"Sitaki kulieleza zaidi jambo hili. Lakini hivyo ndivyo
ilivyokuwa. Vitu vingi sana vimepanda bei; na kila mtu kaumia; wenye kipato
kidogo waliumia zaidi kuliko wenye kipato kikubwa. Tumetangaza bei zaidi kwa
mazao ya wakulima na tumepandisha mishahara ya wafanyakazi wote. Najua sasa
hivi kuna kushangilia kwingi kila mahali. Wakulima wanashangilia na wafanyakazi
mnashangilia. Mnayo haki ya kushangilia, kwa sababu vitendo hivyo vya Serikali
vinaweza kuinua hali ya maisha ya Watanzania. Nasema, vinaweza. Sikusema lazima
vitainua maisha ya watanzania"
Mwalimu Julius Nyerere; Mei 1974.
No comments:
Post a Comment
Maoni yako