December 22, 2012

PhD YA KWANZA KUANDIKWA KWA LUGHA YA KISWAHILI UDSM

Na Honorius Ngachipanda, Mbeya

Katika hali ambayo inaleta matumaini makubwa kwa wapenzi wa lugha ya Kiswahili, taarifa wkamba Dk. Metho Samweli amefanikiwa kuandika Thesis yake ya PhD ya somo la Kiswahili kwa lugha ya Kiswahili ni za kusisimua.
Kwa mujibu wa gazeti la THE HILL OBSERVER la Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Dk Method Samweli amekuwa mhitimu wa kwanza wa Chuo hicho kuandika Thesis ya PhD kwa lugha ya Kiswahili. The Hill Observer limeeeleza kuwa kwa muda mrefu sana wahitimu wote walikuwa wakiandika thesis zao lwa lugha ya kiingereza. 
Lakini Dk Method Samweli mwenye miaka 32 ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu kishiriki cha Elimu (UDSM-DUCE) ametunukiwa PhD hivi karibuni wakati wa sherehe za 42 zilizofanyika kwenye ukumbi wa MCCC (Mlimani City Conference Center).
Mkuu wa Idaya ta fasihi, Mawasiliano na Uchapishaji katika Idara ya Kiswahili ya Chuo kikuu cha Dar es salaam, Dk. Shani Omari alisema kuwa kabla ya thesis ya Dk method Samweli, hapakuwahi kutokea Thesis yoyote iliyoandikwa kwa lugha ya Kiswahili Chuoni hapo. 
Aidha, Chuo Kikuu cha Dar es salaam kinafuata nyayo za Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) ambacho tayari wapo wanafunzi kadhaa walioandika thesis zao lugha ya Kiswahili. Miongoni mwa wahitimu wa PhD waliofanikiwa kuandika Thesis zao kwa lugha ya kiswahili, ni Mohamed Seif Khatibu ambaye ni waziri mwandamizi na kiongozi wa siku nyingi ndani ya CCM.

WASIFU WA DK. METHOD SAMWELI
Alijiunga sekondari ya Ndanda, kisha akajiunga na UDSM mwaka 2002 hadi mwaka 2006 alipomaliza masomo yake ya B.A with Education na kuwa mhadhiri msaidizi wa UDSM-DUCE. Kati ya mwaka 2006 na 2008 alimaliza masters katika masomo ya Linguistic hapo hapo UDSM. 

NAFASI YA KAZI ICT TECHNICIAN; MWISHO JANUARI 14, 2013

Anahitajika ICT TECHNICIAN, mwenye uzoefu, ujuzi na uwezo wa kusimamia masuala yote ya IT katika mtandao, servers, software development, maintenance and trouble shooting, and hardware maintenance.
Kama unazo sifa hizo hapo juu basi unakaribishwa kuomba nafasi ya kazi hiyo ukiambatanisha WASIFU WAKO (CV) na kuzipeleka kwenye ofisi zetu zilizopo ghorofa ya 9 katika jengo la NSSR HIFADHI HOUSE makutano ya mitaa ya Samora Avunue/Azikiwe Street Dar es salaam. Tuma kwa njia ya P.O BOX 3209 Dar es salaam.
Tarehe ya mwisho kupokea maombi hayo ni januari 14, 2013.
WAHI SASA.

December 21, 2012

WAZIRI MKUU AAHIDI KUCHANGIA SH. 25M/- ZA JENERETA

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ameahidi kuchangia gharama za ununuzi wa jenereta kwa ajili ya kata ya Majimoto wilayani Mlele mkoani Katavi ili waweze kuwa na umeme wa uhakika.
Alitoa ahadi hiyo jana mchana (Jumatano, Desemba 19, 2012) wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Majimoto kwenye uwanja wa mpira akiwa katika siku ya saba ya ziara yake jimboni kwake Katavi wilayani Mlele, mkoani Katavi.
“Kuna wafanyabiashara wa hapa Majimoto ambao walikuja kuniona na wakasema wako tayari kuchangia ununuzi wa jenereta lenye uwezo wa kutoa kilovoti 60 za umeme kwa nyumba kama 300. Wao watoe milioni 25 wakiwa tayari na mimi nitatoa milioni 25... jaribuni mkae na kupanga namna ya kuchangia gharama.”
“Baada ya muda fulani mtakuta mmemaliza kuchangia, tuwarudishie wafanyabiashara hela yao ili hilo jenereta liwe la kijiji. Mkilipata, nitawasiliana na TANESCO ili watupatie nguzo za umeme,” alisema.
Akijibu hoja kuhusu viwanja, Waziri Mkuu ambaye ni mbunge wa jimbo la Katavi alisema upimaji wa viwanja ulifanyika miaka miwili iliyopita na vikapatikana viwanja 270 lakini hadi sasa havijagawiwa kwa wananchi. Aliwataka viongozi wa kata na wilaya wasimamie zoezi hilo.
Hata hivyo, Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwaonya juu ya ujenzi wa nyumba za makazi na biashara kando ya barabara kuu. ” Ninawasihi sana mheshimu sheria za barabara... msijenge nyumba zenu ndani ya hifadhi ya barabara.
Kesho (Ijumaa, Desemba 21, 2012) Waziri Mkuu atakwenda kata ya Usevya ambako atazindua mradi wa umemejua (solar power) kwenye sekondari ya kata ya Usevya na kuhutubia wananchi.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMISI, DESEMBA 20, 2012.

NAFASI ZA KAZI DESEMBA HII MPAKA MWEZI JANUARI MWAKA 2013

WADAU: kwa wale wanaoendelea kutafuta kazi mbalimbali kwenye amshirika na taasisi za umma yaani serikalini, kuna nafasi za kazi zimetolewa ambazo nanyi wadau mnatakiwa kuzifuatilia.
Kwahiyo hapa naweka tanagzo hili ambali lionyesha nafasi za kazi katika sekta binafsi na umma.

BONYEZA HAPA KUSOMA ZAIDI

December 20, 2012

MAKAA YA NGAKA KUIMARISHA UZALISHAJI VIWANDANI


Mitaa ya mbinga mjini.
picha kwa hisani ya Prof Joseph Mbele

Uzalishaji wa makaa ya mawe unatarajiwa kuongezeka baada ya mradi wa uchambiaji wa makaa ya mawe mjini NGAKA wilayani MBINGA katika mkoa wa Ruvuma kufanza kufanyiwa kazi na kampuni ya uchimbaji makaa hayo wilanai humo.
KWA TAARIFA ZAIDI BONYEZA HAPA KUSOMA HABARI NZIMA

SERIKALI YATENGA SH. BILIONI MOJA KUJENGA DARAJA LA KAVUU

mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi.

SERIKALI imetenga kiasi cha sh. bilioni moja kwa ajili ya kazi za awali za ujenzi wa daraja la mto Kavuu linalounganisha kata za Mamba, Kasansa, Majimoto, na kijiji cha Inyonga yalipo makao makuu ya wilaya mpya ya Mlele. 

Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda jana jioni (Jumatano, Desemba 19, 2012) wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Mamba kwenye uwanja wa mpira akiwa katika siku ya saba ya ziara yake jimboni kwake Katavi wilayani Mlele, mkoani Katavi. 
Waziri Mkuu alisema Serikali ina nia ya kufungua mawasiliano kati ya bonde la Rukwa na mikoa ya kaskazini ambako kuna uhaba wa chakula. “Bonde hili linasifika kwa uzalishaji mkubwa wa nafaka kwa hiyo kujengwa kwa daraja hilo ni ukombozi mkubwa wa kufungua soko kwa mazao mnayozalisha huku,” alisema. 
Alisema katika mwaka huu wa fedha, barabara ya kutoka Sitalike kupitia Kibaoni, Majimoto, Mamba hadi Kasansa yenye urefu wa kilomita 33.5 imetengewa sh. milioni 837/- na kwamba wakandarasi wawili wamekwishapatikana ili kuifanyia ukarabati barabara hiyo.
Kuhusu barabara ya Majimoto hadi Inyonga yenye urefu wa kilometa 135, Waziri Mkuu alisema zimetengwa sh. milioni 943/- kwa ajili ya ujenzi wa madaraja katika barabara hiyo. 
Alipoulizwa kuhusu kuwepo kwa fedha hizo, Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Katavi, Mhandisi Isaack Kamwelwe alimthibitishia Waziri Mkuu kuwepo kwa fedha hizo. 
“Fedha zimeshatengwa na leo nimepokea kibali cha kutangaza zabuni za ujenzi wa daraja hilo. Zabuni zitatangazwa kuanzia Januari 2013,” alisema. 
Kutokuwepo kwa daraja la Kavuu kunawafanya wakazi waishia bonde la Rukwa (maeneo ya Majimoto na Mamba) kila wanapotaka kwenda Inyonga, walazimike kupitia Mpanda yaliko makao makuu ya wilaya yao ambako ni zaidi ya kilometa 350. 
Kesho (Ijumaa, Desemba 21, 2012) Waziri Mkuu atakwenda kata ya Usevya ambako atazindua mradi wa umemejua kwenye sekondari ya kata ya Usevya na kuhutubia wananchi.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMISI, DESEMBA 20, 2012.