December 27, 2012

MIKONO NA MOYO WA NATHAN MPANGALA KUWAFANYA WATOTO WENYE SARATANI KUTABASAMU

Nathan Mpangala akiwa anawafundisha watoto kuchora michoro mbalimbali. 
Nathan Mpangala ni miongoni mwa watanzania wanaogusa mioyo ya watu kutokana na kazi zao za sanaa. Wengi wanakumbuka michoro ya katuni za Kijastibikozi na mingine mingi sana. 
Yeye ndiye mwasisi wa michoro ya katuni za Daladala ambazo huchapishw ana gazeti la MAJIRA hapa nchini. Tasnia ya uchoraji imemfikisha katika nchi mbalimbali kuhudhuria mihadhara ya kuelimisha jamii akiwa miongoni mwa waandishi wa habari wanaotumia vipaji vyao kufikisha ujumbe kwa njia ya sanaa za michoro. Moja ya kazi zake kubwa zinazoonekana kote nchini kupitia Televisheni ya ITV ni kibonzo cha MTU KWAO. 
Kibonzo hivyo hubeba ujumbe mbalimbali wenye nia ya kuelimisha na kuburudisha jamii. Kutokana na kipaji chake, Nathan Mpangala anarudisha faida anayopata kwa kazi hiyo kwenda kwa jamii. 
Amekuwa akifanya hivyo kupitia programu ya WAFANYE WATABASAMU akiwa na lengo la kuwaliwaza watoto wote wanaougua saratani nchini. Juhudi hizo ni kutokana na mapenzi yake kwa jamii na nchi kwa ujumla. Kama anavyoonekana pichani akiwa na watoto hao, pamoja na mchoro mwingine upande wa kulia unavyoonyesha watu wasiofikiria jamii yao. 
Hakika Mikono na moyo wa NATHAN MPANGALA umekuwa faraja kwa wazazi wa watoto na watoto hao kwa ujumla. Nawe waweza kuchangia juhudi zake kwa kuungana naye katika WAFANYE WATABASAMU.


Anaelezea zaidi safari yake .............
UCHORAJI UMEPAMBA MOTO. Baadhi ya watoto wanaendelea na matibabu ya saratani katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, jijini Dar es Salaam, wakijimwayamwaya wakati wakichora. Kupitia Program ya Wafanye Watabasamu, nilitembelea watoto hao kuwapa zawadi kisha kuchora nao. 
Katika ziara hiyo niliyoambatana na baadhi ya wachoraji katuni na marafiki wa Wafanye Watabasamu tuliwazawadia watoto zawadi kisha kuchora nao. Kwa niaba ya watoto, nawashukuru ndugu na marafiki wa Programu ya Wafanye Watabasabu kwa zawadi mbalimbali walizochangia ambazo zimefanya ziara hiyo kuwa ya mafanikio. Pia nawashukuru sana marafiki na wachoraji wote waliojitokeza na kuungana nami Muhimbili. Picha na michoro mbalimbali iliyochorwa na watoto hayo iko njiani.

December 22, 2012

PhD YA KWANZA KUANDIKWA KWA LUGHA YA KISWAHILI UDSM

Na Honorius Ngachipanda, Mbeya

Katika hali ambayo inaleta matumaini makubwa kwa wapenzi wa lugha ya Kiswahili, taarifa wkamba Dk. Metho Samweli amefanikiwa kuandika Thesis yake ya PhD ya somo la Kiswahili kwa lugha ya Kiswahili ni za kusisimua.
Kwa mujibu wa gazeti la THE HILL OBSERVER la Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Dk Method Samweli amekuwa mhitimu wa kwanza wa Chuo hicho kuandika Thesis ya PhD kwa lugha ya Kiswahili. The Hill Observer limeeeleza kuwa kwa muda mrefu sana wahitimu wote walikuwa wakiandika thesis zao lwa lugha ya kiingereza. 
Lakini Dk Method Samweli mwenye miaka 32 ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu kishiriki cha Elimu (UDSM-DUCE) ametunukiwa PhD hivi karibuni wakati wa sherehe za 42 zilizofanyika kwenye ukumbi wa MCCC (Mlimani City Conference Center).
Mkuu wa Idaya ta fasihi, Mawasiliano na Uchapishaji katika Idara ya Kiswahili ya Chuo kikuu cha Dar es salaam, Dk. Shani Omari alisema kuwa kabla ya thesis ya Dk method Samweli, hapakuwahi kutokea Thesis yoyote iliyoandikwa kwa lugha ya Kiswahili Chuoni hapo. 
Aidha, Chuo Kikuu cha Dar es salaam kinafuata nyayo za Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) ambacho tayari wapo wanafunzi kadhaa walioandika thesis zao lugha ya Kiswahili. Miongoni mwa wahitimu wa PhD waliofanikiwa kuandika Thesis zao kwa lugha ya kiswahili, ni Mohamed Seif Khatibu ambaye ni waziri mwandamizi na kiongozi wa siku nyingi ndani ya CCM.

WASIFU WA DK. METHOD SAMWELI
Alijiunga sekondari ya Ndanda, kisha akajiunga na UDSM mwaka 2002 hadi mwaka 2006 alipomaliza masomo yake ya B.A with Education na kuwa mhadhiri msaidizi wa UDSM-DUCE. Kati ya mwaka 2006 na 2008 alimaliza masters katika masomo ya Linguistic hapo hapo UDSM. 

NAFASI YA KAZI ICT TECHNICIAN; MWISHO JANUARI 14, 2013

Anahitajika ICT TECHNICIAN, mwenye uzoefu, ujuzi na uwezo wa kusimamia masuala yote ya IT katika mtandao, servers, software development, maintenance and trouble shooting, and hardware maintenance.
Kama unazo sifa hizo hapo juu basi unakaribishwa kuomba nafasi ya kazi hiyo ukiambatanisha WASIFU WAKO (CV) na kuzipeleka kwenye ofisi zetu zilizopo ghorofa ya 9 katika jengo la NSSR HIFADHI HOUSE makutano ya mitaa ya Samora Avunue/Azikiwe Street Dar es salaam. Tuma kwa njia ya P.O BOX 3209 Dar es salaam.
Tarehe ya mwisho kupokea maombi hayo ni januari 14, 2013.
WAHI SASA.