November 15, 2012

NAFASI ZA KAZI, MWISHO NOVEMBA 29, 2012

SEKRETARIETI YA AJIRA NCHINI

INATANGAZA NAFASI ZA KAZI. Soma hapo JUU katika LINK

Details for TANGAZO LA KAZI Swahili 15 Novemba 2012


PropertyValue
Name:TANGAZO LA KAZI Swahili 15 Novemba 2012
Description:Mwisho wa kupokea barua za maombi ni Tarehe 29-Novemba-2012
Filename:TANGAZO LA KAZI Swahili 15 Novemba 2012.pdf
Filesize:180.32 kB
Filetype:pdf (Mime Type: application/pdf)
Creator:psrsweb
Created On:11/15/2012 11:57
Viewers:Everybody
Maintained by:Editor
Hits:863 Hits
Last updated on:11/15/2012 12:00
Homepage:

ELIMU NI UHAI, WATU WAPE ELIMU

Sehemu ya jengo la madarasa katika shule ya Sekondari Lituhi, mjini Lituhi. Kwa sasa hali ya mabadiliko imekuwa kubwa kutokana na shule hiyo kukabidhiwa kwa serikali ambapo mwanzoni ilikuwa ikimilikiwa na wazazi ambao waliamua kujenga sekondari hiyo kwa lengo la kuondokana na kero ya ukosefu wa elimu kwa watoto wao.

Hosteli za shule ya Sekondari ya Mbamba bay, mjini Mbamba Bay. Hatua hii itasaida kuondoa ukosefu wa mabweni katika shule nyingi za Kata katika wilaya ya Nyasa. Kwakuwa sekondari ya Mbamba Bay ni ya Kata basi inaweza kuchukuliwa kama mfano wa shule zingine ili kuondokana na kero mbalimbali za elimu na kuwafanya wanafunzi wasome kwa utlivu wakiwa na maeneo mazuri ya kusomea.
Jengo la madarasa matatu katika shule ya sekondari ya Linda iliyopo nje kidogo ya mji mkuu wa wilaya ya Nyasa, Mbamba Bay. Ujenzi wa madarasa hayo unatarajiwa kukamilika ifikapo mwanzoni mwa mwaka 2013. Ambapo Ujenzi wake ulianza katika mwaka fedha 2008/2009. Hii ni hatua nzuri ambayo inahitaji msukumu zaidi ili kukamilisha huduma za elimu kwa wakazi wa mji wa Linda na wilaya Nyasa kwa ujumla.


Madrasa ya shule ya sekondari ya Wukiro, iliyokarabatiwa kwa baadhi ya vifaa vya LCDGC, ambapo ukarabati katika majengo hayo haujakamilika. matarajio yake ni kukamilishwa mwanzoni mwa mwaka ujao 2013.

PICHA ZOTE NA HOOPS KAMANGA, Nyasa.

November 14, 2012

SHULE ZA AWALI NYASA ZINAKABILIWA NA CHANGAMOTO LUKUKI


Na Albano Midelo, Nyasa
SERIKALI kupitia wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi iliamua kuanzisha mfumo wa elimu ya awali katika shule za msingi kwa lengo la kuwaandaa watoto wenye umri kuanzia miaka mitano.
Wizara ya elimu imedhamiria kuhakikisha kuwa watoto wenye umri wa miaka mitano hadi sita wanasoma darasa la awali kabla ya kuanza kuingia shule ya msingi wanapokuwa na umri wa miaka saba.
Uchunguzi uliofanywa katika kata za Kihagara na Liuli umebaini kuwa madarasa ya awali katika shule hizo yanakabiliwa na changamoto mbalimbali hali ambayo inaathiri utoaji wa elimu hiyo muhimu kabla ya kuanzia shule za msingi.

Wanafunzi wa Darasa la Awali wapatao 90 katika Shule ya Msingi PUULU, Kata ya LIULI, wilayani Nyasa wakiwa katika darasa ambalo halina dawati hata moja.

Mwalimu wa taaluma katika shule ya msingi Ndonga kata ya Kihagara Amos Kilongo anasema shule hiyo ina darasa la awali lenye wanafunzi 37 ambao wanasomea kwenye mti kutokana na kukosekana kwa chumba cha darasa na kwamba mwalimu anayefundisha katika darasa hilo ni aliyemaliza kidato cha nne.
“Wanafunzi wa darasa la awali hawana darasa wanasomea chini ya mti,pia darasa halina madawati wa awali wanakaa  wakati wa mvua wanafunzi hao wanasome katika kanisa katoliki ambalo tumewaomba wamiliki wa kanisa hilo wamekubali kutusaidia’’,alisisitiza.
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kihagara Anet Ngindo anasema shule hiyo ina darasa la awali lenye wanafunzi 52 ambao wanasomea chumba cha shule ya msingi wakifundishwa na mwalimu ambaye hajapata mafunzo ya ualimu na sio mwajiriwa analipwa posho kupitia michango inayochangwa na wazazi.
Mwalimu mkuu katika shule ya msingi Tumbi  Evaristo Ndiwu anasema katika shule yake kuna darasa la awali lenye watoto 45 ambalo halina chumba cha kusomea ambapo mwalimu wake hana taaluma ya ualimu ni mhitimu wa kidato cha nne analipwa posho kutokana na michango ya wazazi na walezi.
Katika shule ya msingi Mango,mkuu wa shule hiyo anasema katika shule yake kuna darasa ka awali lenye wanafunzi 60 ambao hawana chumba cha kusomea na  wanafundishwa na mwalimu ambaye hajapata mafunzo ya ualimu sio mwajiriwa badala yake analipwa posho na wazazi kati ya shilingi 30,000 hadi 50,000 kwa mwezi.
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Ngehe Silivanus Mbeya anasema katika shule yake kuna darasa la awali lenye watoto 36 ambalo halina chumba cha kusomea na linafundishwa na mwalimu ambaye amehitimu kidato cha nne hana mafunzo ya ualimu analipwa posho na wazazi ambayo haikidhi mahitaji ya mwalimu huyo.

Uvuvi ni shughuli inayoongeza kipato na ukuaji wa uchumi kwa wakazi wa wilaya ya nyasa. hapa wavuvi wakiwa kazini.

Katika shule ya msingi Puulu  mwalimu mkuu wa shule hiyo Cathibert Maluka anasema katika shule yake kuna darasa la awali lenye wanafunzi 90 na kwamba wanafunzi hao wanakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo na ukosefu wa madawati ambapo wanafunzi wote wanasoma kwa kukaa chini.
“Darasa la awali katika shule yetu limebahatika kuwa na walimu wawili ambao wamepata mafunzo rasmi ya kufundisha wanafunzi wa darasa la awali hali ambayo inawawezesha kutoa elimu ya awali kulingana na malengo ya wizara ya elimu licha ya wanafunzi kusomea chini’’,alisema .
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Nkali Erasmus Haule  anasema shule hiyo yenye jumla ya wanafunzi 210 ina darasa la awali lenye wanafunzi 45 ambao hawana darasa badala yake wanasomea kwenye banda ambalo jioni linatumika kama klabu cha pombe na kwamba mwalimu anayefundisha hajasomea.
Katika shule ya msingi Hongi  kwa mujibu wa mwalimu mkuu Simon Ndunguru shule hiyo ina darasa la awali lenye wanafunzi 52 changamoto kubwa hakuna chumba maalum cha kusomea na kwamba mwalimu anayefundisha sio mwajiriwa na wala hajasomea kufundisha darasa la awali.
Katika shule ya msingi Mwongozo yenye wanafunzi 654 inakabiliwa na changamoto ya ubovu wa darasa la awali lenye watoto 81 halina sakafu lina mwalimu mmoja ambaye hana mafunzo ya ualimu ,hajaajiriwa analipwa posho na wazazi wenye watoto hao
Baadhi ya wadau wa elimu katika kata za Kihagara na Liuli ambao ni Neema Msumba,John Ndunguru,Joel Makelele,Melikion Mapunda na Victor Komba wametoa wito kwa serikali kuhakikisha kuwa kila shule ya msingi inajenga darasa rasmi kwa ajili ya elimu ya awali badala ya shule nyingi kutumia vyumba vya shule ya msingi.
Wameitaka wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi kuhakikisha kuwa kila darasa la awali inapeleka walimu waliopata mafunzo rasmi ya namna ya kufundisha watoto wa awali badala ya tabia ambayo inafanywa na shule nyingi kuwatumia vijana ambao wamehitimu kidato cha nne huku wakiwa hawajapata elimu ya ualimu.
Mratibu elimu kata ya Liuli Abrahamu Challe amesema kata yake imejipanga kuhakikisha kuwa changamoto zote zinazoikabili elimu ya awali katika kata yake yenye shule saba zinatafutiwa ufumbuzi haraka ikiwemo kuwa na chumba rasmi kwa ajili ya awali,walimu na madawati.
Challe ametoa wito kwa serikali kutumia mfumo wa uboreshaji wa elimu ya awali kama ilivyokuwa kwa uboreshaji wa elimu ya msingi na sekondari kwa kujenga  vyumba viwili vya madarasa kwa kila shule na kusisitiza kuwa vifaa vyote vya ujenzi vitolewe na serikali na wananchi waachie ujenzi.
Afisa elimu msingi katika Halmashauri ya wilaya ya Mbinga David Mkali ambaye anahusika na wilaya ya Nyasa anasema elimu ya awali ni sera ya wizara ya elimu kuhakikisha kila shule ya msingi inakuwa na darasa la awali kwa lengo la kuinua elimu hapa nchini.
Ameahidi kushirikiana na viongozi mbalimbali wakiwemo madiwani,watendaji wa vitongoji,vijiji,kata,tarafa pamoja na wenyeviti wa vijiji kuhakikisha wanahamasisha wananchi katika maeneo yao kusimamia ujenzi wa madarasa ya awali na kutengeneza madawati ili watoto hao waweze kusoma katika mazingira bora.
“Ni ukweli madarasa ya awali yaliyo mengi yanafundishwa na walimu wasiopata elimu ni kutokana na uhaba mkubwa wa walimu uliopo katika shule nyingi nchini,lengo ni kuhakikisha tunapata walimu wa kutosha ikibidi hata kuwatumia walimu wanaostaafu kufundisha katika madarasa ya awali’’.alisisitiza.

Unaweza kuwasiliana na mwnadishi kwa anuani ifuatayo: albano.midelo@gmail.com,simu 0766463129

UHARIBIFU WA MAZINGIRA KIJIJI CHA NDUMBI??

 Zipo taarifa kwamba kampuni ya uchimbaji ya makaa ya mawe, TANCOOL katika kijiji cha NDUMBI kilichopo wilaya ya Nyasa imesababisha uharibu wa mazingira ndani ya kijiji hicho. Taarifa hizi zimeifikia mtandao huu wa KARIBUNI NYASA kupitia kwa mdau wetu Egbert Jeremy, ambaye yupo kwenye wilaya hiyo katika shughuli za utengenezaji wa Barabara na mradi mkubwa wa mami safi na salama wilayani humo. 
Kutokana na suala hili, mtandao huu unafuatilia kwa karibu taarifa za kampuni ya TANCOOL ili kubaini ukweli, na ikiwezekana kuishauri njia na umuhimu wa kulinda mazingira mbali ya mradi wao wa uwekezaji. Tuna imani wataelewa na watasaidia ulindwaji wa mazingira ya kijiji cha NDUMBI ambacho kama kitaharibiwa bila shaka yoyote kinaweza kuwa Jangwa kutokana na hali yake ya hewa kukosa uoto wa asili.

MKEKA HADI MBINGA

Hii ni barabara ya Mbinga kutoka Songea mjini. Barabara hii ilikuwa mbovu kwa muda mrefu, lakini sasa imetengenezwa kwa kiwango cha Lami. Kwa sasa suala la usafiri baina ya miji ya Songea na Mbinga imerahisishwa kutokana utengenezwaji wa Barabara hii kwa kiwango cha Lami ambayo itachangia ukuaji wa uchumi baina ya miji hii. Ujenzi wa Miundombinu kama hii inasaidia sana kukuza biashara na ongezeko la kipato miongoni mwa wananchi ama wafanyabiashara. Shughuli za kiuchumi na fursa mbalimbali zitajitokeza zaidi na kuufanya mji wa Mbinga kukuza uchumi wake maradufu. Maendeleo ni uhai. Na sasa unaweza kusafiri salama kabisa bila makorongo, magema, au vikwazo vingine barabarani. Ni mkeka tu huo hadi Mbinga ukitokea Songea. KARIBUNI KUWEKEZA

November 09, 2012

WADAU WA MAENDELEO YA WILAYA YA NYASA WAJADILI MUSTAKABALI WA WILAYA YAO

 MICHAEL NCHIMBI akandika kwenye mtandao wa Facebook kuhusu Wilaya ya Nyasa. Kupitia mtandao wa NYASA akasema kuwa; .... "Jamani hivi Nyasa hakuna matatizo yoyote yale ya kijamii? Sababu ndugu Komba(John) mbunge wa jimbo la Nyasa hajawahi kusimama Bungeni tangu lianze tarehe 30 kueleza matatizo ya wananchi wa Nyasa"! 
 
 Mbunge wa Jimbo la Mbinga Magharibi, Kapteni John Komba akifungua Zahanati ya Tumbi, wa kwanza kulia ni Katibu wa CCM Wilaya ya Mbinga Anastia Amasy 

 WADAU WAKACHANGIA YAFUATAYO;

1. JOSEPH NDOMONDO ... akasema, "Huyo mtu vijana wenye mtazamo tulimkataa, But(lakini) CCM, pesa ya wananchi na akina mama wakinyasa ndiyo waliyompa nafasi tena. Kwahiyo hata hajasimama bungeni hiyo imekula kwetu. Kwahiyo guys(vijana) tuwaelimishe wamama(wanawake) wapendwa wa Nyasa ili Nyasa iwe mfano 2015 tumbwage. But i'm not interested with political now. Pamoko kwa sana ila mje Nyasa siyo kwenye Facebook tuuu@Joe.

2. JAMES ZOTTO, akasema haya ........ " Kwani ni lazima aongee kila Bunge?"

3. MAURICE NCHIMBI ... akachangia pia, " Acha siasa bwana Zotto kwani Bunge lililopita aliongea nini..."

4. JAMES ZOTTO, 
 Akarejea tena kuchangia  ..."Aliongea mpaka wetu na Malawi na Huduma za Jamii lakini wanaomlaumu John Komba ni wanafiki sana maana wao ndio wa kwanza kumpigia debe na kumchagua. Kwani alichaguliwa na nani? Je, nani alijitolea kutoa elimu kwa wapiga kura na kuwafahamisha wanyasa kuwa tunataka mabadiliko? Si Komba tu, ni mfumo mzima umedorora! Labda hapa nitaeleweka, nitagombea 2015, Mtanisapoti?

5. MARKUS MPANGALA, ..... 
 Nami nikajongea na kusema haya ..."Kaka James Zotto, kabla hujagombea una kazi kubwa ya kufanya naomba hilo wazo sogeza hadi 2020. Nadhani sasa tushughulikie hili unalofanyia kazi sasa na mengineyo. Suala la John Komba kutoongea jamani inabidi tujiulize nani KERO ipi inatakiwa kuzungumziwa na hatua gani zilichukuliwa ama zinafanyiwa nini. Binafsi kuna juhudi zinanifurahisha sana ndio maana nazijaza kwenye blog hata kama ni kidogo lakini zinaleta matumaini. Mimi natamani ELIMU na AFYA ziwe kipaumbele. Je, mbunge wetu anaweza kufanya kila kitu kuhusu Nyasa? Na kila jambo linategemea Bunge? Kama tulivyo na desturi yetu ya kujitolea kwa maendeleo yetu Wanyasa, naomba tudumishe hilo. Kaka Hoops Kamanga ananipa mengi na kuelewa Nyasa inaelekea wapi. Nina miaka mitano mbele naamini Nyasa itakuwa na fursa nyingi mno na habari za Dar es salaam syndrome zitaanza kutoweka angalau kidogo. 

6. HOOPS KAMANGA, 

Naye akachangia haya, ..............." Markus lazima tukubali kuwa vijana na wasomi wa leo tuna tatizo la kulalamika pengine bila hata kujifikirisha nn kiini cha ttz kumlaumu komba kuwa haongei bungeni ni kutojua kinachoendelea nyasa jamaa ana influnce kubwa sana kwenye hii serikali nyasa hv leo kuna miradi mikubwa ya maendeleo ambayo hatukuwahi kuiona kwa serikali hii ya ccm sion mwakilishi atakaeisaidia nyasa zaidi ya huyu kuna haja gani kuongea bungeni wakat ukipeleka kimemo kwa waziri unatekelezewa hv mnajua nani ali push ishu ya wilaya mpya na mwez ujao halmashauri inaanza.....kwa nafasi zetu tuanze ss kurudisha fadhila nyasa napendekeza tuanzishe online harambee tukusanye fedha kila baada ya miezi 3 au 6 tuanze kuwanunulia wadogo zetu vitabu nawasilisha.