi. Hii ni harakati mojawapo ya maendeleo katika wilaya ya Nyasa

Jengo linalofuata hapo chini  ni Zahanati ya ya Kijiji cha Mitawa baada ya kukamilika kwa ujenzi wake. Kijiji chicho kipo katika  wilaya mpya ya Nyasa. Hii ni harakati ya kusogeza huduma  za afya kwa usahihi. Hii ni harakati mojawapo ya maendeleo kwa wananchi, ingawa juhudi zinahitajika. 
 Ujenzi wa Zahanati ya ya Kijiji cha Mkali kilichopo katika Kata ya Lipingo, kwenye Tarafa ya Ruhekei iliyopo wilaya mpya ya Nyasa.  Ujenzi wa kituo hicho unaendelea.


Katika jamii yoyote suala la kupiga hatua ni muhimu sana. Na jamii haiwezi kupiga hatua kama haijaanza kutengeneza hatua husika. ili mafanikio yapatikane ni lazima juhudi zifanyike, ni muhimu kutunza kile kinachoanza kutengenezwa ili tuweze kuboresha. Pengine Zahanati hizi zisiwe na kiwango bora cha huduma za afya. lakini ni heri kuanza kwa hatua hiyo kuliko kutokuwepo kabisa. Nchi yako kwnaza.
PCIHA ZOTE NA Hoops Kamanga, Nyasa