MICHAEL NCHIMBI akandika kwenye mtandao wa Facebook kuhusu Wilaya ya Nyasa. Kupitia mtandao wa NYASA akasema kuwa; .... "Jamani hivi Nyasa hakuna matatizo yoyote yale ya kijamii? Sababu ndugu Komba(John) mbunge wa jimbo la Nyasa hajawahi kusimama Bungeni tangu lianze tarehe 30 kueleza matatizo ya wananchi wa Nyasa"!
Mbunge wa Jimbo la Mbinga Magharibi, Kapteni John Komba akifungua Zahanati ya Tumbi, wa kwanza kulia ni Katibu wa CCM Wilaya ya Mbinga Anastia Amasy
WADAU WAKACHANGIA YAFUATAYO;
1. JOSEPH NDOMONDO ... akasema, "Huyo mtu vijana wenye mtazamo tulimkataa, But(lakini) CCM, pesa ya wananchi na akina mama wakinyasa ndiyo waliyompa nafasi tena. Kwahiyo hata hajasimama bungeni hiyo imekula kwetu. Kwahiyo guys(vijana) tuwaelimishe wamama(wanawake) wapendwa wa Nyasa ili Nyasa iwe mfano 2015 tumbwage. But i'm not interested with political now. Pamoko kwa sana ila mje Nyasa siyo kwenye Facebook tuuu@Joe.
2. JAMES ZOTTO, akasema haya ........ " Kwani ni lazima aongee kila Bunge?"
3. MAURICE NCHIMBI ... akachangia pia, " Acha siasa bwana Zotto kwani Bunge lililopita aliongea nini..."
4. JAMES ZOTTO,
Akarejea tena kuchangia ..."Aliongea mpaka wetu na Malawi na Huduma za Jamii lakini wanaomlaumu John Komba ni wanafiki sana maana wao ndio wa kwanza kumpigia debe na kumchagua. Kwani alichaguliwa na nani? Je, nani alijitolea kutoa elimu kwa wapiga kura na kuwafahamisha wanyasa kuwa tunataka mabadiliko? Si Komba tu, ni mfumo mzima umedorora! Labda hapa nitaeleweka, nitagombea 2015, Mtanisapoti?
5. MARKUS MPANGALA, .....
Nami nikajongea na kusema haya ..."Kaka James Zotto, kabla hujagombea una kazi kubwa ya kufanya naomba hilo wazo sogeza hadi 2020. Nadhani sasa tushughulikie hili unalofanyia kazi sasa na mengineyo. Suala la John Komba kutoongea jamani inabidi tujiulize nani KERO ipi inatakiwa kuzungumziwa na hatua gani zilichukuliwa ama zinafanyiwa nini. Binafsi kuna juhudi zinanifurahisha sana ndio maana nazijaza kwenye blog hata kama ni kidogo lakini zinaleta matumaini. Mimi natamani ELIMU na AFYA ziwe kipaumbele. Je, mbunge wetu anaweza kufanya kila kitu kuhusu Nyasa? Na kila jambo linategemea Bunge? Kama tulivyo na desturi yetu ya kujitolea kwa maendeleo yetu Wanyasa, naomba tudumishe hilo. Kaka Hoops Kamanga ananipa mengi na kuelewa Nyasa inaelekea wapi. Nina miaka mitano mbele naamini Nyasa itakuwa na fursa nyingi mno na habari za Dar es salaam syndrome zitaanza kutoweka angalau kidogo.
6. HOOPS KAMANGA,
Naye akachangia haya, ..............." Markus
lazima tukubali kuwa vijana na wasomi wa leo tuna tatizo la kulalamika
pengine bila hata kujifikirisha nn kiini cha ttz kumlaumu komba kuwa
haongei bungeni ni kutojua kinachoendelea nyasa jamaa ana influnce kubwa
sana kwenye hii serikali nyasa hv
leo kuna miradi mikubwa ya maendeleo ambayo hatukuwahi kuiona kwa
serikali hii ya ccm sion mwakilishi atakaeisaidia nyasa zaidi ya huyu
kuna haja gani kuongea bungeni wakat ukipeleka kimemo kwa waziri
unatekelezewa hv mnajua nani ali push ishu ya wilaya mpya na mwez ujao
halmashauri inaanza.....kwa nafasi zetu tuanze ss kurudisha fadhila
nyasa napendekeza tuanzishe online harambee tukusanye fedha kila baada
ya miezi 3 au 6 tuanze kuwanunulia wadogo zetu vitabu nawasilisha.







