April 22, 2013

INTERNATIONAL AFRICAN FESTIVAL TUBINGEN, GERMANY 2013


Welcome  to !

International African Festival Tübingen, Germany 2013

Be part of 100.000 visitors at the largest Extravanganza !

 
Madam Enie Muyang Tatah
 African Pilgrimage to Tübingen, Germany 2013 – outdoor & Entry Free

International African Festival Tübingen proudly announces its 2013 season today, bringing together world class African lifestyle, music, food, exciting newcomers to the international stage from 8- 11 august 2013 – African Village (Festplatz) Open-air –Down town Tübingen, Germany
It is the fastest and largest growing Diaspora cultural event transforming the city of Tübingen in south of Germany into a pilgrim city, bringing African Diaspora worldwide irrespective of country of origin, gender and religious background , friends and well wishers of Africa together
More than 100.000 visitors are expected to attend International African Festival Tübingen 2013
This event promises a multi-dimensional exploration of interplay of authentic African culture and lifestyle -150 artists –live- featuring fresh sounds and voices –Ngoma Africa Band, Soweto Entsha, Wamali percussions, street arts, workshops and culinary expression.
The Festival once again invites artist and audiences of all ages to experience African music, arts, culture and party, a mélange between traditional and modern Africa, bringing African hip-hop, Bongo Dansi,Kwaito,Afro-Pop,soukouss and African movies on the international stage
Festival highlights will include- a grandiose opening ceremony lead by African children & youths, celebrities, African ambassadors rep. in Germany under the chairman ship of the Ghana Ambassador, program for families, panel discussion and late night events - the biggest African party in Germany, Stuttgart on Saturday night –form 22 o’clock featuring celebrities and Sunday will be special day for family – special church and Gospel day and closing ceremony
Visual art is at the focus on our Festival and this year the African royal ballet is visiting all the way from Mali featuring Djiby & Basy Kouyate, dance styles and moves to support and build schools in Mali,   Christoffel-Blindemission project helping the blind to see in Africa, bongob trust and many more.
Stay updated on www.afrikafestival.net, follow and like us on facebook

For more details you may  please contact:

Madam Enie Muyang Tatah,CEO and Founder / Call +49-15210610374 /Email: kontakt@afrikafestival.net

UVUMILIVU WA KISIASA BUNGENI


Edgar Mwandemani, Dar es salaam
Na Edgar Mwandemani, Dar es salaam

Inaelezwa kuwa matokeo ya haya yanayoendelea hivi sasa katika siasa za Tanzania (kuzomeana, matusi na kukashfiana) ni, pamoja na mambo mengine, ukosefu wa uvumilivu wa kisiasa. Sitaki kusema tafsiri hii ni kweli ama si kweli. Pamoja na kwamba neno hili 'Uvumilivu wa Kisiasa' ni zuri linapotamkwa na wakati mwingine humwenyesha aliyelitamka ni mstaarabu, mwenye busara na asiyependa makuu.

Katika muktadha wa siasa za Kiafrika, Tanzania kwa upekee, utamaduni huu umetumika kama silaha ya kuadhibiana miongoni mwa makundi hasimu katika siasa. Kwa upande wa chama tawala kimekuwa kikiwashutumu mahasimu wake kwamba ni kutokana na uchanga wao katika siasa ndio maana wanafanya hayo wayafanyayo. Imefika hatua katika siasa za kibunge, spika wa bunge la Tanzania amewahi kusema vurumai zilizotokea mwaka jana bungeni ni matokeo ya utoto wa wabunge wa upinzani.

Kwa upande mwingine wale wa upinzani wameendelea kujitetea kwamba wanayafanya wayafanyayo katika kutekeleza ile haki ya kimsingi ya kikatiba ya 'uhuru wa maoni' na 'kusimamia maslahi ya umma'. Na kwamba juhudi zozote za kuwanyamazisha ni kuminya uhuru huo. Ili mradi kila upande unajitetea kwa namna yake!

Profesa S.S Mushi anatafsiri dhana hii kuwa ni "...harmonization of diversity or the extent to which public authorities accommodate divergent views in political governmental processes". Kwa ujumla wake ni kuvumila mawazo ya tofauti bila kujali nani ameyatoa. Lakini kuvimila mawazo/maoni tofauti si sawa na kumilia lugha chavu/matusi mbele ya jamii; kwa hivyo kwa muktadha wa yanayotokea hivi sasa hapa nyumbani, waheshimiwa hawa kwa maoni yangu hawatofautiani maoni/hoja bali tafsiri ya maneno machafu/matusi.

Aidha, Mushi anaendelea kueleza kuwa dhana hii 'uvumilivu wa kisiasa' chanzo chake ni mambo makuu mawili. Moja, ni kiwango cha mgawanyiko kilicho katika jamii yenyewe. Mgawanyiko wa makundi mfano, makabila, dini, rangi na kitaasisi unamchango mkubwa kujua kiwango cha 'uvumilivu wa kisiasa'. Jambo la pili ni, Tabia na sera za asasi za umma; kwamba ziko zile zinazowaleta pamoja raia na zingine huwagawa.

Tulipofikia jamii ya watazania imezama katika dimbwi la mgawanyiko. Hivi sasa mgawanyiko wa kidini, kimakabila, kimaeneo, makundi rika, jinsia na itikadi za vyama umeendelea kuliguguna taifa letu kiasi cha kusababisha mafarakano, magomvi na vifo katika maeneo fulani. Watu wamevaa tofauti zao kama silaha dhidi ya wenzao, hakuna tena umoja wa kitaifa. Bahati mbaya ni kuwa mambo haya yamechochewa na fikra za kipumbavu miongoni mwa makundi hayo; fikra za kujiona kila mmoja ni bora dhidi ya mwingine. Vyama siasa kwa mfano, vimedhani kwa muda mrefu, rangi zao za bendera ndio utanzania: kila chama kinataka kupuuza uwepo wa kingine!

Taasisi nazo si haba. Nyingi zake zimeendelea kuendeshwa kwa tabia na sera zinazochochea migawanyiko katika jamii. Tukichukua mfano wa Bunge letu hivi sasa; mijadala mingi inayoendeshwa humo imekuwa ikijikita katika kuonyeshana ubabe na ununda wa vyama vya siasa. Kwa upande wa chama tawala wamekuwa hawaheshimu wala kuzingatia maoni ya wale wengine kwa kisingizio cha wingi dhidi ya uchache. Upinzani nao kwakisingizio cha 'kusimamia mabadiliko' na 'uhuru wa maoni' wamekuwa wakijiona wao ndio kila kitu na kwa kuwa wamekuwa wakipuuzwa basi ni vitimbi.

Bunge limebaki kuwa mahali pa vihoja badala ya hoja; na kwa mwenye kihoja kikubwa ndio wa maana kuliko mwenzake. Katika mazingira haya itakuwa si kweli kudai kuwa siasa za Tanzania zimekosa 'uvumilivu wa kisiasa' kwani kilichopo hivi sasa ni vihoja uvumilivu utatoka wapi? Hakuna wa kuvumilia vihoja!

Kama kweli tunataka kuwepo na 'uvumilivu wa kisiasa' lazima tujitafakari juu utamaduni wa siasa zetu. Siasa ni matokeo ya utamaduni wa maisha ya kila siku katika jamii. Tusipoujenga tutarajie vurumai zaidi katika maeneo mbalimbali!

MBUNGE WA JIMBO LA MBINGA MAGHARIBI, JOHN KOMBA ALIPOKUTANA NA WADAU WA WILAYA YA NYASA.

Na Mwandishi Wetu, Dar

Mbunge wa Jimbo la Mbinga Magharibi ambako sasa imeanzishwa wilaya mpya, alifanya mkutano na wadau wa wilaya Nyasa hapa jijini dar es salaam. John Komba akiwa na ameambatana na mkuu wa wilaya ya Nyasa na mkurugenzi wa halmashauri hiyo walizungumza na wadau wa wilaya Nyasa walioko jijini Dar es salaam kwa kunia ya kuchochea maendeleo zaidi katika wilaya hiyo. 

Mbunge John Komba akihutubia wadau wa Nyasa, jijini Dar.
Moja ya changamoto kubwa zilizojitokeza ni hali ya matokeo mabaya ya kidato cha nne ambako wilaya Nyasa ilikishika mkia kati ya wilaya zote za mkoa wa Ruvuma. Kwa Mujibu wa mkurugenzi wa wilaya hiyo alisema kunahitajika mchango wa haraka kutoka kwa wadau wa wilaya ya Nyasa ili waweze kufanikisha upatikanaji wa maendeleo. 
Hata hivyo mbunge John Komba aliwaomba wadau hao kuwa ni lazima washiriki kuchochea maendeleo ya wilaya Nyasa tofauti na ilivyo sasa ambako mchango wao ni finyu. Aidha, alihimiza kuwekeza kwa dhati kwa elimu ya watoto wa kike ambapo alisema kwa wilaya ya Nyasa kiwango cha watoto wa kike kusomeshwa ni cha chini sana hivyo aliwaomba wadau kufanya juhudi kubwa kufanikisha ajenda za wilaya zinafanyiwa kazi ipasavyo. 

wadau wa nyasa
Kwa upande wa wadau hao walidai kuwa ni vyema mkuu wa wilaya na mkurugenzi wa wilaya hiyo wakahakikisha upatikanaji wa vyuo vya ufundi ambavyo vitasaidia vijana wengi wa wilaya hiyo ambao hutegemea kilimo na uvuvi. Pia walisema ni vyema halmashauri ya wilaya ikashirikiana na asasi za dini au AZAKI kufanikisha mpango wa kuanzisha chuo cha uvuvi kama ilivyokuwa Chuo cha Mbegani, kilichokuwa mjini Liuli na kuendeshwa na kanisa la Anglikana. 
Wadau hao walisema halmashauri ya wilaya ihakikishe kunakuwepo vyuo vya mafunzo ya ufundi kwa kushirikiana na VETA ambayo itawakomboa vijana wengi ambao hushindwa kumudu maisha hasa wanapomaliza shule za msingi. mbunge kOmba alisisitiza kuwa ofisi ya mbunge imefanya uchunguzi na kubaini watoto wa kike wengi huishia darasa la saba na baada ya hapo hawasomeshwi, kwahiyo aliwataka wadau kusaidia kuondokana na tatizo hilo ili kuleta uasawa kijamii. 

Nilikuwa miongoni mwao.
Pamoja na mambo mengine makubaliano ya wadau na viongozi wao ilikuwa ni kuboresha elimu, kuvumbua njia mbadala za kuwawezesha wakazi wa wilaya ya Nyasa kuishi katika maisha yenye uhakika kwa kuzingatia elimu ya ufundi. Pia suala la afya lilizingatiwa pia hasa kuboresha hopsitali/zahanati zote za wilaya Nyasa ili kuhakikisha wananchi wanakuwa kwenye hali nzuri. 
Aidha jambo kubwa zaidi ni namna wajawazito wanavyocheleweshwa kufikishwa hospitali kutokana na matatizo mbalimbali. Hata hivyo wadau hao walipongeza juhudi za miradi mbalimbali ikiwemo Maji na ujenzi wa barabara, ambapo kwa sasa upo kwenye upembuzi yakinifu kati ya Mbamba Bay hadi Lituhi, baada ya ujenzi wa barabara ya Songea hadi Mbamba Bay kuendelea kujengwa.
Kutokana na hali hiyo wadau walimhimiza mkuu wa wilaya, mkurugenzi na mbunge kuhakikisha wananchi wa wilaya Nyasa wananufaika na rasilimali zao zote wilayani humo. Moja ya changamoto kubwa iliyojitokeza ni namna gani serikali itafanya juhudi kuendeleza miradi ya ujenzi wa viwanda mfano Sukari, na vingine. Pia upatikanaji wa soko la uhakika kwa wakulima ambao watakuwa wanauza mazao yao hasa mpunga,mahindi na kadhalika.
wadau
Mbunge, Komba pia alifanya jambo zuri kumwalika aliyekuwa mpinzani wake Alex Shauri ambaye alimhimiza mbunge huyo kuhakikisha kabla ya mwaka 2015 angalau kuwepo na utaratibu wa upatikanaji wa nishati ya umeme. Alex Shauri alisema wananchi wa Nyasa wanahitaji mambo makuu mawili elimu na afya. Akaongeza kuwa kama hayo yatafanyika basi hakuna shaka yoyote kuwa maendeleo ya wilaya yatapatikana watu wakiwa na afya njema, hivyo upatikanaji wa madawa na matibabu yenye uhakika ni muhimu zaidi.

wadau
Kwa upande mwingine wadau walikubaliana na mbunge kuwa changamoto ya mchango wao kuwa finyu itafanyiwa mabadiliko, ambapo hapohapo kulianzishwa harambee ya kuchangia maendeleo ya wilaya hiyo. 
MUHIMU; picha za wadau wa Nyasa waliohudhuria mkutano huo katika ukumbi wa Msimbazi Center wa kanisa katoliki jijini dar es salaam.

sehemu ya waliohudhuria.

wadau

wadau wa nyasa.

wadau wakiwa makini

wadau wa nyasa

muziki mnene huo

wadau wa Nyasa

walikosa viti lakini walisikiliza hotuba.

wadau pia

wadau wakisiliza hotuba.

kona ambayo waliketi wazee.

vijana hawakubaki nyuma

wadau wa Nyasa wametulia na kusikiliza

wadau wakisiliza

Mwenye nguo rangi ya orange katikati ni FARAJA KISHINDO, dada na rafiki yangu mkubwa tangu nikiwa sekondari. Hapo ilipita miaka 13 ndio tulionana kwenye mkutano huo.

wauliza maswali wamepanga mstari

foleni ya kuuliza maswali kwa viongozi.

Akina mama kama walisimama imara kuhimiza maendeleo ya wilaya

wadau wakibadilishana mawazo juu ya mada zilizowasilishwa

Mzee huyu alisifika kwa maswali yake kuhusu elimu na afya.

NAFASI YA KAZI AFISA MAENDELEO DARAJA II


COMMUNITY DEVELOPMENT OFFICER GRADE II) – NAFASI 22
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Waajiri wafuatao:- Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, Mtwara, Sumbawanga, Simanjiro, Halmashauri ya Mji Njombe, Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba, Newala, Nkasi, Bukoba, Sengerema, Rufiji, na Mpanda na Halmashauri ya Jiji la Mwanza.
71.1 MAJUKUMU YA KAZI
Maafisa Maendeleo ya Jamii Dalaja la II watapangiwa kazi katika ngazi za Kata au Makao Makuu ya Halmashauri na kazi zao zitakuwa zifuatazo:
· Kuandaa na kupendekeza mipango na mikakakti ya kubadili fikra za watu ili waweze kuwa na mawazo ya maendeleo sawia na Sera za Serikali na wakati uliopo
· Kupitia mbinu shirikishi kuwezesha jamii kuanzisha miradi ya kijamii kama vile:-
- Usafi wa mazingira
- Ujenzi wa nyumba bora
- Ujenzi wa shule
- Ujenzi wa zahanati
- Kuchimba au kuzifanyia matengenezo barabara hasa za vijijini
- Ujenzi wa majosho
- Uchimbaji wa visima vifupi
44
- Utengenezaji wa malambo
· Kuhamasisha matumizi endelevu ya mazingira
· Kusambaza na kuhamsisha matumizi ya teknolojia sahihi kama vile uvunaji wa maji ya mvua, majiko sanifu, matumizi ya mikokoteni
· Kuhamasisha watu kutumia huduma za mafunzo ya Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi
· Kuwasadia wanachi vivijini kuandaa maandiko (Project Write ups) ya kuombea fedha za kuendesha miradi yao
· Kuhamasisha, kuandaa na kutoa elimu kwa umma kuhusu uraia na Utawala bora
· Kukusanya, kutunza, kutafsiri na kusambaza takwimu na kumbukumbu muhimu kwa ajili ya matumizi ya jamii
· Kuwezesha wananchi kupambana na mila zenye madhara kwa afya za wanchi hasa wanawake na watoto wa kike, kuenea kwa virus vya UKIMWI na magonjwa ya mlipuko.
· Kuelimisha viongozi wa Serikali za Vijiji, Dini na Mashirika yasiyo ya Kiserikali kuhusu Sera mbalimbali za Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto na kutumia Sera hizo
· Kutoa taarifa za hali ya jamii kwa ngazi mbalimbali
71.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wahitimu wa Shahada au Stashahada ya Juu ya Maendeleo ya Jamii kutoka Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali katika fani zifuatazo:-
 Maendeleo ya Jamii (Community Development)
 Elimu ya Jamii (Sociology)
 Masomo ya Maendeleo (Development Studies)
 Mipango na Usimamizi wa Miradi (Project Planning and Management)
 Maendeleo na Jinsia (Gender and Development)
71.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.
72.0 MLEZI WA WATOTO MSAIDIZI (CHILD CARE ASSISTANT) – NAFASI 5
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Manispaa ya Singida na Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga.
72.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kulea watoto katika vituo vya kulelea Watoto wadogo mchana
· Kutoa mafunzo kwa akina mama juu ya malezi bora ya watoto wadogo wenye umri kati ya miaka 0 hadi 8
· Kusaidia shughuli za kinga za magonjwa ya watoto vijijini/sehemu au eneo la kituo
· Kuwa kiongozi wa kituo cha malezi ya awali ya Watoto wadogo
45
72.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajriwa wahitimu wa kidato cha nne waliofaulu mafunzo ya mwaka mmoja ya malezi ya awali ya watoto wadogo wenye umri kati ya miaka 0 hadi 8 kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali au wenye cheti cha mwaka mmoja cha mafunzo ya Ustawi wa Jamii.
72.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B kwa mwezi.
62.0 MAENDELEO YA JAMII MSAIDIZI II (COMMUNITY DEVELOPMENT ASSISTANT GRADE II) – NAFASI 52
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Manispaa ya Mtwara na Kigoma/Ujiji. Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, Babati, Pangani, Mkinga, Sengerema, Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Halmashauri ya Mji Njombe, Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji, Kibondo na Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
62.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kuwa kiungo kati ya wanakijiji, Afisa Mtendaji wa kata na watumishi wengine wa Serikali katika kutekeleza shughuli za maendeleo
· Kuhamasisha wanakijiji katika kazi za kujitegemea
· Kubainisha na kuratibu matumizi ya rasilimali kwa miradi ya kijiji
· Kukusanya, kutunza, kutafsiri na kusaidia wanakijiji kutumia takwimu na kumbukumbu mbalimbali kwa shughuli za maendeleo ya kijiji
· Kutoa taarifa za utekelezaji wa shughuli za maendeleo kila mwezi kwa uongozi wa kijiji na kwa Afisa Maendeleo ya Jamii ngazi ya Kata
· Kuwahamisha na kuwawezesha wananchi kulinda na kuhifadhi vyanzo vya maji
37
· Kusaidia kuunda vikundi vya kijamii na kimaendeleo
· Kuratibu shughli za Asasi zisizo za kiserikali na kijamii
· Kuandaa tararifa za utekelezaji kazi vijinjini za kila mwezi, robo, nusu na mwaka mzima
· Kuratibu shughuli za kupambana na UKIMWI
62.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV/VI wenye Stashahada ya Maendeleo ya Jamii kutoka katika Vyuo vya Maendeleo ya Jamii (Buhare au Rungemba) au Vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali.
62.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.C kwa mwezi
63.0 AFISA MTENDAJI WA KATA DARAJA LA II (WARD EXECUTIVE OFFICER GRADE II) – NAFASI 106
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma, Morogoro, Mtwara, Halmashauri ya Wilaya ya Babati, Bunda, Mafia, Biharamulo, Newala, Kondoa, Masasi, Mtwara na Halmashauri ya Jiji la Mwanza.
63.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Atakuwa Mtendaji Mkuu wa Kata na kiungo cha Uongozi kwa Idara zote katika kata na atashughulikia masuala yote ya kata
· Atakuwa Mhamasishaji mkuu wa Umma katika mikakati mbalimbal.i ya uzalishaji, mali, kuondoa njaa na Umasikini.
· Atakuwa ni Katibu wa kamati ya maendeleo ya kata.
· Ataratibu na kusimamia upangaji wa shughuli za maendeleo ya kata, vijiji na Mtaa.
· Atatafsiri sera na kusimamia utekelezaji wa sheria ndogondogo katika Kata yake.Atamsaidia Mkurugenzi Kuratibu na kusimamia shughuli za Uchaguzi katika Kata.
· Kumsaidia na kumwakilisha Mkurugenzi katika kusimamia maendeleo ya eneo lake.
· Kusimamia utendaji kazi wa wataalamu na watendaji wengine katikangazi ya Kata.
· Kuratibu na kuandaa taarifa za utekelezaji na kuziwasilisha kwa mkurugenzi na nakala kwa Katibu Tarafa.
· Atakuwa mwenyekiti katika vikao vinavyowahusisha wataalamu na watendaji wa vjiji, na NGO’S katika kata yake.
· Atakuwa Msimamizi na mratibu wa takwimu zote zinazokusanywa katika vijiji, vitongoji, na kata yake.
38
63.2 SIFA ZA MWOMBAJI.
· Kuajiriwa wenye Shahada ya Sanaa yenye mwelekeo wa Sayansi ya Jamii (Social Sciences) Utawala, (Public Administration and Local Gorvernment), Sheria au Sifa nyingine inayolingana na hizo kutoka Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
63.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS D. kwa mwezi.
64.0 AFISA MTENDAJI WA KATA DARAJA LA III (WARD EXECUTIVE OFFICER GRADE III) – NAFASI 91
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Halmashauri ya Manispaa ya Singida, Kigoma/Ujiji na Songea, Halmshauri ya Wilaya ya Chato, Songea, Handeni, Kibondo, Mkinga, Tunduru, Mbeya, Mkuranga, Kibaha, Kwimba, Njombe, Rufiji, Bukoba, Mwanga, Sengerema na Mpanda
64.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Atakuwa Mtendaji Mkuu wa Kata na kiungo cha Uongozi kwa Idara zote katika kata na atashughulikia masuala yote ya kata
· Atakuwa Mhamasishaji mkuu wa Umma katika mikakati mbalimbali ya uzalishaji, mali, kuondoa njaa na Umasikini.
· Atakuwa ni Katibu wa kamati ya maendeleo ya kata.
· Ataratibu na kusimamia upangaji wa shughuli za maendeleo ya kata, vijiji na vitongoji.
· Atatafsiri sera na kusimamia utekelezaji wa sheria ndogondogo katika Kata yake.Atamsaidia Mkurugenzi Kuratibuna kusimamia shughuli za Uchaguzi katika Kata.
· Kumsaidia na kumwakilisha Mkurugenzi katika kusimamia maendeleo ya eneo lake.
· Kusimamia utendaji kazi wa wataalamu na watendaji wengine katika ngazi ya Kata.
· Kuratibu na kuandaa taarifa za utekelezaji na kuziwasilisha kwa mkurugenzi na nakala kwa Katibu Tarafa.
· Atakuwa mwenyekiti katika vikao vya vinavyowahusisha wataalamu na watendaji wa vjiji, na NGO’S katika kata yake.
· Atakuwa Msimamizi na mratibu wa takwimu zote zinazokusanywa katika vijiji, vitongoji, na kata yake.
64.2 SIFA ZA MWOMBAJI.
· Kuajiriwa waliohitimu kidato cha nne au sita na kuhudhuria mafunzo ya Stashahada yenye mwelekeo wa Sayansi ya Jamii (Social Sciences) Utawala, (Public Administration and Local Gorvernment), Stashahada ya Sheria au Sifa nyingine inayolingana na hizo kutoka Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
64.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya Mshahara TGS C kwa mwezi. 39
65.0 AFISA MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA II (VILLAGE EXECUTIVE OFFICER GRADE II) – NAFASI 57
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Waajiri wafuatao:- Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, Kondoa, Tandahimba,Wilaya ya Mbeya, Babati, Mkuranga, Simanjiro, Newala na Ruangwa
65.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Atakuwa Mtendaji na Mshauri Mkuu wa Serikali ya Kijiji na Kamati zake katika Mipango ya Maendeleo ya kijamii na Utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo.
· Atakuwa Afisa Mhasibu wa Serikali ya Kijiji na atasimamia mapato na matumizi ya Serikali ya kijiji
· Atakuwa Mlinzi wa Amani na Msimamizi wa Utawala Bora katika Kijiji.
· Ataratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo ya kijiji
· Atakuwa Katibu wa Kamati ya Halmashauri ya Kijiji.
· Atatafsiri Sera, ataratibu na kusimamia utekelezaji wa Sheria ndogondogo za Halmashauri ya Kijiji.
· Ataratibu na kuandaa taarifa ya utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuziwasilisha kwenye Halimashauri ya Kijiji na baadae kwenye kata .
· Ataongoza vikao vya maendeleo ya Kijiji vitavyowahusisha wananchi na wataalamu waliopo kwenye eneo lake.
· Atahamasisha wananchi katika kampeni za kuondoa njaa, umasikini, na kuongeza uzalishaji mali.
· Atasimamia matumizi bora ya Nguvu kazi.
· Atakuwa Kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya Kitaalamu Katika Kijiji.
· Atasimamia ukusanyaji wa kumbukumbu za walipa kodi, wataalamu mbalimbali na NGO waliopo katika kijiji.
65.2 SIFA ZA MWOMBAJI.
· Kuajiriwa wenye elimu ya kidato cha IV na VI waliohitimu Stashahada ya kawaida katika fani yoyote yenye mwelekeo wa Sayansi ya Jamii (Social Sciences) Utawala, (Public Administration and Local Gorvernment), Stashahada ya Sheria au Sifa nyingine inayolingana na hizo kutoka Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
65.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya Mshahara TGS C kwa mwezi.
66.0 AFISA MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III (VILLAGE EXECUTIVE OFFICER GRADE III) – NAFASI 207
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Waajiri wafuatao:- Halmashauri ya Manispaa ya Singida, Halmashauri ya Mji Njombe, Halmashauri ya Wilaya ya Chato, Handeni, Mkinga, Sengerema, Tunduru, Babati, Masasi, Mtwara, Mwanga, Kwimba, Rufiji, Ngara, Tarime na Mpanda 40
66.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Atakuwa Mtendaji na Mshauri Mkuu wa Serikali ya Kijiji na Kamati zake katika Mipango ya Maendeleo ya kijamii na Utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo.
· Atakuwa Afisa Mhasibu wa Serikali ya Kijiji na atasimamia mapato na matumizi ya Serikali ya kijiji
· Atakuwa Mlinzi wa Amani na Msimamizi wa Utawala Bora katika Kijiji.
· Ataratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo ya kijiji
· Atakuwa Katibu wa Kamati ya Halmashauri ya Kijiji.
· Atatafsiri Sera, ataratibu na kusimamia utekelezaji wa Sheria ndogondogo za Halmashauri ya Kijiji.
· Ataratibu na kuandaa taarifa ya utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuziwasilisha kwenye Halimashauri ya Kijiji na baadae kwenye kata.
· Ataongoza vikao vya maendeleo ya Kijiji vitavyowahusisha wananchi na wataalamu waliopo kwenye eneo lake.
· Atahamasisha wananchi katika kampeni za kuondoa njaa, umasikini, na kuongeza uzalishaji mali.
· Atasimamia matumizi bora ya Nguvu kazi.
· Atakuwa Kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya Kitaalamu Katika Kijiji.
· Atasimamia ukusanyaji wa kumbukumbu za walipa kodi, wataalamu mbalimbali na NGO waliopo katika kijiji.
66.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Elimu ya Kidato cha Nne au cha sita waliohitimu Astashahada (Certificate) katika Fani yoyote yenye mwelekeo wa Sayansi ya Jamii (Social Sciences) Utawala, (Public Administration and Local Gorvernment), Astashahada ya Sheria au Sifa nyingine inayolingana na hizo kutoka Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
66.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS B kwa mwezi.
67.0 AFISA MTENDAJI MTAA II (MTAA EXECUTIVE OFFICER GRADE II) – NAFASI 36
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, Halmashauri ya Manispaa ya Songea na Sumbawanga
67.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kutoa ushauri katika utekelezaji wa sheria za Serikali za Mitaa.
· Kutoa ushauri juu ya uanzishaji na uendeshaji wa mamlaka mpya za Serikali za Mitaa.
· Kutoa ushauri juu ya makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali za Mitaa.
· Kusimamia na kushauri juu ya matumizi bora ya fedha za Serikali.
· Kutayarisha taarifa za robo mwaka na mwaka zinazohusu mwenendo wa Serikali za Mitaa.
41
· Kufanya kazi nyingine zitakazoagizwa na Watendaji, Wasimamizi wa masuala ya Serikali za Mitaa.
67.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa waliohitimu kidato cha nne au sita na kuhudhuria mafunzo ya Stashahada ya yenye mwelekeo wa Sayansi ya Jamii (Social Sciences) Utawala, (Public Administration and Local Gorvernment), Stashahada ya Sheria au Sifa nyingine inayolingana na hizo kutoka Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
67.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya Mshahara TGS.C kwa mwezi.
68.0 AFISA MTENDAJI MTAA DARAJA LA III (MTAA EXECUTIVE OFFICER GRADE III) – NAFASI 46
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma, Morogoro, Mtwara, Kigoma/Ujiji na Singida na Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji.
68.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Atakuwa Mtendaji na Mshauri Mkuu wa Serikali ya Mtaa na Kamati zake katika Mipango ya Maendeleo ya kijamii na Utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo.
· Atakuwa Afisa Mhasibu wa Serikali ya Mtaa na atasimamia mapato na matumizi ya Serikali ya Mtaa
· Atakuwa Mlinzi wa Amani na Msimamizi wa Utawala Bora katika Mtaa
· Ataratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo ya Mtaa
· Atakuwa Katibu wa Kamati ya Halmashauri ya Mtaa.
· Atatafsiri Sera, ataratibu na kusimamia utekelezaji wa Sheria ndogondogo za Halmashauri ya Mtaa
· Ataratibu na kuandaa taarifa ya utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuziwasilisha kwenye Halimashauri ya Mtaa na baadae kwenye Kata.
· Ataongoza vikao vya maendeleo ya Mtaa vitavyowahusisha wananchi na wataalamu waliopo kwenye eneo lake.
· Atahamasisha wananchi katika kampeni za kuondoa njaa, umasikini, na kuongeza uzalishaji mali.
· Atasimamia matumizi bora ya Nguvu kazi.
· Atakuwa Kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya Kitaalamu Katika Mtaa.
· Atasimamia ukusanyaji wa kumbukumbu za walipa kodi, wataalamu mbalimbali na NGO waliopo katika Mtaa.
68.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wenye Elimu ya Kidato cha Nne au cha sita waliohitimu Astashahada (Diploma) katika Fani yoyote yenye mwelekeo wa Sayansi ya Jamii (Social Sciences) Utawala, (Public Administration and Local Gorvernment), Atashahada ya Sheria au
42
Sifa nyingine inayolingana na hizo kutoka Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
68.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya Mshahara TGS B kwa mwezi.
69.0 AFISA USTAWI WA JAMII DARAJA LA II (SOCIAL WELFARE OFFICER GRADE II) – NAFASI 25
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Waajiri wafuatao: – Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Katibu Tawala Mkoa wa Pwani, Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, Singida, Sumbawanga, Halmashauri ya Wilaya ya Babati, Handeni, Mkinga, Newala, Tandahimba, Bahi na Chamwino na Halmashauri ya Jiji la Mwanza
69.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kuendesha Usaili wa wahudumia (watu wenye ulemavu, wazee, familia zenye matatizo, watoto na vijana wenye matatizo mbalimbali).
· Kufanya ukaguzi wa mazingira wanayoishi wahudumiwa ili kupata taarifa zao kamili
· Kuandaa taarifa za usaili na ukaguzi wa mazingira ya wahudumiwa.
· Kupokea na kukusanya taarifa za Ustawi wa Jamii kutoka kwa wadau na vituo mbalimbali vya Ustawi wa Jamii.
· Kupokea na kukusanya takwimu zinazohusu huduma za watu wenye ulemavu, wazee, malezi ya watoto na familia zenye matatizo.
· Kupokea, kuchambua na kuandaa orodha ya maombi ya uandikishaji vituo vya kulelea watoto wadogo mchana, malezi ya kambo (foster care) na vituo vya walezi wa watoto wadogo mchana.
· Kupokea, kuchambua na kuandaa orodha ya maombi ya msaada wa Rais kutoka kwa akina mama, walojifungua watoto watatu au zaidi kwa mara moja.
· Kupokea, kuchambua na kuandaa orodha ya maombi ya watoto yatima au wanaohitaji misaada mbalimbali
· Kupokea, kuchambua na kuandaa orodha ya maombi mbalimbali toka kwenye familia za watu wenye dhiki
· Kuhoji na kuandaa taarifa za washitakiwa.
· Kusimamia wahudumiwa katika makazi, vyuo vya mafunzo ya Ufundi Stadi vya watu wenye ulemavu, Mahabusu za watoto na shule za maadilisho.
· Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake.
69.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wenye Shahada ya BA (Social Works or Sociology) au Stashahada ya juu ya Ustawi wa Jamii (Advanced Diploma in Social Works) kutoka Chuo cha elimu ya juu kinachotambuliwa na Serikali
43
69.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.
70.0 MSAIDIZI USTAWI WA JAMII DARAJA LA II (SOCIAL WELFARE ASSISTANT GRADE II) – NAFASI 6
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga, Ruangwa
70.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kutambua na kuhudumia watu walio katika makundi maalum na mazingira hatarishi.
· Kukusnya takwimu zinazohusu watu walio katika makundi maalum na mazingira hatarishi.
· Kuchambua na kuandaa orodha ya maombi mbalimbali kutoka kwenye familia na watu wenye dhiki.
· Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake.
70.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne au sita wenye cheti cha mafunzo ya mwaka mmoja ya Ustawi wa Jamii kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali
70.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS C kwa mwezi.
NB: MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania.
ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iv. Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe katika kichwa cha habari cha barua na juu ya bahasha, kutozingatiwa hili kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.
v. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.

vi. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwawale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka kupotea.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Computer Certificate
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
- Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.
vii. “Transcripts”, “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
viii. Waombaji wawe na umri usiozidi miaka 45.
ix. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
x. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
xi. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xii. WAAJIRI WOTE WALIOPO NJE YA DAR ES SALAAM WANAOMBWA KUSAMBAZA MATANGAZO HAYA KWENYE MBAO ZA MATANGAZO NA MAENEO MENGINE.
xiii. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 8 Juni, 2013
xiv. Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajira HAURUHUSIWI.
xv. Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza na yatumwe kupitia posta kwa anuani ifuatayo.
Secretary,
Public Service Recruitment
Secretariat,
P.O.Box 63100
Dar es Salaam.

AU

Katibu,
Sekretariati ya Ajira katika
Utumishi wa Umma,
SLP.63100, 

April 20, 2013

MAFURIKO YALIYOTOKEA WILAYA YA NYASA



Na Hoops Kamanga, Mbamba Bay

Mnamo tarehe 14 mwezi huu, kulitokea maafa makubwa yaliyosababishwa na mvua iliyonyesha katika maeneo mbambali wilayani Nyasa katika mkoa wa Ruvuma. Kama tunavyojua kuwa wilaya hiyo inasehemu kubwa ya ukanda wa ziwa nyasa, hivyo wahanga wa mafuriko hayo ni wakazi wa ukanda wa nyasa. 

Kama tulivyosema mwanzoni kwamba haya ni maafa makubwa na ahaykuwahi kutokea katika kipindi chochote kwani yameacha hasara kubwa kwa jamii za wanyasa. Kwa kipindi cha miaka ya nyuma kuliwahi kutokea maafa hayo yaliyosababishwa na kimbunga lakini hakukuwa na hasara kubwa kama hii. 

Kulingana na rekodi ambazo zinapatikana wilayani hapa, mpaka sasa maafa hayo ya mafuriko usiku wa kuamkia tarehe 14/04/2013, kuna hasara mbalimbali kama ifuavyo;
1. Mtu mmoja  amefariki dunia katika kijiji cha Ndengere, nje kidogo ya mji Mbamba Bay
2. Ng’ombe 7 wamesombwa na maji huku ikipatikana zaidi ya mizoga 6.
3. Mamba wamesombwa watatu wamesombwa kutoka mtoni kwenye mashamba ya mpunga karibu na makazi ya watu. 
4. Jumla ya hekari 87 za mpunga zimeharibika kabisa na mafuriko hayo katika vijiji vya Mbamba bay, Kilosa na Ndesule.