December 06, 2012

HAPA NA PALE WILAYANI MBINGA

Kilimo cha Kahawa husaidia kuongez akipato na kukuza uchumi wa wakazi wa wilaya ya Mbinga. Pichani mkulima akifurahia mavuno yake. 

Hii ni moja ya sehemu ya kukumbukwa sana. Ni mji wa Mbuji uliopo wilayani Mbinga. Mji wa mbuji unasifika kwa kuwa na na Mwamba huu ambao hutembelewa na watu wengi sana kujionea maajabu. Mwamba huu hutembelewa pia na wanafunzi wa shule mbalimbali katika ziara za kimasomo ili kujifunza mengi zaidi. Mji wa Mbuji hupokea wageni wengi kutokana na mwamba huu ambao haujaandikwa vya kutosha katika vitabu vya historia.

Mandhari ya wilaya ya Mbinga.

Picha zote kwa hisani ya credo Paul, mkazi wa Mbinga.

UKIMWI, AJIRA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA MBINGA


Na Aaron Kinunda, Mbinga
Mambo niliyoochunguza nikiwa MBINGA ambayo kimsingi yanahatarisha ustawi na maisha ya wanambinga wote kiujumla.
1. Uharibifu wa mazingira uliokithiri ambao unatishia uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara.
2. Kuongezeka kwa kasi maambuzi ya UKIMWI. Hali hii ni mbaya zaidi, kwa haraka haraka unakuja kugundua kuwa takribani karibu katika kila mtaa kuna familia kadhaa ambazo zinawaathirika wanaotumia ARV. 
maeneo ya wilaya Mbinga
Mbaya zaidi wengi ni vijana wenye watoto wadogo na ndio nguvu kazi ya jamii. Hali hii ni mbaya sana kwani kuna hatari baada ya miaka kadhaa tukawa na yatima wengi sana na wazee wakabakiwa na majukumu mazito ya kulea watoto hao. Kinachosikitisha zaidi ni ile hali ya watu kutochukua tahadhari wala kujali na pale wanafunzi wa shule zetu za kata kujikuta wakiingia kwenye huu mtandao mkubwa wa UKIMWI.
3. Ongezeko la vijana wasiojishughulisha na kazi yoyote na badala yake kubaki kucheza Kamali na kuiba mazao na mifugo ya wazee wao.
Stendi kuu ya Usafiri, Mbinga
HALI INATISHA KWELI, JARIBU KUCHUNGUZA MAENEO UNAYOTOKEA NA UONE HALI HALISI NA NINI SULUHISHO? HATUA ZA MAKUSUDI INABIDI ZICHUKULIWE VINGNEVYO....

UKATAJI MITI NA UUZAJI ARDHI HOLELA WASHAMIRI MBINGA

Na Robert Hyera, Mbinga

Habari zenu,
Kuna mambo machache tu nataka nikwambieni. Katika wilaya ya Mbinga kuna watu wanamiliki ardhi bila hati miliki za ardhi. Kwa sasa kama hujui kuna wageni ambao wananunua ardhi kwa bei ya chini sana ili baadaye wanufaike.
Ardhi inaporwa na werevu, wenyeji tumebaki mikono mitupu, mbali na hilo leo Mbinga kuna wageni weeeengi ambao wananunua miti na kuchana mbao kwa rahisi sana. Bei ya miti hiyo ni shilingi elfu 11 had 20. 

Mandhari ya Mbinga katika kilimo cha kahawa ambalo ni zao kuu linaloongeza kipato cha wenyeji wa Wilaya hiyo, iliyopo mkoani Ruvuma.

Llakin sehemu nyingine kama Iringa mti huohuo unauzwa elfu 85. Kwa sasa 65% ya miti iliyopandwa zamani yote imekatwa. Kwa kuwa mazingira ndio kila kitu kwa binadamu, nilijaribu kuongea na viongozi wachache nnaowafahamu wakaniambia watachukua hatua lakini hakuna kilichofanyika. 
Sasa hebu tusaidiane nyie wote mnaotoka Mbinga tutafanyaje ili kulinda mazingira? Kwa hili la hati miliki, sisi wenye uelewa tuwaelimishe watu wanaotuzunguka waende ofisi za ardhi za wilaya kwa ajili ya kupata hati miliki za ardhi vinginevyo tutakosa hata sehemu ya kupanda mahindi ya kuchoma.

Oktoba 19, via Facebook

December 04, 2012

HAPA NA PALE WILAYANI NYASA

Shamba la Mtama na mikorosho la shule yya sekondari ya Lituhi

Shamba la Mpunga lililolimwa katika vyanzo vya Maji kwenye kijiji cha Mkako.

Bomba la mradi wa Maji Kindimba Juu.

KUITWA KWENYE USAILI DESEMBA 6&7

WALIOOMBA KAZI KATIKA SEKRETAIETI YA AJIRA NCHINI.

SOMA HAPA ....

December 02, 2012

TAARIFA KWA WAWEKEZAJI WAPYA KATIKA KILIMO CHA MITI YA MBAO, KARATASI NA NGUZO.

Fresh Farms & Tours (T), biashara tanzu ya Anesa Co.,Ltd (Nyaluke Business Empire); inayojishughulisha na upandaji, utunzaji na uendelezaji wa mashamba ya miti ya mbao, karatasi na nguzo-mkoani Iringa. Pia inahusika na uvunaji na usambazaji wa mazao ya miti, (mbao na nguzo za umeme) sambamba na ufugaji.
Fresh Farms ilianzisha programu maalumu, mapema mwaka jana; inayolenga kuwawezesha watanzania wengine kuwekeza katika kilimo cha miti kwa urahisi. Tayari makumi wa watanzania wamechangamkia fursa hii. Fresh Farms & Tours (T) tunapenda kuwaarifu wale wote wenye nia ya kuwekeza nasi; KWAMBA kuanzia tar 1, Feb, 2013 kutakuwa na mabadiliko ya bei na gharama za uendeshaji kwa mashamba ya miti. Mashamba tunayoyauza laki sita kwa sasa; bei mpya itakuwa milioni moja; na yale tunayouza laki nane gharama yake itakuwa milioni moja na nusu.
Bei hizi hazitawaathiri wateja wa awali na wale ambao wamekwisha wasilisha oda zao. Fresh Farms & Tours (T) tunaendelea kuboresha huduma, taarifa na usaidizi kwa wote wanaowekeza nasi. Kabla ya mwisho wa mwaka huu; tutazindua tovuti maalaumu itakayobeba taarifa za uwekezaji katika kilimo na ufugaji; pia kila anaewekeza nasi atapata nafasi ya kufungua akaunti yake katika tovuti hiyo; na akaunti hiyo itamwezesha kufuatilia mwenendo wa mashamba yake popote alipo duniani. Fresh Farms & Tours (T)-GREENING THE WORLD AND FEEDING PEOPLE. (C) Anesa Co., Ltd